Shaban mlacha ni nani udom!!??

Baba Tina

Senior Member
Dec 22, 2010
131
2
Prof SHABAN MLACHA (profesa wa kiswahili) anatajwa kua mtu anaye vuruga chuo kikuu cha dodoma (UDOM). Yeye naibu makamu mkuu wa chuo anayesimamia mipango, PESA, na utawala lakin inasemekana ndiye mwenye nguvu zaidi kuliko hata makamu mkuu wa chuo hicho. Anatajwa kua mtu mwenye kiburi, ubabe, dharau na majivuno kiasi cha kusababisha wahadhiri na wafanyakazi wengi kuhama chuoni hapo kila kukicha. Kiburi chake kinahusishwa na uswahiba wa karibu sana alionao na JK ambapo inasemekana wameoa sehemu moja.!! WADAU MNAOMFAHAMU HUYU MTU MNASEMAJE?
 
kawaida ya tanganyika mpaka siku moja wafanyakazi wamwage damu au wavunje ofisi ndo watamtoa mlacha hapo.... jk anakula kuku tu...sidhani hata habari za mlacha anazo...
 
Prof SHABAN MLACHA (profesa wa kiswahili) anatajwa kua mtu anaye vuruga chuo kikuu cha dodoma (UDOM). Yeye naibu makamu mkuu wa chuo anayesimamia mipango, PESA, na utawala lakin inasemekana ndiye mwenye nguvu zaidi kuliko hata makamu mkuu wa chuo hicho. Anatajwa kua mtu mwenye kiburi, ubabe, dharau na majivuno kiasi cha kusababisha wahadhiri na wafanyakazi wengi kuhama chuoni hapo kila kukicha. Kiburi chake kinahusishwa na uswahiba wa karibu sana alionao na JK ambapo inasemekana wameoa sehemu moja.!! WADAU MNAOMFAHAMU HUYU MTU MNASEMAJE?

Je, Umewahi kusoma riwaya ya Kusadikika ya Shaaban Robert? Isome na utamjua huyu mtu ni nani. Katika riwaya hiyo yeye ndiye mhusika aitwae Majivuno, ni waziri wa Mfalme wa Kusadikika ambaye ana nguvu kumlikoMfalme mwenyewe. Shaaban Robert alimjua Mlacha miaka mingi iliyopita. Majivuno alijihesabu mwenyewe kuwa KIDOLE CHAKE CHA MWISHO KINA AKILI KUILIKO MIILI NA VICHWA VYA WASADIKIKA WOTE VIKIWEKWA PAMOJA (uk.7). Huyo Mlacha unayemzungumzia, Kwa maneno yake mwenyewe anaTUambia mimi na wewe, na Watanzania wote, kuwa Tunamshinda kwa vitu viwili tu, 1. ni Urefu kwa kuwa yeye ni mfupi sana na 2. ni umaskini kwa kuwa yeye anazo fedha halali kwa malipo ya shilingi za Kitanzania za Kutosha sana. Huyo ndiye Waziri majivuno wa Kusadikika. Maneno hayo hapo, kwamba tunamzidi kwa Umaskini na Urefu, yanalingana sana na kejeli za Majivuno (uk 4) aliposema " Mikono ya mshitakiwa ni mifupi kwa kutenda wema wowote" Tafakari na chukuwa hatua.....!
 
..........Yote haya atasemwa lakini ukitafuta a Real story, huwezi kuelezea mafanikio ya UDOM bila kumtaja Profesa Mlacha, ana shule ya Sekondari sawa, lakini ungetegemea mtu ambaye ni profesa ashindwe kuwa na shule ya kusaidia wanafunzi wa tanzania au kwa vile tumezoea ma-profesa wetu kusinzia tu pale UDSM na kwingineko..BRAVO MLACHA songa mbele.....
 
Mara nyingi watu wanonekana wabaya katika kutekeleza majukumu yao huwa ni watu wenye mabadiliko chanya "ukimchekea nyani utayavuna mabua"nawasilisha!!
 
Sijasoma udom lakini nimeshasikia sifa ya hako kajamaaa, ni kashenzi mbaya.. Nasikia kanadai anachozidiwa na wanafunzi wa udom na walimu ni umaskini tu.. As yeye ana pesa mbaya
 
..........Yote haya atasemwa lakini ukitafuta a Real story, huwezi kuelezea mafanikio ya UDOM bila kumtaja Profesa Mlacha, ana shule ya Sekondari sawa, lakini ungetegemea mtu ambaye ni profesa ashindwe kuwa na shule ya kusaidia wanafunzi wa tanzania au kwa vile tumezoea ma-profesa wetu kusinzia tu pale UDSM na kwingineko..BRAVO MLACHA songa mbele.....
Unampa sifa tele huyu prof mlacha unamjua kiundani wewe?Nenda kawaulize wafanyakazi na wanafunzi wa
chuo kikuu cha Dodoma watakupa hali halisi,kazi inawezekana anafanya sana,hilo sikatai
Lakini huyu bwana ana mapungufu mengi pia kwenye utendaji kazi wake ikiwa ni pamoja na jeuri,dharau, dhulma especially(FINANCE DEPARTMENT) ambao wako chini yake, na ana roho ngumu sana, ni rahisi jk kukusaidia lakini sio huyu mtu, ukienda na matatizo ya madai yako, mikopo au hata ya kazi anakufukuzia mbali na maneno ya kashfa.Anaamini hamna mtu mwenye uwezo wa kumtoa kwenye hicho cheo alichonacho.
WITO: Ajirekebishe asifikiri hii Dunia ina watu wake!!
 
..........Yote haya atasemwa lakini ukitafuta a Real story, huwezi kuelezea mafanikio ya UDOM bila kumtaja Profesa Mlacha, ana shule ya Sekondari sawa, lakini ungetegemea mtu ambaye ni profesa ashindwe kuwa na shule ya kusaidia wanafunzi wa tanzania au kwa vile tumezoea ma-profesa wetu kusinzia tu pale UDSM na kwingineko..BRAVO MLACHA songa mbele.....

Mamluki weweeee, acha kuongea habari zako, kila mtu anamlalamikia yeye huoni kama ni tatizo hilo, mimi mwenyewe nilikuwa pale nikaondoka kwa ajili ya mambo yake,sema tu kwa sabau nchi tuna shida ya ajira ndo mana watu wanaomba pale lakini hapafai,
 
Ni kweli Professor Mlacha tunamzidi urefu na umasikini. Huo ndo ukweli japo unauma kwani yeye ni ki-mtu kifupi chenye pesa mingi kuliko wengi wetu. Isitoshe kwenye nyanja ya elimu tayari chenyewe ni ki-Professor na hakuna level ya juu ya elimu zaidi ya u-prof.
 
Sijasoma udom lakini nimeshasikia sifa ya hako kajamaaa, ni kashenzi mbaya.. Nasikia kanadai anachozidiwa na wanafunzi wa udom na walimu ni umaskini tu.. As yeye ana pesa mbaya

Anasema wanachomzidi ni Urefu na Umaskin.(ni kafupi kinoma)
 
Back
Top Bottom