Elections 2010 Shahada na masanduku ya ziada yaandaliwa kuiba kura

Ex Spy

JF-Expert Member
Jan 15, 2007
213
1,726
Kuna taarifa kwamba kikao kimoja kimefanyika leo na watu wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) wamepewa jukumu la kuandaa karatasi za ziada za kupigia kura na masanduku.

Kikao hicho kimefanyika (mahala tunapahifadhi kwa sasaa) na aliyekabidhiwa ni mwanamama mmoja mwenye jina linaloanza na herufi R na la pili S yaani (RS) wa Kurugenzi ya Mipango TAMISEMI.

More to come
 
this was expected na ndio maana wali-procure mapema ili kupata samples za ballot papers

sasa wasimamizi wa wapinzani wakae mkao wa kula
 
Hivi kuna "KAMATI YA KUIBA KURA" ndani ya sisi em? Na wanalipwa na kodi zetu?
 
Hivi watanzania tumerogwa na nani badala ya kufanya kampeni ya nguvu tunategemea kuiba kura, haya mambo ni serious leo tunayachekea lakini ndiyo huwa yanaleta umwagaji wa damu sehemu nyingi duniani. Aaaaaaaaaa kama watataka tufike huko sawa lakini wajue kila mtu ana roho moja sidhani kama wao wanazo mbili kuwa wakifa leo kesho wanarudi.

Tatizo lingine ni hawa wanaoitwa ma external observer leo hawajali kinachoendelea wanasubiri hadi tuanze kukatana mapanga ka Kenya ndo waje eti kusuluhisha to hell with them why shouldn't act now. Na baadhi yao wanapewa taarifa kama hizi lakini wanasema hayo ni mambo ya ndani lakini siku ya uchaguzi sijui ndo yanakuwa mambo ya nje. But anyone who is involved will one day pay the price.
 
Hivi kuna "KAMATI YA KUIBA KURA" ndani ya sisi em? Na wanalipwa na kodi zetu?

Habari nilizonazo ni hizi: CCM wengi wanajiamini kushinda... lakini bado kuna baadhi (haswa Kikwete na Lowassa) wana wasiwasi ... Kuingia kwa Slaa kumewapa kisebusebu sana! Kikwete wasiwasi wake ni kungolewa na Slaa, japo wengi wanamtuliza na kumwambia haitawezekana.

Lowassa yeye wasiwasi wake ni kuwa japo CCM itashinda, lakini huenda ikawa kwa kura kiduchu. Na hiki ndicho kitu ambacho hataki kabisa kabisa kitokee kwani anaona 2015 inaweza kula kwake. Kuna mikakati ya hapa na pale inafanyika ili kwa udi na uvumba CCM ishinde kwa kishindo.... nia ikiwa ni kuwafanya watanzania wakate tamaa kabisa na upinzani.

Na vilevile kuna mamluki kibao wame/wana-cross kwenda CHADEMA, ili baada ya uchaguzi watumike kukibomoa kama ilivyokuwa NCCR mageuzi.
 
Kama CCM waliweza kufanyiana faulo wenyewe kwa wenyewe ni wazi mwaka huu tutashuhudia ukiukwaji mkubwa wa taratibu za Uchaguzi Mkuu na dalili zimeanza kuonekana mapema kabisa.

Kwamba huko Singida mtoto wa mhujumu moja ameweza kuwaengua wazalendo wanne kwenye kinyang'anyiro kwa kuwawekea pingamizi zisizo na kichwa wala miguu ni jambo la kusikitisha kwa kweli.

Hivyo Judge Lewis Makame, mwenyekiti wa tume ya uchaguzi, akae akijua kuwa kama machafuko yatatokea ni yeye atawajibika and he wont get off so easily kama mwenzake Kiviutu wa Kenya mwaka 2008.

Mungu atuepushie mbali !!
 
Hivi hawa wanaoshinda kwa kuiba kura wanaweza kuwa na moral authority kweli ya kuongoza nchi...

Inasikitisha sana kuona chama kinachojivunia mtandao wa wanachama hadi ngazi ya kijiji inatumia mabillioni na bado inahitaji ushindi kwa njia ya wizi. Ni wazi kuwa hofu yao inashadidiwa na ukweli kuwa wanajua wananchi wamewachoka na hawajaweza kabisa kufikia japo nusu ya matarajio ya wananchi.
 
Mkuu, hivi vifaa vishaingia nchini tayari? Basi this' a terrible mistake!
sina hakika kama vishavuka customs ila najua procurement ilishafanyika kitambo and more likely sample watu walishapokea

si unajua product lazma ikaguliwe?
 
Wajaribu kwenye jimbo langu waone. Mtu atondolewa shingo nakwambia. Ninaahidi kulinda kura zangu kunguvu zangu zote na akili zangu zote na roho yangu yote.

Haya basi wajaribu waone. Walishazoea sasa ndio mwisho wa game. Nasema sasa ndio mwisho wa game ati.

Hakuna askari kujaribu game hili. Tutamalizana nakwambia.
 
Wakimaliza kuandaa hayo makaratasi, wachimbe na mahandaki kabisa, no wonder wanazimia zimia kila mahali
 
Wajaribu kwenye jimbo langu waone. Mtu atondolewa shingo nakwambia. Ninaahidi kulinda kura zangu kunguvu zangu zote na akili zangu zote na roho yangu yote.

Haya basi wajaribu waone. Walishazoea sasa ndio mwisho wa game. Nasema sasa ndio mwisho wa game ati.

Hakuna askari kujaribu game hili. Tutamalizana nakwambia.

Ni vigumu kuwakata shingo. watakukata wewe usipokuwa mwangalifu. Tena wanaweza kukuondoa kilaini na ukakubali matokeo. ila vizuri na wewe ukapanga mkakati wa kuwaibia
 
Wajaribu kwenye jimbo langu waone. Mtu atondolewa shingo nakwambia. Ninaahidi kulinda kura zangu kunguvu zangu zote na akili zangu zote na roho yangu yote.

Haya basi wajaribu waone. Walishazoea sasa ndio mwisho wa game. Nasema sasa ndio mwisho wa game ati.

Hakuna askari kujaribu game hili. Tutamalizana nakwambia.

I like this much confidence and boldness my broda!

Sasa nyie akina MF, sambazeni habari katika majimbo yote kuwa kuna hatari kubwa sana ya wizi ili wote wakae mkao wa "moto-stuka"!

Hao wameshajigundua kuwa bila uchakachuaji watakuwa flat!..huh!
 
Umenena lililo la kweli. Habari hizi zisiishie JF,zinatakiwa nienee kama kimbunga kuwa kuna mpango kabambe umeandaliwa kuwaibia kura zao wananchi ili wajiandae kuzilinda mapema sio kusubiri uchakachuaji ushafanyika kisha kulalamika.

Mwaka huu hakuna kulalamika ila mpaka kieleweke. Wameshatuona wapuuzi sana kwa muda mrefu. Hawawezi kutuibia rasilimali zetu, uhuru wetu na sasa na kura zetu na sie tunaangalia tu kama mazezeta. Upuuzi mkubwa. Its 2010 or never
 
Haoooo...taratiiibu wanatafuta VISINGIZIO... kwa hali mlinoyo hamuhitaji hata kuibiwa,,sawa sawa kumsukuma mlevi....
teh teh teh...........
 
Back
Top Bottom