SGR Dar Morogoro kuanza kutumika mwaka huu

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
3,893
2,000
Msemaji Mkuu wa Serikali, Dk Hassan Abbas amesema ujenzi wa reli ya kisasa ya umeme (SGR) kipande cha kutoka Dar es Salaam hadi Morogoro, kinatarajiwa kukamilika na kuanza kutumika mwaka huu, baada ya Serikali kutoa Sh274 bilioni.

Dk Abbas ameyasema hayo leo Januari 31, 2021 wakati akizungumza na vyombo vya habari jijini Dodoma, kuelezea mambo mbalimbali yanayotekelezwa na Serikali ya awamu ya tano.

Amesema azma ya Serikali ni kuhakikisha ujenzi huo unakamilika kwa wakati na kwamba mradi haujasimama katika kipindi cha Julai mpaka Desemba kipindi cha nusu ya kwanza ya mwaka wa bajeti Serikali imetoa Sh274 bilioni kuendelea na ujenzi.

“Rafiki zangu wa Morogoro na Dar es Salaam wataanza majaribio mwaka huu, nikija hapa nitatoa ratiba lini tutatest kwa mara ya kwanza na tena nitasema lini tutapokea vichwa vya kisasa vya treni ambavyo tulishatangaziana nyuma, wengine walisema havitakuja waendelee kuwa matomaso.

“Reli hii ya kisasa itafufua, itaimarisha, kuchagiza uchumi wetu na maisha ya Mtanzania mmojammoja ni treni ya kisasa na ya kasi kuliko zote ukanda wa Afrika, kuna mataifa mengine wamejitahidi kilomita 120 kwa saa sisi itakwenda kilomita 160 kwa saa ni moja ya treni za kasi sana za umeme katika ukanda wa Afrika Mashariki na Afrika kwa ujumla,” amesema.

Dk Abbas ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo amesema Serikali inaendelea kutoa fedha kila inapohitajika.

“Hatujawahi kukwama wala kukwamishwa kwa namna yoyote, kazi inaendelea ikikamilika itafanya safari ya Dar kwenda Morogoro kwa dakika 90 na ile kwenda Makutupora mpaka Dodoma makao makuu itakuwa na mwendo wa saa 3 zenye utulivu unacheza na internet, WiFi,” amesema.

1612105310614.png
 
Karne

JF-Expert Member
Jun 13, 2016
5,044
2,000
Dar-Moro dakika 90 kama itachomoka na ku-maintain hiyo uniform speed bila kusimama kwenye station yoyote ya njiani kitu ambacho ni next to impossible.
 
elvischirwa

JF-Expert Member
Jan 26, 2013
10,077
2,000
Msemaji Mkuu wa Serikali, Dk Hassan Abbas amesema ujenzi wa reli ya kisasa ya umeme (SGR) kipande cha kutoka Dar es Salaam hadi Morogoro, kinatarajiwa kukamilika na kuanza kutumika mwaka huu, baada ya Serikali kutoa Sh274 bilioni.

Dk Abbas ameyasema hayo leo Januari 31, 2021 wakati akizungumza na vyombo vya habari jijini Dodoma, kuelezea mambo mbalimbali yanayotekelezwa na Serikali ya awamu ya tano.

Amesema azma ya Serikali ni kuhakikisha ujenzi huo unakamilika kwa wakati na kwamba mradi haujasimama katika kipindi cha Julai mpaka Desemba kipindi cha nusu ya kwanza ya mwaka wa bajeti Serikali imetoa Sh274 bilioni kuendelea na ujenzi.

“Rafiki zangu wa Morogoro na Dar es Salaam wataanza majaribio mwaka huu, nikija hapa nitatoa ratiba lini tutatest kwa mara ya kwanza na tena nitasema lini tutapokea vichwa vya kisasa vya treni ambavyo tulishatangaziana nyuma, wengine walisema havitakuja waendelee kuwa matomaso.

“Reli hii ya kisasa itafufua, itaimarisha, kuchagiza uchumi wetu na maisha ya Mtanzania mmojammoja ni treni ya kisasa na ya kasi kuliko zote ukanda wa Afrika, kuna mataifa mengine wamejitahidi kilomita 120 kwa saa sisi itakwenda kilomita 160 kwa saa ni moja ya treni za kasi sana za umeme katika ukanda wa Afrika Mashariki na Afrika kwa ujumla,” amesema.

Dk Abbas ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo amesema Serikali inaendelea kutoa fedha kila inapohitajika.

“Hatujawahi kukwama wala kukwamishwa kwa namna yoyote, kazi inaendelea ikikamilika itafanya safari ya Dar kwenda Morogoro kwa dakika 90 na ile kwenda Makutupora mpaka Dodoma makao makuu itakuwa na mwendo wa saa 3 zenye utulivu unacheza na internet, WiFi,” amesema.

View attachment 1691019
Mbona iliishaanza! TBC wamekuwa wakiivurumisha kwenye vipindi vyao vya kusifu. Naona madereva waliamua kuziendesha bila ruhusa.
 
Wyatt Mathewson

JF-Expert Member
Dec 22, 2017
12,035
2,000
Msemaji Mkuu wa Serikali, Dk Hassan Abbas amesema ujenzi wa reli ya kisasa ya umeme (SGR) kipande cha kutoka Dar es Salaam hadi Morogoro, kinatarajiwa kukamilika na kuanza kutumika mwaka huu, baada ya Serikali kutoa Sh274 bilioni.

Dk Abbas ameyasema hayo leo Januari 31, 2021 wakati akizungumza na vyombo vya habari jijini Dodoma, kuelezea mambo mbalimbali yanayotekelezwa na Serikali ya awamu ya tano.

Amesema azma ya Serikali ni kuhakikisha ujenzi huo unakamilika kwa wakati na kwamba mradi haujasimama katika kipindi cha Julai mpaka Desemba kipindi cha nusu ya kwanza ya mwaka wa bajeti Serikali imetoa Sh274 bilioni kuendelea na ujenzi.

“Rafiki zangu wa Morogoro na Dar es Salaam wataanza majaribio mwaka huu, nikija hapa nitatoa ratiba lini tutatest kwa mara ya kwanza na tena nitasema lini tutapokea vichwa vya kisasa vya treni ambavyo tulishatangaziana nyuma, wengine walisema havitakuja waendelee kuwa matomaso.

“Reli hii ya kisasa itafufua, itaimarisha, kuchagiza uchumi wetu na maisha ya Mtanzania mmojammoja ni treni ya kisasa na ya kasi kuliko zote ukanda wa Afrika, kuna mataifa mengine wamejitahidi kilomita 120 kwa saa sisi itakwenda kilomita 160 kwa saa ni moja ya treni za kasi sana za umeme katika ukanda wa Afrika Mashariki na Afrika kwa ujumla,” amesema.

Dk Abbas ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo amesema Serikali inaendelea kutoa fedha kila inapohitajika.

“Hatujawahi kukwama wala kukwamishwa kwa namna yoyote, kazi inaendelea ikikamilika itafanya safari ya Dar kwenda Morogoro kwa dakika 90 na ile kwenda Makutupora mpaka Dodoma makao makuu itakuwa na mwendo wa saa 3 zenye utulivu unacheza na internet, WiFi,” amesema.

View attachment 1691019
Blah blah blah

Takataka hizi nikae niamini zinachoongea....I have shit to do!
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom