Shabiki wa Simba afariki dunia baada ya Mgalu kukosa penati dhidi ya Tanzania Prisons

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,000
9,862
Mpenzi wa timu ya Simba Ally Rashidi Kuntika (71)katika mamlaka ya mji mdogo wa Namtumbo mkoani Ruvuma alidondoka ghafla na kufariki dunia papohapo mara baada ya mchezaji wa timu ya Simba Chris Mugalu kukosa kufunga goli la penati dhidi ya timu ya Tanzania Prison.

Afisa mtendaji mkuu wa mamlaka ya mji mdogo wa Namtumbo bwana Geofrey Kalikawe alisema marehemu alikutwa na umauti huo akiwa katika kibanda umiza kwa mzee kikoti akiangalia mpira kati ya timu ya simba na timu ya Tanzania Prison na mara baada ya timu ya simba kupata penati alionekana kuwa na furaha isiyo na kifani.

Kalikawe alidai marehemu alikaa katika benchi akiwa na watazamaji wengine wakati wanasubiri mchezaji wa simba kupiga mpira wa penati dhidi ya timu ya Tanzania Prison palikuwa na mabishano ya hapa na pale wengine wakidai anakosa na yeye akidai hawezi kukosa.

Kitendo cha mchezaji wa Simba kukosa kufunga penati hiyo marehemu aliinama kwa muda mrefu na baada ya watazamaji wengine waliokuwa wakishangilia kukosa kufungwa kwa goli hilo walisogea kwa marehemu ili kumdhihaki lakini walipofika kwake walikosa ushirikiano baada ya kudhania kuwa amezimia na katika harakati za kuokoa maisha yake wakagundua amefariki dunia.

Kwa mujibu wa mtoto wa marehemu Barakati Ally kuntika alisema baba yake amefariki dunia wakati anatazama mpira katika kibanda umiza kwa William Enas Kikoti kwa kuwa mzee wao alikuwa mpenzi wa timu ya Simba kindakindaki na kwa kuthibitisha hilo alidai baba yake aliwahi kutoa mbuzi( beberu)wakati timu ya simba ilipokuwa inapita namtumbo kuelekea songea kucheza na timu ya majimaji kupitia njia ya Lindi na amewahi kuvunja redio baada ya timu ya simba kufungwa na timu ya Yanga siku za nyuma.

Mashabiki wa timu ya Simba katika mamlaka ya mji mdogo wa Namtumbo akiwemo Charles Mkandawile na Moses Bakari walidai wamempoteza mpenzi na shabiki wa kweli wa timu ya simba ambaye alikuwa anashikilia msimamo wake wa kuipenda simba hata wakati ule simba inafanya vibaka katika ligu kuu yeye alionekana kuitetea Simba kwa hali na mali na kumpatia mtoto wake wa kiume jina la kichuya.

Marehemu atazikwa katika makaburi ya Namtumbo kati ambapo ameacha wanawake 3,watoto 17 wakiwa wanawake 9 na watoto wa kiume 8.

1615477527298.png
 
Rip mzee but penalty kik is just like any other free kiki sio kila penalty inazaa goli kama its Constant
 
Simba lazima Waandae wachezaji maalum wa kupiga penati. Sielewa kama wanafanya mazoezi ya kupiga penati.

Nammisi sana Erasto Nyoni kwenye penati.
 
Back
Top Bottom