===
SGR ikikamilika inaweza kubeba mizigo yote ya Bandari ya Dar es Salaam kwa siku 250 Tu,
Kama SGR itakamilika bila ya Bandari ya Bagamoyo kujengwa basi Malori yote ya mizigo mnayoyaona hapa nchini yatalazimika kupaki
Iko hivi,treni moja ya mizigo ya SGR inauwezo wa kubeba Jumla ya Tani elfu 10 karibu sawa na Malori 500 kwa Safari moja,
TRC ikiwa na Treni mbili tu za mizigo zinazopishana kwa kila siku basi tutasafirisha Jumla ya Tani elfu 20 kwa siku moja sawa na Malori 1,000.
Nimejaribu kutafuta wastani wa mizigo iliyopakuliwa pale bandari ya Dar es salaam kati ya mwaka 2016|2020 nimepata ni wastani wa Jumla ya Tani milioni tano ( 5M )
Kwamsiofahamu, 98% ya mizigo yote inayoingia na kutoka Tanzania na nchi jirani inapitia bandari ya Dar es Salaam,
Tujiulize, Kama tani elfu 20 kwa SGR zinaweza kubebwa kwa siku moja kwa kutumia treni mbili za SGR zinazopishana,
Je hizi tani 5M zinazopakuliwa pale bandari ya Dar es salaam kwa mwaka mzima zitabebwa kwa muda gan kwa kutumia hii SGR?
Fanya hivi,gawanya tani 5M kwa tani elfu 20 utapata Jumla ya siku 250 za kuisafirisha mizigo yote ya mwaka ya bandari ya Dar es salaam kwa kutumia SGR,
Mkumbuke kuwa, Safari ya Treni ya Mzigo toka Dar -Mwanza ni wastani wa masaa tisa ( 9 ) wakati Safari ya Lori ni zaidi ya masaa 48,
Lakini pia,bei ya kusafirisha mizigo kwa SGR ni ndogo kuliko ile ya Lori na Usalama wa mzigo kwenye SGR ni mkubwa kuliko ule wa kwenye Lori,
Sikia,Nimfanyabiashara mjinga tu ndio anaweza kuacha kupakia SGR yenye nafasi akapakia mzigo kwenye Lori
Sababu pekee inayoweza kuyanusuru haya Malori yetu ni kuwa na bandari nyingine kubwa itakayokuwa na uwezo mkubwa wa kushusha mizigo mingi zaidi ya ile ya Dar es salaam ili SGR ibebe na isaze na Malori ya bebe pia,
Kama hili halitafanyika kuna watu wengi mnakwenda kukosa ajira zenu hapo baadae kidogo,
Nadhani hii ni moja ya sababu ya kwanini Rais Samia anataka bandari hii ijengwe tena kwa haraka kabla ya kumalizika kwa SGR,
NB, Mnaolalamika kuhusu Ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo rudieni tena kusoma andiko hili kwa makini
Bandari ya Tanga! ambayo inakuzwa na pesa zipo!