Miss Zomboko
JF-Expert Member
- May 18, 2014
- 4,495
- 9,275
Singida. Aliyekuwa Ofisa Masoko wa Benki ya Posta Tanzania Tawi la Singida na mkazi wa Kibaoni mjini hapa, Elihuruma Emmanuel (46), amehukumiwa kifungo cha miaka sita kwa wizi wa Sh 1.7 milioni.
Emmanuel, amehukumiwa jana (Alhamisi) na Mahakama ya Hakimu Mkazi Singida.
Imeelezwa kuwa mshitakiwa, Elihuruma kabla kuwa Ofisa Masoko, alikuwa mchungaji wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri (KKKT) Dayosisi ya Singida, Jimbo la Kati.
Awali Mwendesha Mashitaka na Mwanasheria wa Serikali, Neema Mwaipyana, amedai mbele ya Hakimu Mfawidhi Mwandamizi wa mahakama hiyo, Joyce Minde, kuwa kati ya Agosti na Septemba 2016, mshitakiwa alikusanya Sh 1.7 milioni zikiwa ni akiba kwa ajili ya mikopo ya wanavikundi vya kukopa na kuweka.
Fedha hizo zilitolewa na wanavikundi wapatao 15.
Mwaipyana amesema katika kipindi hicho, mshitakiwa alipewa ajira ya mkataba wa mwaka mmoja na Benki ya Posta Tanzania Tawi la Singida.
Amesema jukumu la mshitakiwa lilikuwa ni kuelimisha wananchi juu ya huduma/shughuli mbalimbali zinazotolewa na benki hiyo ikiwemo huduma za mikopo.
“Mshitakiwa Elihuruma, Agosti mwaka jana akiwa amevaa sare ya Benki ya Posta Tanzania, yenye nembo, alifika katika vijiji vya Kitukuntu na Ulemo wilaya ya Iramba. Lengo ni kutoa elimu juu ya shughuli mbalimbali za benki hiyo kwa wananchi wa vijiji hivyo.
Jumla ya watu 15 waliweza kuunda kikundi cha Maendeleo Tumaini, ili waweze kukopa kwenye benki hiyo,” amesema Mwaipyana.
Mwaipyana amesema wanakikundi hao walitoa Sh 15,000 za kufungulia akaunti na Sh3000 kwa ajili ya kitambulisho kila mmoja.
Pia kila mmoja alimpa mshitakiwa kati ya Sh150, 000 na 300,000 ikiwa ni amana ya mikopo waliyoomba.
Kadhalika, mwendesha mashitaka huyo amesema Septemba mwaka jana, mshitakiwa alifika Kijiji cha Matare, wilayani Ikungi na kufanikiwa kuunda kikundi cha Nguvu Kazi.
“Katika kikundi hicho,wanachama wawili walitoa kila mmoja Sh18,000 zikiwa ni za kufungulia akaunti na za vitambulisho. Pia walitoa zaidi ya Sh300,000 ikiwa ni amana kwa ajili ya mkopo,”amesema.
Mwendesha mashitaka huyo, amesema mshitakiwa Elihuruma, alifungua akaunti za wanavikundi vyote viwili.
Lakini hakuingiza kwenye akaunti za wahusika, fedha zote za akiba kiasi cha Sh1.7 milioni badala yake alizitumia kwa matumizi yake binafsi.
Kabla ya kutolewa hukumu hiyo, mwendesha mashitaka aliiomba mahakama hiyo impe mshitakiwa adhabu kali, ili iwe fundisho kwake na kwa wengine.
Kwa upande wake mshitakiwa, aliiomba mahakama hiyo impe adhabu nafuu kwa madai ana familia inayomtegemea.
Akitoa hukumu hiyo, Hakimu Minde amesema upande wa mashitaka umethibitisha pasina kuacha shaka yoyote kuwa Elihuruma ana hatia kama alivyoshitakiwa.
chanzo; mwananchi