Shabiki Yanga achafukwa, aamua kuchoma tisheti ya Niyonzima

kirerenya

JF-Expert Member
Aug 27, 2013
1,696
2,252
NIYONZIMA.jpg

Baada ya shabiki mmoja wa Yanga kuonekana akiichoma moto jezi ya kiungo Haruna Niyonzima.
Niyonzima raia wa Rwanda, ameamua kuondoka Yanga baada ya mkataba wake kwisha na klabu ya Yanga ikawa haina fedha ya kumsajili tena kutokana na dau lake aliloweka mezani.

Mjadala mkubwa mitandaoni ni namna ambavyo shabiki huyo amechoma jezi hiyo akionyesha hasira kwa kuwa Niyonzima ameamua kuondoka na kuna taarifa kwamba anakwenda Simba.
Mashabiki kadhaa wamekuwa wakimuunga mkono aliyefanya hivyo. Lakini wako wengi ambao wamekuwa wakimpiga, wakiamini si jambo sahihi.

Mjadala huo unaonekana kuwa mkali na kuna sehemu watu wanashindwa kuthibiti jazba zao kwa kuanza kutoa maneno makali.

Mjadala huo ulianza jana jioni mara tu baada ya picha mnato na zile za videoza shabiki akichoma jezi, zilipoanza “kutambaa” mitandaoni.

Chanzo: Salehe Jembe
 
Mashabiki wa yanga hawana akili KBS.mbona washabiki wa simba hawajachoma jezi ya ajibu kijana aliekulia msimbazi .mbona mashabiki was simba kila mwaka yanga inachukua wachezaji wake kibabe lkn simba hawafanyi mnayofanya nyinyi ngumbaru wa yanga..mnapaswa kuelewa mpira ni kazi ni maisha mchezaji mpira ni biashara ni vyema kumbariki mchezaji anapoondoka kuliko kumlaani..au mnataka km ngasa ambae alidhani yanga ndio baba ndio mama matokeo sasa anahaha mpira umekwisha sasa umaskini unamjia..nawapongeza sana mashabiki wa simba kwa hekima na utulivu wenu.
 
Niyonzima alipendwa sana na mashabiki wa Yanga.Alitakiwa ajue hilo.
Niyonzima ni kama alivyokuwa Ngassa kwa mashabiki
 
Hata Ulaya hayo mambo yapo Liverpool walichoma jezi za Torres, Barcelona walichoma za Figo na juzi juzi West Ham walichoma za Payet
 
Mashabiki wa yanga hawana akili KBS.mbona washabiki wa simba hawajachoma jezi ya ajibu kijana aliekulia msimbazi .mbona mashabiki was simba kila mwaka yanga inachukua wachezaji wake kibabe lkn simba hawafanyi mnayofanya nyinyi ngumbaru wa yanga..mnapaswa kuelewa mpira ni kazi ni maisha mchezaji mpira ni biashara ni vyema kumbariki mchezaji anapoondoka kuliko kumlaani..au mnataka km ngasa ambae alidhani yanga ndio baba ndio mama matokeo sasa anahaha mpira umekwisha sasa umaskini unamjia..nawapongeza sana mashabiki wa simba kwa hekima na utulivu wenu.
Mkuu umetukosea sana mashabiki wa Yanga. Nadhani si sahihi kuwa_attack mashabiki wa Yanga kwa kosa la shabiki mmoja. Naamini wapo mashabiki kibao wa Yanga wasiokubaliana na uchomaji wa jezi hiyo.

Sisi kama wanamichezo tusimame pamoja kumlaani shabiki mwenzetu aliyechoma jezi hiyo na siyo kuchukulia kuwa tukio hilo linakubalika kwa mashabiki wote wa Yanga.

Mchezaji anapomaliza mkataba na klabu yoyote anakuwa huru kujiunga na klabu yoyote. Hakuna sababu ya kuwa na mihemuko, wachezaji hawachezi kwa ridhaa, wanahitaji malipo bora.

Mchezo wa soka ni mchezo wa kiungwana ndani na nje ya uwanja.

Msimamo wangu:
Nalaani kitendo cha kuchoma jezi hiyo namba 8, si kitendo cha kiungwana.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom