Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,732
- 40,839
Nimesikia tangu sakata la rada lianze kuwa SFO wanafanya uchunguzi kuhusu BAE na malipo ya karibu Bilioni 21 kwa dalali Vithlani. Kila tukiwauliza watawala wetu wanatuambia "uchunguzi unaendelea" na wengine wanasema "tuache uchunguzi ufanyike".
Naomba mwenye kujua, je Tanzania inamkata na SFO kuchunguza makosa ya uhalifu yaliyofanyika Tanzania au kufanywa na Watanzania Tanzania? Hawa SFO wanavyochunguza wanachunguza kwa niaba ya serikali ya Tanzania au ya Uingereza?
Iweje SFO wachunguze viongozi wetu na taasisi zetu ili kuridhisha wananchi wa nchi zao na serikali yao. Je tusubiri FBI na State Dept kuanzisha uchunguzi kuhusu Richmond kwa niaba yetu?