Shahada za Utaalam wa mazishi zatolewa UK

Richard

JF-Expert Member
Oct 23, 2006
14,939
20,399
Chuo kikuu cha Bath nchini Uingereza, kimeanzisha shahada ya mazishi.

Wahitimu watakuwa na ujuzi na utaalam wa mambo yote yanayohusu kushughulikia mwili wa marehemu mpaka unapopumzishwa kaburini.

Kozi hio itachukua miaka miwili ya awali (foundation course) na itakuwa na topics kama kutoa ushauri kwa wafiwa au mfiwa, sheria, huduma kwa wateja (wafiwa au mfiwa) na namna ya kuuteketeza mwili kwa moto.

Chuo kikuu cha Bath kiko katika mji uitwao Bristol uliopo kusini magharibi ya Uingereza na ni moja ya vyuo vikuu maarufu katika msimamo wa ligi ya vyuo nchini humo.

Kwa kawaida kuna makampuni yaitwayo (funeral directors ) ambayo hutoa vyeti tu mara mtu anapomaliza kozi fupi ya namna ya kuendesha shughuli za mazishi na ndio wenye leseni za kufanza shughuli hizo.

Haya basi wajasirimali wa pale nje ya hospitali ya Muhimbili mnaotengeneza majeneza, mnaweza kuinuka kimaisha kwa kuangalia njia kama hizi za kupata ujuzi zaidi.
 
Mazishi ni sherehe kama zilivyo sherehe nyingine tu mfano harusi kinacho leta mshangao hapa ni utamaduni wetu tu ila kama kwenye harusi kuna watu wamesomea ayo mambo kwa nini isiwe mazishi ingawa recently hata sisi tumeanza kufanya mazishi kama sherehe na tunaelekea uko kwa kasi.
 
Back
Top Bottom