Shaffih Dauda & Co. acheni uzandiki wenu wa kuiandama Yanga..... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Shaffih Dauda & Co. acheni uzandiki wenu wa kuiandama Yanga.....

Discussion in 'Sports' started by Balantanda, Apr 21, 2012.

 1. Balantanda

  Balantanda JF-Expert Member

  #1
  Apr 21, 2012
  Joined: Jul 13, 2008
  Messages: 12,322
  Likes Received: 1,039
  Trophy Points: 280
  Kwa muda mrefu sasa nimeshangazwa na propaganda chafu zinazoenezwa na Shaffih Dauda kupitia blog yake pamoja na kipindi cha Sports Extra cha Clouds FM dhidi ya timu ya Yanga.....Shaffih na wenzake akina Ibrahim Masoud ''Maestro'(ambaye ni kiongozi wa watani zetu Simba) kwa muda mrefu sasa wamekuwa wakiisakama Yanga kupitia blog hiyo na Redio kiasi cha kusema kwamba Yanga inakufa sasa.....

  Nataka tu kumwambia Shaffi na wenzake Maestro,Jeff Leya na Alex(Luambano) kwamba pamoja na uzishi na fitna zao Yanga kamwe haitakufa,kutokufanya vizuri mwaka huu si kigezo cha kuitabiria kifo Yanga na akumbuke kwamba Yanga sasa hivi iashika nafasi ya 3 na si ya mwisho wala ya 2 ama 3 kutoka mwishoni sasa iweje awaalike akina Mwaisabula na kuanza kuitabiria Yanga kifo?.....Yanga imeanzishwa mwaka 1935 na bado ipo na itaendelea kuwepo......

  Ni upuuzi kuisakama timu ambayo inashika nafasi ya 3 katika msimamo wa ligi na ambayo bado inaweza hata kushika nafasi ya 2......Msimu wa mwaka 1989 Simba iliponea chupuchupu kushuka daraja katika ligi daraja la kwanza lakini hakuna mtu aliyeitabiria Simba kifo.......Chuki binafsi hazijengi,zinabomoa...

  Shaffih na Clouds wanaweza kufanya mambo mengi tu mengine badala ya kutwa kucha kuisakama Yanga kwa sababu tu imepoteza mechi 2......Eti 'MWAISABULA AFUNGUKA: AELEZA SABABU ZA KIFO CHA YANGA'.....Yaani Yanga ife kwa kupoteza mechi na Toto Africans na Kagera Sugar!!!!......Ama kwao Clouds timu kushika nafasi ya 3 ni kiashiria cha kushuka daraja...Yanga ina mechi tatu kumaliza ligi na ikishinda zote inaweza kushika nafasi ya 2....

  Shaffih Dauda in Sports.: MTANGAZAJI WA SPORTS XTRA/BAR YA CLOUDS FM/TV ATIMULIWA NA WANACHAMA KWENYE PRESS CONFERENCE YA YANGA!

  Shaffih Dauda in Sports.: KAMATI YA TIBAIGANA YAITUPILIA MBALI RUFAA YA YANGA.

  Shaffih Dauda in Sports.: OFFICIAL: RUFAA YA YANGA YAPIGWA CHINI !

  Shaffih Dauda in Sports.: SIMBA YAZIDI KUCHANUA MAKUCHA NA KUTAMBA KILELENI - YANGA YAPIGWA TENA HUKO KAGERA

  Shaffih Dauda in Sports.: MATUKIO YA PICHA UWANJA WA KAITABA YANGA NA KAGERA SUGAR

  Shaffih Dauda in Sports.: BAADA YA RUFAA YAO KUTUPWA - YANGA WATAFAKARI CHA KUFANYA

  Shaffih Dauda in Sports.: KENNY MWAISABULA AFUNGUKA: AELEZEA SABABU ZA KIFO CHA YANGA -PART 1

  Shaffih Dauda in Sports.: KENNY MWAISABULA AFUNGUKA: AELEZEA SABABU ZA KIFO CHA YANGA -PART II

  Shaffih Dauda in Sports.: KENNY MWAISABULA AFUNGUKA: AELEZEA SABABU ZA KIFO CHA YANGA -PART III

  Shaffih Dauda in Sports.: WASIKILIZE BAKARI MALIMA ' JEMBE ULAYA ' NA MDAU HEAVY D JUU YA YANGA.

  Tunajua kwamba mmeamua kuisakama Yanga kwa kujipendekeza TFF ili mpatiwe tenda ya kutengeneza tiketi kwa ajili ya mechi za ligi kuu.....  Yanga: Daima Mbele, Nyuma Mwiko
   
 2. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #2
  Apr 21, 2012
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Bala

  Yanga wamepoteza dira mtani, kuna viongozi pale wanaongoza yanga kishabiki kama tuko seventies... for Yanga kubadilika lazima waandamwe

  wakibembelezwa usitegemee chochote mtani
   
 3. Balantanda

  Balantanda JF-Expert Member

  #3
  Apr 21, 2012
  Joined: Jul 13, 2008
  Messages: 12,322
  Likes Received: 1,039
  Trophy Points: 280
  Suala la tatizo la uongozi ninalijua sana cuz.....Na hata hapa nililieleza

  Tatizo ni hawa vijana wa Clouds wanaojifanya wajuaji kiasi cha kuonesha mahaba ya waziwazi kwa lengo wanalolijua wao....Wanafikia hata hatua ya kuitabiria Yanga kifo....

  Hivi umepata muda wa kuwasikiliza hawa Clouds na mada zao zinazoihusu Yanga?....Wanaiongelea Yanga as if inashika nafasi ya mwisho ama ya 2 toka mwisho.....
   
 4. Boflo

  Boflo JF-Expert Member

  #4
  Apr 21, 2012
  Joined: Jan 20, 2010
  Messages: 4,394
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Kumbe Bala ww Yanga !! Mimi napenda Simba timu ya waarabu...
   
 5. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #5
  Apr 21, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Kandambili anapochukia ukweli!
   
 6. M

  Masuke JF-Expert Member

  #6
  Apr 21, 2012
  Joined: Feb 28, 2008
  Messages: 4,606
  Likes Received: 108
  Trophy Points: 160
  Mtani Balatanda relax, hawa jamaa ndo walivyo timu ikifanya vibaya, ungewasikia siku ile Simba imepigwa tatu na wale waarabu wa Algeria kabla Okwi hajafunga goli lililoipa Simba nafasi ya kusonga mbele kama wewe ni mshabiki wa Simba ungeweza kuzima redio, hata kipindi kile cha timu ya Taifa ilivyopigwa tano Misri huwezi amini kama redio iliyokuwa inatangazwa inafanya biashara na watanzania au imepewa leseni na serikali ya Tanzania, mimi nishawazoea wakianza kutangaza habari ambazo sipendi kuzisikia nahamisha stesheni, Kidogo Ibrahim Masoud huwa anajizuia habari mbaya zinazoihusu Simba nadhan kwa sababu ni Kiongozi lakini waliobaki timu yoyote ikifanya vibaya kama unaishabikia ukiwasikiliza sana unaweza kuihama dawa ni kubadili tu radio stesheni na kutotembelea blog yao mara kwa mara.
   
 7. ndetichia

  ndetichia JF-Expert Member

  #7
  Apr 21, 2012
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 27,641
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  hao ndio wataalam wa soka tanzania na wasemaji wa tff na wasemaji wa soka la tz na kama umewafuatilia zaidi wakitoa analysis za kukopi tokea goal.com na supersport ndio wanajiona wao ndio kila kitu bongo ngoja tuone..
   
 8. Faru Kabula

  Faru Kabula JF-Expert Member

  #8
  Apr 21, 2012
  Joined: Mar 26, 2009
  Messages: 10,655
  Likes Received: 2,897
  Trophy Points: 280
  Asante kwa kuniwekea link ya picha za Bukoba
   
 9. CHAI CHUNGU

  CHAI CHUNGU JF-Expert Member

  #9
  Apr 21, 2012
  Joined: Feb 20, 2012
  Messages: 7,160
  Likes Received: 107
  Trophy Points: 160
  Hawa jamaa clouds ni wazandiki sana!
  Tena mm nishawapotezea kitambo tuu.
  Radio ya kishabiki sana ile kwenye upande wa michezo,imejaa usimba na uazam tupu.
   
 10. Ulukolokwitanga

  Ulukolokwitanga JF-Expert Member

  #10
  Apr 21, 2012
  Joined: Sep 18, 2010
  Messages: 8,418
  Likes Received: 3,905
  Trophy Points: 280
  Hii nchi kila mtu ni futbol analyst tatizo ni mahala pa kusemea. Ukibahatika kupata pa kusemea kama Shafii na wenzie si haba kwani wavivu wa kusoma wote utawapata. Mwakani utasikia akina Shafii wako kamati ya ligi kisa tu kutoa analysis za uongo na kuwapamba viongozi wa TFF. Muda si mrefu tunakamata namba 200 katika rank za fifa maana usanii haulipi kimataifa
   
 11. yahoo

  yahoo JF-Expert Member

  #11
  Apr 21, 2012
  Joined: Sep 9, 2011
  Messages: 3,424
  Likes Received: 363
  Trophy Points: 180
  Jamani kazi ya waandishi ni kuuarifu uma juu ya kilichotokea kwenye jamii kama tunavoona kwenye stations za walioendelea,angalau kama hujui english pata mfano kutoka bbc swahili,dochivere, sauti ya ujerumani nk.TUkirudi kWa haWA jamaa wa clouds ,wapo tofauti wao Wanafanya kazi kishabiki,na kutoa amri na maelekezo juu ya matukio mbalimbali haswa kwa masrai ya simba ambao wana masrahi nao.
   
 12. yahoo

  yahoo JF-Expert Member

  #12
  Apr 22, 2012
  Joined: Sep 9, 2011
  Messages: 3,424
  Likes Received: 363
  Trophy Points: 180
  Tegete ni mhanga wa hii mijamaa,maskini kosa la kuingia uwanjani amehukumiwa sawasawa na aliyempiga refa wakati adhabu halali ni red card ambayo mhusika anamiss mechi3 bila faini.KAMA clotds wasingepayuka wangetoa adhabu kihakali ,rara hivi wameanyisha kampeni ya kuuondoa uongozi wa yanga madarakani,eti sabb waliwatimua kwenye press conference...NACHUKIA SANA HAWA JAMAA
   
 13. S

  Saas JF-Expert Member

  #13
  Apr 22, 2012
  Joined: Aug 21, 2011
  Messages: 269
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Bala kati ya watu ambao siwezi kusikiliza wakijadili mpira ni hawa watu wa Clouds akina Shafii mpira wao ni wakukopi na kupaste
   
 14. Maundumula

  Maundumula JF-Expert Member

  #14
  Apr 22, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 7,055
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  Mimi naipenda Yanga lakini lazima tukubai kwamba Yanga safari hii inaenda kibabaishaji sana! Wewe timu gani inamchezesha mchezaji mwenye kadi nyekundu wakati wanafahamu fika swala halijaamuliwa? Wachezaji wanampiga refa viongozi hawasemi lolote! Na wala hamna hatua zinazochukuliwa. Yanga haina timu ya vijana inashindwa hata na simba. Aibu kwa kweli
   
 15. Mtu wa Pwani

  Mtu wa Pwani JF-Expert Member

  #15
  Apr 22, 2012
  Joined: Dec 26, 2006
  Messages: 4,095
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  hivi kusema ukweli ndio iwe nongwa jamani ?
   
Loading...