Shahbaz Sharif, Waziri Mkuu mpya Pakistan

Lady Whistledown

JF-Expert Member
Aug 2, 2021
1,023
1,609
Bunge la Pakistan limemchagua Shahbaz Sharif kuwa Waziri Mkuu mpya wa nchi hiyo, baada ya Imran Khan kuondolewa madarakani kwa kura ya kutokuwa na imani naye mapema siku ya Jumapili Aprili 10, 2022.

Kiongozi wa muungano wa upinzani ambaye alikuwa amefanya kazi ya kumwondoa Khan alipata uungwaji mkono wa wengi Bungeni.

Shahbaz Sharif sasa ataunda Serikali mpya ambayo inaweza kusalia hadi uchaguzi utakapokamilika mnamo Agosti 2023.

Khan, mwenye umri wa miaka 69, alipigiwa kura ya kujiondoa baada ya siku kadhaa za drama kubwa ya kisiasa.

Alikuwa amejaribu kuzuia jaribio la awali la kuleta hoja ya kutokuwa na imani naye kwa kulivunja bunge na kuitisha uchaguzi wa haraka.

Hata hivyo, Mahakama ya Juu ya nchi hiyo iliunga mkono ombi la upinzani kwamba hatua zake ni kinyume na katiba na kuamuru kura ya kutokuwa na imani naye kuendelea.

Leo Jumatatu Aprili 11, 2022, Sharif alichaguliwa bungeni bila kupingwa na atakuwa Waziri Mkuu wa 23 wa Pakistan.

Mgombea mpinzani Shah Mahmood Qureshi alikuwa ametangaza kuwa chama chake cha Pakistan Tehreek-e-Insaf kilikuwa kikisusia kura ya ubunge na kufanya matembezi.

Chanzo: BBC
 
Huyo n nduguye na NAWAZ SHARIFF au? Ufafanuzi kidogo
Ndio,mdogo wake 👇

Screenshot_20220411-153955.png

Screenshot_20220411-154008.png
 
Bunge la Pakistan limemchagua Shahbaz Sharif kuwa Waziri Mkuu mpya wa nchi hiyo, baada ya Imran Khan kuondolewa madarakani kwa kura ya kutokuwa na imani naye mapema siku ya Jumapili Aprili 10, 2022.

Kiongozi wa muungano wa upinzani ambaye alikuwa amefanya kazi ya kumwondoa Khan alipata uungwaji mkono wa wengi Bungeni.

Shahbaz Sharif sasa ataunda Serikali mpya ambayo inaweza kusalia hadi uchaguzi utakapokamilika mnamo Agosti 2023.

Khan, mwenye umri wa miaka 69, alipigiwa kura ya kujiondoa baada ya siku kadhaa za drama kubwa ya kisiasa.

Alikuwa amejaribu kuzuia jaribio la awali la kuleta hoja ya kutokuwa na imani naye kwa kulivunja bunge na kuitisha uchaguzi wa haraka.

Hata hivyo, Mahakama ya Juu ya nchi hiyo iliunga mkono ombi la upinzani kwamba hatua zake ni kinyume na katiba na kuamuru kura ya kutokuwa na imani naye kuendelea.

Leo Jumatatu Aprili 11, 2022, Sharif alichaguliwa bungeni bila kupingwa na atakuwa Waziri Mkuu wa 23 wa Pakistan.

Mgombea mpinzani Shah Mahmood Qureshi alikuwa ametangaza kuwa chama chake cha Pakistan Tehreek-e-Insaf kilikuwa kikisusia kura ya ubunge na kufanya matembezi.

Chanzo: BBC
Tanzania bado ni majaliwa. Mzee wa "yupo ofisini anafanya kazi"
 
Imran Khan amejitakia mwenyewe aliwauzi Sana mabeberu alivojiunga na Putin Pakistan wananchi wanajielewa
Imran Khan amesahau historia, wakati Pakistan unapigana na India, USA na UK walimsaidia Pakistan.

Russia walimsaidia India

Unaona India amesimama na Russia...Yes
 
Back
Top Bottom