Shahidi aeleza Sabaya alivyogawa Rushwa ya milioni 90 Kwa vijana wake

Jembe Jembe

JF-Expert Member
Jun 9, 2016
749
1,797
Shahidi wa 13 katika kesi ya Uhujumu Uchumi inayomkabili Aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai ,Lengai Ole Sabaya(34) na wenzake sita, Ramadhani Juma (39) ameieleza Mahakama kuwa Sabaya alipochukuwa Rushwa ya shilingi milioni 90 kutoka kwa Francis Mrosso aligawa posho ya kazi nzuri kwa vijana wake kiasi Cha sh,300,000 hadi milioni 2.2.


Pia walienda kujipongeza kwa kula na kunywa na vijana wake katika Aim Shooping More iliyopo karibu na ofisi za Shirika la Hifadhi za Taifa{TANAPA} na baadae saa 2 usiku walihamua Katika hotel ya Tulia Lodge Sakini Jijini la Arusha.



Juma ambaye alikuwa Kiongozi Mkuu wa Kikosi kazi cha Upelelezi kilichoshirikisha makachero wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa {TAKUKURU} naJeshi la Polisi Kituo Kikuu cha Polisi Arusha alidai hayo wakati akiongozwa na Mwendesha Mashitaka Mwandamizi wa Serikali Felix Kwetukia mbele ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Arusha,Patricia Kisinda.



Shahidi huyo alidai kuwa katika uchunguzi na upelelezi wa awali ulioshirikisha baadhi ya watuhumiwa akiwemo John Odemba mshitakiwa wa nne katika kesi hiyo Jackson Macha mshitakiwa wa Sita na Nathani Msuya mshitakiwa wa saba walikiri kutumwa na Sabaya na walipewa Rushwa ya shilingi milioni 90 na walimpelekea Sabaya fedha zote akiwa Aim Shooping More alipokuwa akiwasubiri.



Juma ambaye pia ni Afisa Upelelezi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoani Arusha alidai kuwa watuhumiwa hao walikiri na kueleza kuwa walipewa chakula na vinywaji hapo Aim Shooping More na baada ya kazi hiyo saa 2 usiku walipelekwa kupumzika katika Lodge ya Tulia iliyopo Sakina ndani ya Jiji la Arusha.



Shahidi huyo alidai watuhumiwa hao walieleza mgao wa fedha ulivyotolewa na Sabaya baada ya kukabidhiwa na kuweka fedha hizo zilizokuwa katika box kwenye buti ya gari ya serikali STL 5434 ambapo mgao huo ni pamoja na John Odemba alipewa shilingi 300,000 Sadiq Kiiza ambaye hayupo katika mashitaka hayo alipewa shilingi 450,000.



Wengine waliopewa mgao wa shilingi milioni 90 ni pamoja na Mshitakiwa wa saba Nathani Msuya alipewa shilingi 500,000,Mshitakiwa wa tatu Watson Mwahomange alikabidhiwa shilingi 600,000 ,Mshitakiwa wa pili,Enock Mnkeni alipewa mshiko wa shilingi milioni 1.5 ,Slyvester Nyegu mshitakiwa wa tano yeye alipewa kitita cha shilingi milioni 2.2 na Jackson Macha mshitakiwa wa sita alipewa mshiko wa shilingi milioni 1.4



Shahidi Juma alidai kuwa katika uchunguzi wao na taarifa za baadhi ya watuhumiwa walibaini kuwa Sabaya alikodisha chumba Tulia Lodge na siku hiyo ya januari 22 mwaka huu majira ya saa 2 usiku alimwamuru dereva wake akapaki gari ya serikali na dereva alifanya hivyo.



Alidai katika uchunguzi na upelelezi wao waligundua kuwa Mrosso alikwenda benki ya CRDB Tawi la Kwa Mrombo akiwa chini ya ulinzi wa vijana wa sabaya Jackson Macha,Nathan Msuya na John Odemba na kutoa fedha shilingi milioni 90.



Juma alidai waligundua hilo kupitia benk slip ya kutoa ya CRDB ya januari 22 mwaka huu,Taarifa ya akaunti ya Mrosso{Benk statement} vyote alipewa na meneja wa Benki hiyo ikiwa ni sehemu ya nyaraka katika kesi hiyo ambavyo vimepokelewa kama vielelezo katika kesi hiyo.



Hata hivyo Mawakili wa Utetezi wakiongozwa na Mosses Mahuna walipinga shahidi huyo kuichambua video ya CCTV Camera ya CRDB kwa Mrombo kwa madai kuwa yeye sio mtaalamu hatua iliyopingwa na waendesha mashitaka wakiongozwa na Kwetukia ambaye alidai shahidi huyo ni mpelelezi mkuu katika kesi hiyo na baada ya malumbano hayo Hakimu alihairisha kesi hadi disemba 29 mwaka huu ndipo atatoa maamuzi madogo na kesi hiyo na shahidi kuendelea kutoa Ushahidi.


Sabaya na wenzake wamerejeshwa Katika makazi yak Katika Gereza kuu la Arusha,Kisongo kusubiri kuendelea na uamuzi mdogo Katika shauri Hilo.


Ends..


IMG-20211218-WA0015.jpg
 
Hivi huyu Sabaya alikuwa binadamu au mnyama? Naomba kwa hiki apigwe mvua miaka 60 kabisa.
 
Hivi huyu Sabaya alikuwa binadamu au mnyama? Naomba kwa hiki apigwe mvua miaka 60 kabisa.
Sir Baya,
Huyu alipewa Ukuu wa Wilaya baada ya "Jamaa" kumuona anafaa katika kazi zake atakazokua akimtuma. Kifupi Jamaa kwanza kwa roho yake alipelekwa Hai "Strategically" kumshughulikia mti, halafu pili ndo hivyo awe anazipiga piga hizikwa niaba.
 
Back
Top Bottom