Sex tourism in Kenya - Cheap Holliday!

Barbarosa

JF-Expert Member
Apr 16, 2015
22,584
27,786
Haya ndiyo madhara ya kuwa cheap Holliday destination huko Kenya, sasa wakenya wamegeuzwa watumwa na mpaka Wazungu wametengeneza filamu juu ya hilo, angalia jinsi watu wanavyodhalilishwa, ndiyo maana naunga mkono Serikali yangu pendwa kudhibiti Watalii masikini, hatutaki kuwa cheap Holliday destination, tunataka Wazungu, Wajapani matajiri na wastaarabu na siyo hawa maloser wa Ulaya kuja kutuharibia vijana wetu na utamaduni wetu!

* Angalia na sikiliza hiyo clip mpaka mwisho na jaribu kuilewa kabla ya kuhukumu!

Hii hapo chini ni sehemu ya hiyo Filamu!
 
Mkuu si bure hata kama ni mahaba na chama yako yamepitiliza, huwezi kuwa na sh 10000 bila sh 100. Acheni dharau kwa watanzania na wananchi kwa dunia nzima.

Nchi yetu maskini halafu bado unaunga mkono ujinga kama huo kweli? Ni kigezo kipi kinafanya useme hatutaki watalii masikini?
Hata kama hela watayoleta ni kidogo lakini inasaidia kujazia kibubu. Ni mwendawazimu pekee anayemdhalau mtu kisa masikini halafu baada ya muda unapokea misaada toka kwa nchi hizohizo ambazo Raia wake unawaona masikini.
Tuache kejeli kwa mambo yanayogusa maisha ya mtanzania moja kwa moja. Hao wakenya siye hawatuhusu lakini kwenye sector ya utalii ni wapinzani wetu wakubwa. Sasa sio wa kupuuza kamwe.
 
Mkuu usishabikie usichokijua. Nani kakwambia kuwa watalii maskini ndio wanafanya udhalilishaji?

Nbda nikupe pa kianzia..... Nrnda loliondo kwa mwarabu (Jamaa anapokea Royal family) alafu angalia mambo yanayofanyoka.

Amini nikwambie hao unaowaita "watalii maskini" Ndio wanatoa ajira za kutosha kwa vijana wetu.

Nakuonea huruma wewe unayeushabikia usichokijua, na kwataarifa ndigo huu mchezo hauitaji hasira na watagota kutokana na tamaa zao hapo wengi tutakuwa tumeumia.

Nb.
Clip imeshindikana kufunguka na haya niliyoandika ni kutokana na content uliyoieeka hapo
 
Nani kakudanganya kwamba hao watalii wanaofuata sex huko ni masikini??
 
Huwa nakupenda sana Barbarossa maana huwa una-support ujinga na unaongea kama umekatwa kichwa!
 
Paying for sex sio jambo jipya,lipo kwenye maisha yetu ya kila siku!Nenda sinza halafu lete mrejesho,yanafanyika hayo!kuwashutumu watalii mi naona umeegemea upande mmoja!
 
Mleta uzi mbona unakuwa kama umeshushwa kutoka sayari nyingine leo? Kutumia clip hii ili kuunga mkono kauli ya Waziri Maghembe ni kujaribu, tena kwa makusudi, kupotosha ukweli. Mtatumia kila mbinu kujaribu kupotosha lakini ukweli utabaki kuwa bajeti mliyowaletea wananchi haina chochote na utekelezaji wake unaenda kuiumbua serikali. Kushamiri kwa biashara au vitendo vya ngono hakusababishwi tu na hao mnaowaita watalii uchwara, bali kuna factors nyingi tu. Na hii ni global issue!
Wakati wewe unajipinda kuleta clip hii hapa zaidi ya watalii 8000 wamefuta safari kuja tz na kuelekea Kenya baada ya maamuzi yenu mliyoyafanyia gizani huko Dodoma. Na wakati watalii hao 8000 wanaenda Kenya huku Tanzania kuanzia Tandale, Mafinga, Tunduma, Igoma-Mwanza, na maeneo mengine mengi biashara ya ngono inazidi kushamiri bila uwepo wa hao watalii "uchwara"!
 
Mkuu si bure hata kama ni mahaba na chama yako yamepitiliza, huwezi kuwa na sh 10000 bila sh 100. Acheni dharau kwa watanzania na wananchi kwa dunia nzima.

Nchi yetu maskini halafu bado unaunga mkono ujinga kama huo kweli? Ni kigezo kipi kinafanya useme hatutaki watalii masikini?
Hata kama hela watayoleta ni kidogo lakini inasaidia kujazia kibubu. Ni mwendawazimu pekee anayemdhalau mtu kisa masikini halafu baada ya muda unapokea misaada toka kwa nchi hizohizo ambazo Raia wake unawaona masikini.
Tuache kejeli kwa mambo yanayogusa maisha ya mtanzania moja kwa moja. Hao wakenya siye hawatuhusu lakini kwenye sector ya utalii ni wapinzani wetu wakubwa. Sasa sio wa kupuuza kamwe.

Hatutaki cheap tourism kwa maana madhara yake ni makubwa sana Kiutamaduni na pia siyo endelevu!
Nenda Mombasa ukaone watoto wadogo wanavyotumiwa kwenye sex industry na watalii cheap mpaka UN imetoa tamko, kuna sehemu inaitwa Mtwapa huko Mombasa watoto wadogo wasichana kwa wavulana wanaacha Shule kwenda kulala na Watalii mababu wa Kizungu ktk Ulaya!
 
Mleta uzi mbona unakuwa kama umeshushwa kutoka sayari nyingine leo? Kutumia clip hii ili kuunga mkono kauli ya Waziri Maghembe ni kujaribu, tena kwa makusudi, kupotosha ukweli. Mtatumia kila mbinu kujaribu kupotosha lakini ukweli utabaki kuwa bajeti mliyowaletea wananchi haina chochote na utekelezaji wake unaenda kuiumbua serikali. Kushamiri kwa biashara au vitendo vya ngono hakusababishwi tu na hao mnaowaita watalii uchwara, bali kuna factors nyingi tu. Na hii ni global issue!
Wakati wewe unajipinda kuleta clip hii hapa zaidi ya watalii 8000 wamefuta safari kuja tz na kuelekea Kenya baada ya maamuzi yenu mliyoyafanyia gizani huko Dodoma. Na wakati watalii hao 8000 wanaenda Kenya huku Tanzania kuanzia Tandale, Mafinga, Tunduma, Igoma-Mwanza, na maeneo mengine mengi biashara ya ngono inazidi kushamiri bila uwepo wa hao watalii "uchwara"!

Ndiyo maana nimeandika hapo kabla ya kujibu angalia mpaka mwisho hiyo clip halafu jaribu kuilewa maana yake, sasa unajibu tu bila hata kuelewa hata hiyo clip inahusu nini, ngoja nikuulize, ni kwa nini mambo kama hayo huku kwetu hakuna au niseme angalau siyo kwa kiwango kikubwa kama huko Kenya? Ni kwa nini hiyo filamu itengenezwe Kenya na siyo TZ?
 
Haya ndiyo madhara ya kuwa cheap Holliday destination huko Kenya, sasa wakenya wamegeuzwa watumwa na mpaka Wazungu wametengeneza filamu juu ya hilo, angalia jinsi watu wanavyodhalilishwa, ndiyo maana naunga mkono Serikali yangu pendwa kudhibiti Watalii masikini, hatutaki kuwa cheap Holliday destination, tunataka Wazungu, Wajapani matajiri na wastaarabu na siyo hawa maloser wa Ulaya kuja kutuharibia vijana wetu na utamaduni wetu!

* Angalia na sikiliza hiyo clip mpaka mwisho na jaribu kuilewa kabla ya kuhukumu!

Sex Tourism ni mbaya na inatakiwa kupigwa vita lakini lugha unayoiga ya kusema watalii maskini haifai. Ni lugha ya mtu asiyejifahamu na ni aibu kusikia lugha ya aina hiyo kwa mtu anayeitwa waziri. Huna sababu ya kuunga mkono maneno ya aina hiyo kwa kutumia neno serikali. Serikali gani itakayokuwa na ujinga wa kiasi hicho?
 
Sex tourism huletwa na Watalii masikini, watalii matajiri mara nyingi huwa ni watu wastaarabu na ni nadra hufanya mamabo yasikokubalika kwenye jamii kama kutumia watoto wadogo na kwa sababu tu wana uwezo wa kifedha lkn watalii masikini wao hawana ustaarabu hivyo hufanya hayo mambo na hawajali!
 
Mkuu usishabikie usichokijua. Nani kakwambia kuwa watalii maskini ndio wanafanya udhalilishaji?

Nbda nikupe pa kianzia..... Nrnda loliondo kwa mwarabu (Jamaa anapokea Royal family) alafu angalia mambo yanayofanyoka.

Amini nikwambie hao unaowaita "watalii maskini" Ndio wanatoa ajira za kutosha kwa vijana wetu.

Nakuonea huruma wewe unayeushabikia usichokijua, na kwataarifa ndigo huu mchezo hauitaji hasira na watagota kutokana na tamaa zao hapo wengi tutakuwa tumeumia.

Nb.
Clip imeshindikana kufunguka na haya niliyoandika ni kutokana na content uliyoieeka hapo

Mbona mimi nimekupa kithibitisho, lkn wewe unaniambia tu nenda Loliondo, sema hapa wanafanya nini huko? Wanadhalilisha vipi watu wetu na jamii yetu? Weka data hapa na usisema tu nenda Loliondo hata mimi ningeweza kusema nenda Mombasa ukaone lkn najua hiyo kauli imejaa hewa na ndiyo maana nikaja na kielelezo hivyo nategemea na wewe ufanye hivyo!
 
Nani kakudanganya kwamba hao watalii wanaofuata sex huko ni masikini??

Ndiyo! Sehemu kubwa watalii wanaofanya mambo kama haya ni maiskni au low income huko kwao, watu middle class mara nyingi ni watu wastaarabu wana familia zao na mara chache sana hufanya mambo kama hayo hata hiyo clip anasema huyo mama hapo kwamba huko Ulaya wanawake waliokosa waume hawathaminiwi tena na jamii yao huko lkn wakija Afrika (Kenya) ile rangi nyeupe inatosha kuwafanya Miungu watu na wanagombaniwa!
 
Waje na huku tuwashughulikie hao masugar mummy

Tatizo ni kwamba watoto wanatoroka Shule Wasichana kwa Wavulana kwenda kufanya hiyo biashara, fikiria una binti au Mvulana wa miaka 14 halafu anaondoka nyumbani na kwenda kulala na babu au Bibi wa miaka 60 hiyo inaitwa sex exploitation na ndiyo maana ya hiyo Filamu!
 
Haya ndiyo madhara ya kuwa cheap Holliday destination huko Kenya, sasa wakenya wamegeuzwa watumwa na mpaka Wazungu wametengeneza filamu juu ya hilo, angalia jinsi watu wanavyodhalilishwa, ndiyo maana naunga mkono Serikali yangu pendwa kudhibiti Watalii masikini, hatutaki kuwa cheap Holliday destination, tunataka Wazungu, Wajapani matajiri na wastaarabu na siyo hawa maloser wa Ulaya kuja kutuharibia vijana wetu na utamaduni wetu!

* Angalia na sikiliza hiyo clip mpaka mwisho na jaribu kuilewa kabla ya kuhukumu!

Kijana Masikini wa Kitanzania umekaa kwenye mkeka ukicheza bao hafu unasema "Nataka maisha mazuri".....Hamfanyi chochote kutangaza Utalii wetu, siku zote mnategemea Watalii Hawa mnaowasema Masikini pale wanaporudi makwao ndoa Watangaze mazuri yetu,nao hamuwataki, mnataka Matajiri sasa mtasubiri Milele!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom