SGT PHILIPO Imepotelea wapi?

Freewine

JF-Expert Member
Jan 7, 2018
257
212
Kulikuwa na riwaya ya kijasusi hapa inaitwa SGT Philipo sijui imepoteaje hapa jukwaani.

Mrejesho pleaseeee
 
hahaha Jf never bored ....usikute wale tango 4 na tango 5 wameamua kupita nayo mazima riwaya yetu pendwa.
 
KIMYA KINGI KINAMSHINDO MKUU.

kichwa cha habari hapo juu namna kilivyokaa unaweza kusema kuwa ni riwaya mpya imeanza, la hasha! Hii siyo riwaya bali ni story tu ya kawaida.

Wapenzi wasomaji wa riwaya zangu pendwa, nimekuwa mtunzi mzuri kwenu kuanzia mwaka 2013, nimekuwa nikiwaburudisha na kuwaelimisha kupitia riwaya nyingi kama vile ENZI ZA UASKARI WANGU, TRUE STORY, SIKU ZANGU ZINAHESABIKA, WAPELELEZI, SECRET MISSION NA SGT PHILIPO. Nimekuwa nikifarijika sana kuona story zangu zinafikisha ujumbe mzuri kwa hadhira yangu(Askari Polisi) kwakuwa ninyi ndiyo nimewalenga hasa kuwapa elimu na burudani hii. Lakini pia nimefarijika kuona kumbe hata wateja wa nje nao wametokea kuzipenda hizi riwaya zinazotuhusu sisi, nimegundua kuwa kumbe wanapenda sana kuona namna Askari Polisi wanavyofanya upelelezi, namna askari polisi wanavyopambana kwenye mapigano na namna Askari Polisi wanavyoishi kwa ujumla.
Kitendo hiki kimefanya kwa namna moja au nyingine wateja wa nje kufahamu mbinu nzuri wanazotumia askari polisi kufanya upelelezi na namna wanavyopambana kukomesha matukio mbalimbali yenye lengo la kuondoa amani hapa nchini. Hii itasaidia sana wateja wa nje kulipenda jeshi letu pendwa. Mbinu hii imetumiwa sana na mataifa makubwa kama vile USA ambapo wametumia Movies na Series kutangaza na kuonesha uimara wa vyombo vyao vya ulinzi na usalama. Binafsi ningependa na sisi tufike huko.

Siku chache zilizopita nilikuwa kimya sana, sikuweza kutoa muendelezo wa riwaya ya Sgt Philipo, siyo kwamba niliishiwa madini, au niliamua tu kufanya kwa makusudi, hapana! Hiyo yote inasadifu kichwa cha habari "Kimya kingi kina mshindo mkuu" nilikuwa napita kwenye ukurasa huu nakuta wapenzi wangu wasomaji mlivyokuwa mkijaribu kuniita kwa kuweka mapachiko mbalimbali nikawa natamani kuwajibu lakini nikasema leo ndiyo nitaongea nanyi.
Lengo kubwa la kimya kile nilikuwa busy sana asubuhi, mchana, jioni na usiku kuandika na kuandaa softcopy ya mfano wa kitabu cha Sgt philipo pamoja na Secret Mission. Nimefanikiwa kuiandika Sgt Philipo na kuimaliza kabisa, sasa ipo tayari kwa matumizi, wapenzi wasomaji hamtakuwa na shahuku ya kutaka kufahamu nini kinaendelea. Nimeiandaa vizuri sana kwenye mfumo wa PDF, hivyo basi kama mtu umetokea kuipenda stroy hii utakuwa unaisoma kwa kuirudia kila upendavyo wewe.

Sasa basi nini ninaomba kutoka kwenu?
Kitu pekee ninachowaomba wapenzi wafuatiliaji wa story zangu, mmekuwa nami miaka yote hii, ninaomba kuwaletea softcopy hizi kwa ninyi kunichangia kidogo ili nifarijike kidogo na nione kuwa kumbe mpo pamoja nami. Mchango wenu utanipa nafasi ya kupiga hatua mbele, kwa story hizi na nyingine zinazokuja niweze kutoa hardcopy kwakuwa ni gharama kiasi.
Niliona kuwa itakuwa vizuri kama mtanichangia kwa sh 3,000/= tu kwa kila Riwaya (Sgt Philipo na Secret mission) mnaonifuatilia kwenye story zangu mtakuwa mnanielewa. Naomba mnitie moyo kidogo wapendwa. Lakini pia kama mtakuwa na mawazo tofauti nawasikiliza ninyi, kama mtapenda niwaletee hivyo hivyo bila malipo napo haina shida nitaileta pia.

Sasa basi kama tutakubaliana, nimependekeza kuwa nitatengeneza group la whatsapp kwa muda, wale ambao watakuwa tayari kunichangia hicho kidogo nitawaweka humo kwenye group halafu Softcopy ya Sgt Philipo nitaituma humo kwenye group kila mtu anakuwa nayo au hata ukipenda nikutumie binafsi haina shida. Nimependekeza zoezi hili lichukue siku mbili tu yaani leo na kesho ili watu waipate story kwa wakati. Namba yangu ya whatsapp ni 0767 82 97 83. Malipo unaweza kuyafanya kupitia namba 0767 82 97 83 na 0712 37 33 65 majina ni Sweetbert Ndalahwa Masaga, hakikisha majina kabla haujatuma pesa.
Nawatakia kazi njema na Mungu awabariki sana.

Mtunzi: Sweetbert Ndalahwa
 
Kwan apa jf ww umechangia sh ngap ww? Mnazingua sana nyie mnaleta story zenu zikifka nusu mnasitisha mnafanya biashara,
 
Naona una nyegezi za kutukanwa wewe😁[QU
OTE="Kurunzi, post: 29228396, member: 17757"]watu mnapenda vya dezo mpaka povu linawatoka[/QUOTE]
 
Mimi ninayo yote. Kwa kweli mwandishi amejitahidi sana, katika haduthi hii ameinyesha kubadilika na kuimarika kadili episodes zilivyokua zinakwenda.
nimependa zaidi eneo la mahakamani.
 
Back
Top Bottom