Shahidi aeleza jinsi alivyokaa siku 10 bila kula.

Bujibuji Simba Nyamaume

JF-Expert Member
Feb 4, 2009
74,870
155,831
Dar es Salaam. Mohamed Ling'wenya, shahidi wa pili upande wa utetezi katika kesi ndogo ndani ya kesi ya msingi inayomkabili mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na wenzake amedai hakula chakula siku kumi akiwa katika kituo cha polisi Mbweni.
Shahidi huyo amedai alifikishwa kituo cha polisi Mbweni Agosti 9, 2020 hadi Agosti 19, 2020 alipofikishwa mahakama ya Kisutu ndipo alikula ugali na dagaa.
Soma zaidi: Utata waibuka alipo mtuhumiwa kesi ya kina Mbowe
Ling'wenya ametoa madai yake leo Jumanne Septemba 27, 2021 katika mahakama kuu divisheni ya makosa ya rushwa na uhujumu uchumi wakati akitoa ushahidi wake katika kesi hiyo ndogo.
Mbali na Mbowe ambaye ni mshtakiwa wa nne na Mohamed, wengine katika kesi hiyo namba 16 ya mwaka 2021 ni Halfan Bwire Hassan na Adamu Hassan Kasekwa .
Soma zaidi: Shahidi kesi ya Mbowe aeleza alivyoshinda njaa siku kumi polisi
Akihojiwa na wakili wa Mbowe, Peter Kibatala, shahidi huyo alidai kuwa alifikishwa kituo cha Polisi Mbweni Agosti 9, 2020 akitokea kituo cha Tazara na kwamba muda wote aliokaa mahabusu katika kituo hicho takribani siku kumi hakuwahi kula chakula.
Jibu hilo lilimfanya wakili Kibatala kubakia njia panda asiamini huku Jaji Siyani naye akisema kuwa anapata shida kurekodi moja kwa moja jibu hilo.
Sehemu ya mahojiano kati ya Kibatala na shahidi huyo yalikuwa kama ifuatavyo:
Wakili:
Shahidi, mlipokuwa katika kituo cha Polisi Mbweni, hali ya Adamu (mshtakiwa wa pili) ilikuwaje?

Shahidi: Haikuwa nzuri maana alikuwa hali.
Wakili: Wewe ulijuaje kama alikuwa hali?
Shahidi: Kama mimi nilikuwa sili lazima hata yeye alikuwa hali.
Wakili: Kwani ulipokuwa kituo cha Mbweni ulikula mara ngapi?
Shahidi: Mimi sikula tangu nilipofikishwa hapo tarehe 9, mwezi wa Nane hadi nilipopelekwa mahakamani tarehe 19, mwezi wa Nane, 2020 ndipo nikala chakula.
Soma zaidi: Boaz, Kingai kizimbani kesi ya Mbowe
Wakili: Siku zote hizo?
Shahidi: Ndio, siku zote hizo sikula chakula.
Wakili: Mimi mwenyewe ni kwa uzoefu wa kazi lakini napata shida kidogo katika hilo.
Shahidi: Ni kweli.
Jaji Siyani: Kwa hiyo mimi niandike hukula siku 10? ameuliza jaji, huku akitabasamu kidogo, baada ya kimya kidogo akimwangalia shahidi
Shahidi: Ndio Mheshimiwa Jaji, nilikula siku tuliyopelekwa mahakamani.
Wakili: Vipi hali ya maji pale mahabusu yalikuwa yanapatikana?
Shahidi; Ndio mle kulikuwa na bomba
Wakili: Shahidi, mimi bado napata shida kubwa, kutoka tarehe 9 mwezi wa Nane mpaka tarehe 19, huli unakunywa maji tu, hebu iweke sawa Mahakama.
Shahidi: Nikisema hatujala, yaani wahusika hawajatupatia chakula cha kisheria (chakula cha mahabusu). Yaani walisema sisi ni mahabusu special hivyo kwenye selo yetu hawakuja.
Wakili: Hebu iambie mahakama ukiwa pale Mbweni, kuna chochote cha msaada ulichopata kama chakula?
Shahidi: Mbweni nilikuwa napewa msaada tu na yule Koplo (aliyemtaja awali kuwa baadaye walikuwa karibu naye) lakini si chakula cha mahabusu.
Wakili: Angalau sasa napata amani kwamba ulikuwa unapata chakula cha msaada.
Baada ya kumaliza kuhojiwa na wakili Kibatala, shahidi huyo sasa anahojiwa na upande wa mashtaka.
Source:- Mwananchi
 
Kuna watu wanakaribia kuwa wateja wa ICC kwa uhalifu dhidi ya binadamu.
 
Haya mambo yasikie kwa mwenzio, unaweza kusema mimi nililiwa na simba mpaka nikaisha kabisa na ukaona uko sawa.
 
Halafu ili kufanikisha hilo lengo la kumnyima chakula, wakimuingiza kituoni mtuhumiwa kwanza wanampa jina feki ili ndugu zake wakija kumuulizia mtu wao waambiwe hapa hayupo, baada ya hapo ndio mtuhumiwa anakosa msaada wa chakula huku akiendelea kupokea dozi ya mateso ya kila aina kila siku.
 
Gaidi ni mtu hatari mno ,nashangaa wanamchelewesha kumtwanga mvua 30

😂😂!

IMG_20210928_212038_069.jpg
 
Dar es Salaam. Mohamed Ling'wenya, shahidi wa pili upande wa utetezi katika kesi ndogo ndani ya kesi ya msingi inayomkabili mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na wenzake amedai hakula chakula siku kumi akiwa katika kituo cha polisi Mbweni.
Shahidi huyo amedai alifikishwa kituo cha polisi Mbweni Agosti 9, 2020 hadi Agosti 19, 2020 alipofikishwa mahakama ya Kisutu ndipo alikula ugali na dagaa.
Soma zaidi: Utata waibuka alipo mtuhumiwa kesi ya kina Mbowe
Ling'wenya ametoa madai yake leo Jumanne Septemba 27, 2021 katika mahakama kuu divisheni ya makosa ya rushwa na uhujumu uchumi wakati akitoa ushahidi wake katika kesi hiyo ndogo.
Mbali na Mbowe ambaye ni mshtakiwa wa nne na Mohamed, wengine katika kesi hiyo namba 16 ya mwaka 2021 ni Halfan Bwire Hassan na Adamu Hassan Kasekwa .
Soma zaidi: Shahidi kesi ya Mbowe aeleza alivyoshinda njaa siku kumi polisi
Akihojiwa na wakili wa Mbowe, Peter Kibatala, shahidi huyo alidai kuwa alifikishwa kituo cha Polisi Mbweni Agosti 9, 2020 akitokea kituo cha Tazara na kwamba muda wote aliokaa mahabusu katika kituo hicho takribani siku kumi hakuwahi kula chakula.
Jibu hilo lilimfanya wakili Kibatala kubakia njia panda asiamini huku Jaji Siyani naye akisema kuwa anapata shida kurekodi moja kwa moja jibu hilo.
Sehemu ya mahojiano kati ya Kibatala na shahidi huyo yalikuwa kama ifuatavyo:
Wakili:
Shahidi, mlipokuwa katika kituo cha Polisi Mbweni, hali ya Adamu (mshtakiwa wa pili) ilikuwaje?

Shahidi: Haikuwa nzuri maana alikuwa hali.
Wakili: Wewe ulijuaje kama alikuwa hali?
Shahidi: Kama mimi nilikuwa sili lazima hata yeye alikuwa hali.
Wakili: Kwani ulipokuwa kituo cha Mbweni ulikula mara ngapi?
Shahidi: Mimi sikula tangu nilipofikishwa hapo tarehe 9, mwezi wa Nane hadi nilipopelekwa mahakamani tarehe 19, mwezi wa Nane, 2020 ndipo nikala chakula.
Soma zaidi: Boaz, Kingai kizimbani kesi ya Mbowe
Wakili: Siku zote hizo?
Shahidi: Ndio, siku zote hizo sikula chakula.
Wakili: Mimi mwenyewe ni kwa uzoefu wa kazi lakini napata shida kidogo katika hilo.
Shahidi: Ni kweli.
Jaji Siyani: Kwa hiyo mimi niandike hukula siku 10? ameuliza jaji, huku akitabasamu kidogo, baada ya kimya kidogo akimwangalia shahidi
Shahidi: Ndio Mheshimiwa Jaji, nilikula siku tuliyopelekwa mahakamani.
Wakili: Vipi hali ya maji pale mahabusu yalikuwa yanapatikana?
Shahidi; Ndio mle kulikuwa na bomba
Wakili: Shahidi, mimi bado napata shida kubwa, kutoka tarehe 9 mwezi wa Nane mpaka tarehe 19, huli unakunywa maji tu, hebu iweke sawa Mahakama.
Shahidi: Nikisema hatujala, yaani wahusika hawajatupatia chakula cha kisheria (chakula cha mahabusu). Yaani walisema sisi ni mahabusu special hivyo kwenye selo yetu hawakuja.
Wakili: Hebu iambie mahakama ukiwa pale Mbweni, kuna chochote cha msaada ulichopata kama chakula?
Shahidi: Mbweni nilikuwa napewa msaada tu na yule Koplo (aliyemtaja awali kuwa baadaye walikuwa karibu naye) lakini si chakula cha mahabusu.
Wakili: Angalau sasa napata amani kwamba ulikuwa unapata chakula cha msaada.
Baada ya kumaliza kuhojiwa na wakili Kibatala, shahidi huyo sasa anahojiwa na upande wa mashtaka.
Source:- Mwananchi
Siku kumi tu analia ,Yesu alikaa siku 40 hakulalamika
 
Back
Top Bottom