joto la jiwe
JF-Expert Member
- Sep 4, 2017
- 26,117
- 46,613
Kenya’s big SGR dream begins to fizzle out as losses mount
Kenya’s big SGR dream begins to fizzle out as losses mount
www-thecitizen-co-tz.cdn.ampproject.org
Kuna msemo maarufu usemao kwamba," Namba hazidanganyi". Hesabu za mapato na matumizi yanaonyesha kwamba, SGR ya Kenya haina uwezo wa kuzalisha hata gharama za uendeshaji kwa mwaka ambayo kwa sasa ni Kshs 12B. Hii ni kutokana na ukweli kwamba imetengeneza 5.8B ndani ya kipindi cha zaidi mwaka mmoja kiasi ambacho ni chini ya 50% ya gharama za uendeshaji. Jambo la kuogopesha zaidi ni kwamba trains zaidi ya 12 kwa siku zimekua zikifanya kazi.
David Ndii, alishawahi kuekeza Mara nyingi sana kuhusu " viability & profitability " ya huu mradi na alishauri kwamba badala ya kujenga reli mpya, ni bora kukopa pesa kidogo ili kufufua reli ya zamani. Maneno yake yametimia:
1) SGR imesababisha Kenya kuwa na deni kubwa linalolipwa na kodi ya wananchi
2) SGR haiwezi kujiendesha, jambo linalolazimisha serikali kutoa pesa za wananchi ili kugharamia gharama za uendeshaji, mwaka Jana pekee serikali ilitoa 6.2B kufikia hasara.
3) Sasa hivi ndio serikali imeona umuhimu wa kufufua reli ya zamani ili kuunganisha na SGR, jambo ambalo litaongeza sana gharama za uendeshaji na usafirishaji kutokana na gharama za kushusha na kupandisha pale Naivasha.