Shahidi akanusha kumchafua Mwanaharakati wa haki za kibinadamu kwenye gazeti la Jamhuri.

buswelu moja

JF-Expert Member
Aug 24, 2014
226
147
Mwandishi wetu, Arusha

Shahidi wa pili katika kesi inayowakabili wakazi wawili wa wilayani Ngorongoro mkoani Arusha pamoja na mhariri wa gazeti la Jamhuri, Manyerere Jackton ameileza mahakama kuwa hajahusika kumchafua wala kumshushia hadhi Mwanaharakati wa haki za kibinadamu na mkurugenzi mtendaji wa shirika lisilo la kiserikali la Pastoral Women's Council (PWC), Maanda Ngoitiko.

Shahidi huyo ambaye pia ni mkurugenzi wa shirika lisilo la kiserikali la Integrated Development People's Organization (KIDUPO), Gabriel Olle Killel alitoa ushahidi wake leo katika kesi ya madai nambari 88 ya mwaka 2017 inayomkabili yeye pamoja na wenzake watatu.

Mbele ya hakimu mkazi wa mahakama ya wilaya ya Arumeru, Hakimu Meena Shahidi huyo alisema kwamba katika gazeti hilo la jumanne tarehe 14 Hadi 20 mwaka 2016 lenye kichwa cha habari "atuzwa kwa kuichafua serikali " alieleza hakuhusika katika kuiandaa habari hiyo bali ni mwandishi wetu.

Shahidi huyo alieleza kwamba pamoja na kwamba jina lake kutajwa ndani ya habari na kwamba ndiye aliyeiandaa lakini hiyo haimaanishi kwamba yeye ndiye aliyeandika.

"Mheshimiwa hakimu pamoja na mimi kutajwa ndani ya habari hiyo kwamba mimi ndiye niliyeiandaa lakini haimaanishi kuwa ndio nimeiandika anayepaswa kutoa maelezo ni mwandishi wetu "aliieleza mahakama

Akiulizwa swali na Wakili upande wa mashtaka, Shilinde Ngalula kwamba anamtambua Maanda Ngoitiko Shahidi huyo alidai hamtambui zaidi ya kumjulia mahakamani hapo.

Wakili Ngalula alimpatia mshtakiwa huyo kielelezo cha ambacho ni nakala ya gazeti la Jamhuri asome aya ya mwisho na kumuuliza nani ametajwa kuandaa taarifa hiyo ndani ya aya hiyo Shahidi huyo alisoma na kisha kueleza kuwa yeye na mshtakiwa wa kwanza,William Alias wametajwa kuiandaa lakini haimaanishi wao ndio waliandika taarifa hiyo.

Hatahivyo, Shahidi huyo akiongozwa na wakili wake, Daud Haraka aliieleza mahakama hiyo kuwa ana watoto wawili lakini hana mke na hapo awali alikuwa padri wa kanisa katoliki nchini kabla ya kuamua kuacha kazi hiyo kwa matakwa yake binafsi.

Mara baada ya maelezo hayo ndipo hakimu anayesikiliza Shauri hilo aliamua kuihairisha Hadi Februari 19 mwaka huu ambapo Shahidi wa tatu atafika mbele ya mahakama hiyo kuwasilisha ushahidi wake.

Katika kesi hiyo inayovuta hisia mbalimbali kwa wakazi wa mkoani Arusha Maanda Ngoitiko anadai fidia ya kiasi cha sh, 2 bilioni kwa kuchafuliwa jina lake, kushushiwa hadhi yake mbele ya jamii jambo ambalo limempelekea usumbufu wa kukamatwa mara kwa mara na jeshi la polisi nchini, kunyang'anywa hati yake ya kusafiria na kisha kuhojiwa na idara ya uhamiaji nchini.

Mbali na madai hayo Mwanaharakati huyo anadai mbele ya mahakama hiyo kwamba habari zilizochapishwa na gazeti hilo imepelekea usumbufu kwa wafadhili wa taasisi yake ambao ni Flora Foundation ya nchini Marekani kutoliamini shirika lake kwa kuhisi kwamba yeye ni mwizi na anafuja fedha hovyo za taasisi anayoisimamia.

Katika kesi hiyo washtakiwa wengine ni mhariri wa gazeti la Jamhuri, Jackton Manyerere ambaye ni mshatakiwa wa tatu pamoja na mhariri mtendaji wa gazeti hilo, Deodatus Balile ambaye ni mshtakiwa wa nne.

Mwisho.

Picha ya kwanza ni Mwanaharakati, Maanda Ngoitiko aliyefungua kesi.

Picha ya pili ni mshatakiwa wa pili katika kesi hiyo, Gabriel Olle Killel akibadilishana nakala mbalimbali za kesi hiyo na Wakili wake, Daud Haraka nje ya mahakama ya wilaya ya Arumeru.

Picha ya tatu ni hati ya mashtaka ya kesi hiyo.
IMG_20200116_193441_561.JPG
IMG_20200116_121442.jpeg
IMG_20200116_093735.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom