Sh 1.7 milioni zamtupa jela miaka sita Ofisa wa Benki

miss zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
2,773
2,000
Singida. Aliyekuwa Ofisa Masoko wa Benki ya Posta Tanzania Tawi la Singida na mkazi wa Kibaoni mjini hapa, Elihuruma Emmanuel (46), amehukumiwa kifungo cha miaka sita kwa wizi wa Sh 1.7 milioni.

Emmanuel, amehukumiwa jana (Alhamisi) na Mahakama ya Hakimu Mkazi Singida.

Imeelezwa kuwa mshitakiwa, Elihuruma kabla kuwa Ofisa Masoko, alikuwa mchungaji wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri (KKKT) Dayosisi ya Singida, Jimbo la Kati.

Awali Mwendesha Mashitaka na Mwanasheria wa Serikali, Neema Mwaipyana, amedai mbele ya Hakimu Mfawidhi Mwandamizi wa mahakama hiyo, Joyce Minde, kuwa kati ya Agosti na Septemba 2016, mshitakiwa alikusanya Sh 1.7 milioni zikiwa ni akiba kwa ajili ya mikopo ya wanavikundi vya kukopa na kuweka.

Fedha hizo zilitolewa na wanavikundi wapatao 15.
Mwaipyana amesema katika kipindi hicho, mshitakiwa alipewa ajira ya mkataba wa mwaka mmoja na Benki ya Posta Tanzania Tawi la Singida.

Amesema jukumu la mshitakiwa lilikuwa ni kuelimisha wananchi juu ya huduma/shughuli mbalimbali zinazotolewa na benki hiyo ikiwemo huduma za mikopo.

“Mshitakiwa Elihuruma, Agosti mwaka jana akiwa amevaa sare ya Benki ya Posta Tanzania, yenye nembo, alifika katika vijiji vya Kitukuntu na Ulemo wilaya ya Iramba. Lengo ni kutoa elimu juu ya shughuli mbalimbali za benki hiyo kwa wananchi wa vijiji hivyo.

Jumla ya watu 15 waliweza kuunda kikundi cha Maendeleo Tumaini, ili waweze kukopa kwenye benki hiyo,” amesema Mwaipyana.

Mwaipyana amesema wanakikundi hao walitoa Sh 15,000 za kufungulia akaunti na Sh3000 kwa ajili ya kitambulisho kila mmoja.

Pia kila mmoja alimpa mshitakiwa kati ya Sh150, 000 na 300,000 ikiwa ni amana ya mikopo waliyoomba.

Kadhalika, mwendesha mashitaka huyo amesema Septemba mwaka jana, mshitakiwa alifika Kijiji cha Matare, wilayani Ikungi na kufanikiwa kuunda kikundi cha Nguvu Kazi.

“Katika kikundi hicho,wanachama wawili walitoa kila mmoja Sh18,000 zikiwa ni za kufungulia akaunti na za vitambulisho. Pia walitoa zaidi ya Sh300,000 ikiwa ni amana kwa ajili ya mkopo,”amesema.

Mwendesha mashitaka huyo, amesema mshitakiwa Elihuruma, alifungua akaunti za wanavikundi vyote viwili.

Lakini hakuingiza kwenye akaunti za wahusika, fedha zote za akiba kiasi cha Sh1.7 milioni badala yake alizitumia kwa matumizi yake binafsi.

Kabla ya kutolewa hukumu hiyo, mwendesha mashitaka aliiomba mahakama hiyo impe mshitakiwa adhabu kali, ili iwe fundisho kwake na kwa wengine.

Kwa upande wake mshitakiwa, aliiomba mahakama hiyo impe adhabu nafuu kwa madai ana familia inayomtegemea.

Akitoa hukumu hiyo, Hakimu Minde amesema upande wa mashitaka umethibitisha pasina kuacha shaka yoyote kuwa Elihuruma ana hatia kama alivyoshitakiwa.
chanzo; mwananchi
 
cocochanel

JF-Expert Member
Oct 6, 2007
24,520
2,000
Ila haya mambo ya sheria ya nchi yetu bado yanashangaza sana. Hata kama walikataa kosa lao.

Watafanya watu waanze kuiba pesa kubwa za mabilioni na juu zaidi, wakikamatwa wakakubali kosa mahakamani... kesi hiyoooo kwisha halafu wanatoka kwa kidunchu cha fedha.
 
the glassroof

JF-Expert Member
Apr 25, 2017
247
500
Kipi bora kati ya kulipa deni ama kutumikia kifungo. Me nafikiri wangekata tu sehem ya mshahara maisha yaendelee.
 
kijani11

JF-Expert Member
Jan 19, 2014
6,270
2,000
Wezi wa Trilioni 108 wanaitwa Ikulu kujadiliana lkn mwizi wa 1.7Milioni anafungwa miaka 6...

Hapo ndipo utajua kwanini Mess ni bingwa wa kufunga lkn kashindqa kufunga ramadhani
Dunia haijawahi na haitakaa iwe na usawa.
 
Yodoki II

JF-Expert Member
Oct 17, 2014
4,944
2,000
Hizo ishu zingine ni kwa sababu watu wanakosa ushauri wa kitaalam.Upo uwezekano huyu bwana hangefungwa kabisa Km angelimpata wakili makini
 
Raimundo

JF-Expert Member
May 23, 2009
13,500
2,000
Ila haya mambo ya sheria ya nchi yetu bado yanashangaza sana. Hata kama walikataa kosa lao.

Watafanya watu waanze kuiba pesa kubwa za mabilioni na juu zaidi, wakikamatwa wakakubali kosa mahakamani... kesi hiyoooo kwisha halafu wanatoka kwa kidunchu cha fedha.
Leo sikusomi somi.
 
Chupaku

JF-Expert Member
Oct 15, 2008
1,092
1,500
Ila haya mambo ya sheria ya nchi yetu bado yanashangaza sana. Hata kama walikataa kosa lao.

Watafanya watu waanze kuiba pesa kubwa za mabilioni na juu zaidi, wakikamatwa wakakubali kosa mahakamani... kesi hiyoooo kwisha halafu wanatoka kwa kidunchu cha fedha.
Mahakimu wengine bwana. Kwani hiyo miaka sita atakula milioni ngapi huko jela? Too much
 
areafiftyone

JF-Expert Member
Jan 4, 2017
7,403
2,000
Singida. Aliyekuwa Ofisa Masoko wa Benki ya Posta Tanzania Tawi la Singida na mkazi wa Kibaoni mjini hapa, Elihuruma Emmanuel (46), amehukumiwa kifungo cha miaka sita kwa wizi wa Sh 1.7 milioni.

Emmanuel, amehukumiwa jana (Alhamisi) na Mahakama ya Hakimu Mkazi Singida.

Imeelezwa kuwa mshitakiwa, Elihuruma kabla kuwa Ofisa Masoko, alikuwa mchungaji wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri (KKKT) Dayosisi ya Singida, Jimbo la Kati.

Awali Mwendesha Mashitaka na Mwanasheria wa Serikali, Neema Mwaipyana, amedai mbele ya Hakimu Mfawidhi Mwandamizi wa mahakama hiyo, Joyce Minde, kuwa kati ya Agosti na Septemba 2016, mshitakiwa alikusanya Sh 1.7 milioni zikiwa ni akiba kwa ajili ya mikopo ya wanavikundi vya kukopa na kuweka.

Fedha hizo zilitolewa na wanavikundi wapatao 15.
Mwaipyana amesema katika kipindi hicho, mshitakiwa alipewa ajira ya mkataba wa mwaka mmoja na Benki ya Posta Tanzania Tawi la Singida.

Amesema jukumu la mshitakiwa lilikuwa ni kuelimisha wananchi juu ya huduma/shughuli mbalimbali zinazotolewa na benki hiyo ikiwemo huduma za mikopo.

“Mshitakiwa Elihuruma, Agosti mwaka jana akiwa amevaa sare ya Benki ya Posta Tanzania, yenye nembo, alifika katika vijiji vya Kitukuntu na Ulemo wilaya ya Iramba. Lengo ni kutoa elimu juu ya shughuli mbalimbali za benki hiyo kwa wananchi wa vijiji hivyo.

Jumla ya watu 15 waliweza kuunda kikundi cha Maendeleo Tumaini, ili waweze kukopa kwenye benki hiyo,” amesema Mwaipyana.

Mwaipyana amesema wanakikundi hao walitoa Sh 15,000 za kufungulia akaunti na Sh3000 kwa ajili ya kitambulisho kila mmoja.

Pia kila mmoja alimpa mshitakiwa kati ya Sh150, 000 na 300,000 ikiwa ni amana ya mikopo waliyoomba.

Kadhalika, mwendesha mashitaka huyo amesema Septemba mwaka jana, mshitakiwa alifika Kijiji cha Matare, wilayani Ikungi na kufanikiwa kuunda kikundi cha Nguvu Kazi.

“Katika kikundi hicho,wanachama wawili walitoa kila mmoja Sh18,000 zikiwa ni za kufungulia akaunti na za vitambulisho. Pia walitoa zaidi ya Sh300,000 ikiwa ni amana kwa ajili ya mkopo,”amesema.

Mwendesha mashitaka huyo, amesema mshitakiwa Elihuruma, alifungua akaunti za wanavikundi vyote viwili.

Lakini hakuingiza kwenye akaunti za wahusika, fedha zote za akiba kiasi cha Sh1.7 milioni badala yake alizitumia kwa matumizi yake binafsi.

Kabla ya kutolewa hukumu hiyo, mwendesha mashitaka aliiomba mahakama hiyo impe mshitakiwa adhabu kali, ili iwe fundisho kwake na kwa wengine.

Kwa upande wake mshitakiwa, aliiomba mahakama hiyo impe adhabu nafuu kwa madai ana familia inayomtegemea.

Akitoa hukumu hiyo, Hakimu Minde amesema upande wa mashitaka umethibitisha pasina kuacha shaka yoyote kuwa Elihuruma ana hatia kama alivyoshitakiwa.
chanzo; mwananchi
Mimi huwa najua Wachungaji walio wengi elimu zao ni ndogo kwa hiyo generally ufahamu wao ni mdogo sana. Also wanakuwa mara nyingi wana maisha ya kupungukiwa sana,kwa hiyo wakipata mwanya
wako eager to close the gap quickly.Sasa ilikuwaje in that background Mchungaji huyu wa KKKT kuwa Afisa Masoko wa Bank ya Posta? What is behind the curtain.Inashangaza,tena sio kidogo.Niseme tu kwamba the Bank has itself to blame.Utamtupiaje Fisi mzoga?
 
Zesh

JF-Expert Member
Apr 27, 2017
14,636
2,000
Dah pendeshee ndama pamoja na makosa yote alihukumiwa miaka mitano tu ila huyu kisenti cha 1.7 kinamfungisha miaka saba......kweli dunia kizunguzungu
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom