Shabaab restaurant assault leaves 19 dead in Mogadishu

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,622
8,397
Shambulizi la bomu la kujitoa mhanga na la bunduki katik hoteli moja na mgahawa kwenye mji mkuu wa Somalia, Mogadishu, limewaua takriban watu 19.

Shambulizi hilo lilianza siku ya Jumatano jioni wakati waislamu walikuwa wakifungua siku yao ya kufunga ya mwezi mtukufu wa Ramadan

Wanamgambo kutoka kundi la Al-Shabab waliwashikilia zaidi ya mateka 20 wakati waaufyatuaji wa risasi ambao kwa sasa umekwisha.

Kundi hilo lenye uhusiano na kundi al-Qaeda lilikiri kutekeleza shambulizi hilo lililofanyika mapema Alhamisi.

Shambulizi hilo lilianza mwendo wa saa mbili usiku wakati gari lililokuwa limejazwa milipuko lilishambulia hoteli hiyo ya kifahari karibu na mgahawa, ambalo ndilo eneo pekee mjini Mogadishu lililo na discco.

Kisha watu wenye bunduki wakaingia mgahawa uliokuwa karibu na kuwashika watu mateka.

Wenyeji wanasena walisikia sauti za risasi usiku kucha lakini hali kwa sasa imetulia.

Pia kuna ripoti ambazo hazijathibitishwa kuwa washambuliaji walikuwa wamevalia sare za polisi.

Vikosi kutoka kwa Muungano wa Afika viliwatimua wanamgambo wa al-Shabab kutoka mjini Mogadishu mwaka 2011, lakini eneo kubwa la nchi bado liko mikononi mwa wanamgambo hao.

=====
At least 19 people were killed when Islamist attackers launched a car bomb and gun attack on a busy hotel and adjacent restaurant in the Somali capital, a police officer said on Thursday.

A car driven by a suicide bomber rammed into the Posh Hotel in south Mogadishu on Wednesday evening before gunmen rushed into a Pizza House, an adjacent restaurant, and took 20 people hostage. Posh Hotel is the only venue with a discotheque in the capital. Abdi Bashir told Reuters that the Somali security forces took control of the restaurant at midnight after the gunmen held hostages inside for several hours. Five of the gunmen were killed, Bashir said.

Extremist snipers fired on security troops who surrounded the restaurant building and used big guns mounted on the backs of vehicles to neutralize militants. Soldiers entered the ground floor while the insurgent attackers held positions upstairs.

“We are in control of the hotel but it was mostly destroyed by the suicide bomber,” Bashir told Reuters by phone. Witnesses said there were bodies lying at the scene on Thursday morning as ambulances came to take them away.

Al Shabaab, the Islamist militant group, claimed responsibility for the attack.
 
Back
Top Bottom