Shahada ya kwanza ya Sheria(LL.B) pekee haimfanyi mtu kuwa na sifa ya kuwa Wakili

Abeto Malakoti

Senior Member
Feb 7, 2018
122
234
SHAHADA YA KWANZA YA SHERIA (LL.B) PEKEE HAIMFANYI MTU KUWA NA SIFA ZA KUWA WAKILI.

Kuna wanasheria na wanasiasa hata raia wa kawaida wanaamini au kuaminishwa kuwa kupata shahada ya kwanza ya sheria (LL.B) pekee inamfanya mtu kuwa na "sifa za kuwa wakili" kwa minajiri ya kuteuliwa ya kuteuliwa kuwa mwanasheria mkuu wa serikali. Watu wanaounga mkono hoja hii wanasema kuwa Dr. Kilangi alipata shahada ya kwanza ya sheria mwaka 2000 hivyo alikuwa na sifa za kuwa wakili kuanzia mwaka 2000, hii ikiwa na maana kwamba wakati anateuliwa kushika wadhifa wa mwanasheria mkuu tiyari alikuwa na zaidi ya miaka 15 akiwa na sifa za kuwa wakili. Wapinzani wa hoja hii wanasema kuwa Dr. Kilangi alipata sifa za kuwa wakili baada ya kufaulu bar examinations chini ya Baraza la Elimu ya sheria na kuwa wakili mwaka 2011 hivyo bado hajafikisha miaka 15 ya uwakili au ya kuwa na sifa za kuwa wakili. Maoni yangu kuhusu swala la shahada ya kwanza ya sheria kumpa mtu sifa za kuwa wakili ni kama ifuatavyo;

Ibara ya 59 (2) ya katiba imeweka masharti kuwa ili mtu ateulie kuwa mawanasheria mkuu wa serikali lazima awe "wakili" au awe na "sifa za kuwa wakili". Swala la kuwa "wakili" halina utata liko wazi mno na haliitaji mjadala kabisa na swala lenye utata ni mtu mwenye "sifa za kuwa wakili". Mtu mwenye shahada ya kwanza ya sheria hana kabisa "sifa za kuwa wakili" kwa sababu sheria mbili zinataja kwa uwazi mtu mwenye sifa za kuwa wakili katika jamhuri ya muungano wa Tanzania. Sheria zimeweka aina tano (5) za watu wenye sifa za kuwa wakili kama ifuatavyo;

Kwanza, "mtu mwenye Post-Graduate Diploma in Legal Practice" ambayo imetolewa na Law School of Tanzania ana sifa za kuwa wakili, hii ni kwa mujibu wa section 12 (3) of the Law School of Tanzania Act, 2007 (sheria Na. 18 ya 2007). Na mtu kamwe hawezi kupata Post-Graduate Diploma in Legal Practice" ambayo imetolewa na Law School of Tanzania mpaka awe na shahada ya sheria au sifa zingine za kitaalum ambazo zinatambuliwa na Baraza la Elimu ya Sheria (Council for Legal Education), hii ni kwa mujibu wa section 11 (1) (a) and (b) of the Law School of Tanzania Act, 2007

Pili, mtu ambaye ana shahada ya sheria ya sheria kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam au Chuo Kikuu cha Afrika Mashariki au chuo kikuu chochote ambacho kinatambuliwa na Baraza la Elimu ya Sheria na awe amefauli "Bar examinations" inayosimamiwa na Baraza la Elimu ya Sheria , na hii ni kwa mujibu wa Section 8 (1) (a) (i) and (b) (i) of the Advocate Act, Cap. 1.

Tatu, Mtu ambaye amekuwa wakili Zanziba, Kenya na Uganda kwa kipindi cha miaka 5 kabla ya siku ya kufanya maombi ya kuwa wakili, na hii ni kwa mujibu wa Section 8 (1) (a) (i) and (b) (i) of the Advocate Act, Cap. 1.

Nne, mtu ambaye ni wakili wa mahakama zisizokuwa na mipaka ya mamlaka katika maswala ya jinai na madai (court with unlimited civil and criminal jurisdiction) katika nchi za jumuia ya madola au nchi nyingine zilizoteuliwa na waziri wa sheria kwa ajiri hiyo, na hii ni kwa mujibu wa Section 8 (1) (a) (ii) of the Advocate Act, Cap. 1.

Tano, mtu ambaye ni solisita (solicitor) wa mahakama ya juu ya Uingereza (England), Northern Ireland, Jamhuri ya Ireland na Scotland (United Kingdom).

Hivyo basi, hitimisho langu ni kuwa mtu mwenye shahada ya sheria (LL.B) kamwe hawezi kuwa na sifa za kuwa wakili mpaka apate Post-Graduate Diploma in Legal Practice Kutoka Law School of Tanzania au afaulu mitihani inayosimamiwa na Baraza la Elimu ya Sheria (Council for Legal Education) au awe amekuwa wakili au solisita katika nchi za jumuia ya madola au awe amekuwa wakili katika Kenya, Zanzibar na Uganda kwa kipindi cha miaka mitano.

Zitto, Saint Ivuga
 
Abeto, japo sina vifungu ila Tanzania tuna sifa mbili za mawakili.
1. Watu wote wenye LL.B kabla ya kuanzishwa kwa Law school of Tanzania mwaka 2008, hivyo wahitimu wote wa LL.B kabla ya mwaka 2008, wana sifa za kuwa wakili. Wanachotakiwa kufanya ni kufanya bar exam
2. Wahitimu wote wa kuanzia mwaka 2008 sifa yao sasa ndio hivyo ya Post Graduate ya law school of Tanzania na zile sifa nyingine.

P
 
Mimi hapa sijui chochote kuhusu hii mada. Ila nisaidie kuna nini kimetokea hadi kuandika haya
 
Abeto, japo sina vifungu ila Tanzania tuna sifa mbili za mawakili.
1. Watu wote wenye LL.B kabla ya kuanzishwa kwa Law school of Tanzania mwaka 2008, hivyo wahitimu wote wa LL.B kabla ya mwaka 2008, wana sifa za kuwa wakili. Wanachotakiwa kufanya ni kufanya bar exam
2. Wahitimu wote wa kuanzia mwaka 2008 sifa yao sasa ndio hivyo ya Post Graduate ya law school of Tanzania na zile sifa nyingine.

P

Hiki unachosema ndo hicho hicho nimekiandika katika namba 1 na namba 2. Namba 1 ni kuhusu wanasheria wanaopata sifa za kuwa wakili kutokana na mitihani ya law school of tanzania. Na namba 2 ni kuhusu wanasheria wanaopata sifa za kuwa wakili kutokana Bar Exams inayosimamiwa na Council for Legal Education. Mimi na wewe tumesema kitu kile kile tofauti yetu ni kwamba mimi nimefanya rejea ya vifungu vya sheria husika na wewe haujafanya rejea kwenye vifungu vya sheria lakini sote mimi na wewe tuko sahihi kabisa. Na tofauti nyingine ni kwamba wewe unajua sifa 2 tu wakati sheria inaelekeza kuwa kuna sifa 5 za kumfanya mwanasheria kuwa wakili na kwa kila sifa nimefanya rejea kwenye vifungu vya sheria uhusika. Kuanzia sasa naomba ujue kuwa kuna sifa 5 za kumfanya mwanasheria kuwa wakili na sio 2. Utamu wa sheria ni kwamba unafanya reference kwenye vifungu vya sheria.
 
Nakubaliana na wewe class mate wangu wa sheria unajua tulisomea wapi na lini.
 
Kweni Dr Kilangi ni kilaza aliyependelewa ?
Hapa, Dr. Kilangi sio kilaza hata kidogo. Dr. Kilangi ni mwanasheria mwenye uwezo mkubwa sana, tena amebobea kwenye sheria za mafuta, gesi asilia na madini, ni mtu mwenye ueledi wa hali ya juu kabisa lakini kwa bahati mbaya inaonekana hana sifa za kikatiba kuwa mwanasheria mkuu wa serikali.
 
Hiki unachosema ndo hicho hicho nimekiandika katika namba 1 na namba 2. Namba 1 ni kuhusu wanasheria wanaopata sifa za kuwa wakili kutokana na mitihani ya law school of tanzania. Na namba 2 ni kuhusu wanasheria wanaopata sifa za kuwa wakili kutokana Bar Exams inayosimamiwa na Council for Legal Education. Mimi na wewe tumesema kitu kile kile tofauti yetu ni kwamba mimi nimefanya rejea ya vifungu vya sheria husika na wewe haujafanya rejea kwenye vifungu vya sheria lakini sote mimi na wewe tuko sahihi kabisa. Na tofauti nyingine ni kwamba wewe unajua sifa 2 tu wakati sheria inaelekeza kuwa kuna sifa 5 za kumfanya mwanasheria kuwa wakili na kwa kila sifa nimefanya rejea kwenye vifungu vya sheria uhusika. Kuanzia sasa naomba ujue kuwa kuna sifa 5 za kumfanya mwanasheria kuwa wakili na sio 2. Utamu wa sheria ni kwamba unafanya reference kwenye vifungu vya sheria.

Nyie wanasheria hebu turudi nyuma kidogo, Yule binti mtoto wa Mdee akiwa Bungeni alionyesha wasiwasi kwa waziri wa sheria kupita Bar exam kimizengwe hebu tupeni picha halisi likoje au ni figisufigisu zao za kisiasa?
 
Kwani Mdee alisemaje?
 
Abeto, japo sina vifungu ila Tanzania tuna sifa mbili za mawakili.
1. Watu wote wenye LL.B kabla ya kuanzishwa kwa Law school of Tanzania mwaka 2008, hivyo wahitimu wote wa LL.B kabla ya mwaka 2008, wana sifa za kuwa wakili. Wanachotakiwa kufanya ni kufanya bar exam
2. Wahitimu wote wa kuanzia mwaka 2008 sifa yao sasa ndio hivyo ya Post Graduate ya law school of Tanzania na zile sifa nyingine.

P
Au mtu yoyote hata asipokuwa na sifa, alimradi jaji Mkuu kaamua kumpa uwakili.
 
Au mtu yoyote hata asipokuwa na sifa, alimradi jaji Mkuu kaamua kumpa uwakili.
Hii ya mtu yoyote kiukweli mimi sikuijua, ila ya ma Barristers wa London, niliijua na ndiko alikoibukia Wakili Murtaza Lakha.

Ila kwenye mambo ya sheria kuna vitu vingi havifundishwi darasani, hivyo mimi wewe nakuona kama teacher, maana licha ya kupita pale miaka 4, kuna vitu sikuwahi kuvisikia vikifundishwa ndio nimejifunzia kwako.
Thanks

P.
 
Huyu anayesema mtu yoyote anaweza kupewa uwakili na jaji mkuu hakika ana misconception fulani kuhusu swala hili ingawa pia ana uelewa fulani kuhusu swala hili. Ngoja swala hili niliweke katika mukitadha sahihi. Hiko hivi, Council for Legal Education inayo mamlaka ya kumpatia mtu uwakili mwenye shahada ya kwanza ya sheria bila kufanya Bar Exams, Council for Legal Education possesses legal mandate to exempt any holder of LL.B (Bachelor of Laws) from requirement of sitting for, and passing bar exams, hii ni kwa mujibu wa section 8 (1 A) of the Advocate Act, Cap. 341. Jaji Mkuu hana kabisa mamlaka ya kumpatia mtu uwakili atakeyoona anafaa na hana mamlaka ya kumpatia mtu exemption ya bar exams. Mamlaka ya kumpatia mtu exemption ya bar exams yako mikononi mwa Council for Legal Education na hiyo exemption inatolewa kwa mtu mwenye shahada ya kwanza ya sheria na sio kwa kila mtu, hiyo exemption haiwezi kutolewa kwa mtu mwenye shahada ya sociology au economics. Jaji mkuu yeye ni mjumbe tu wa Council for Legal Education ambayo ina wajumbe 5 tu, hii ni kwa mujibu wa section 5 A (1) of the Advocate Act, Cap. 341., hivyo Jaji Mkuu pekee bila ridhaa ya wajumbe wengine 4 hawezi kutoa exemption na kumruhusu mtu kuwa wakili bila kufanya Bar Exams, ingawa kwa nafasi yake ana ushawishi mkubwa kwenye Council.

Pascal Mayalla
 
5 Reactions
Reply
Back
Top Bottom