Severine Msemwa: Padri aliyefungisha ndoa ya Dkt. John Magufuli na Bi. Janeth

Hussein Massanza

JF-Expert Member
Dec 26, 2012
918
1,994
"Siku mimi nimefunga ndoa, sikuvaa koti, wala mke wangu hakuvaa shela. Tulienda kanisani Chuo Kikuu (UDSM), Padri alitununulia pete, ilikuwa ya shaba, kisha akatununulia soda, nikanywa pepsi, mke wangu akanywa mirinda, mambo yakaishia hapo" Rais Dkt John Magufuli.

Kama ilivyo ada ya JF. Tunaendeleza mijadala pale inapoishia huko nje.

Nimeleta picha ya Padri aliyemfungisha ndoa Rais Dkt John Magufuli, Padri Severine Msemwa. Tunaweza kumpa pongezi kwa wema aliounesha kwa mwanafunzi na muumini wake.

Sidhani kama ni vibaya kuwasifu watu wema ili kuambukiza tabia njema kwa wengine.

Padre.jpg

=============

Historia ya Parokia ya Chuo Kikuu UDSM

Parokia ya Chuo Kikuu ipo katika Chuo Kikuu. Inatoa huduma za kiroho kwa Wanafunzi Wakatoliki wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, chuo kikuu cha ardhi na chuo kikuu cha maji, pia kwa Waalimu, Wafanyakazi na wakazi wa karibu zaidi na vyuo vikuu hivi.

Parokia hii ilikuwa na Kigango kimoja ( Kigango cha Mtakatifu Petro, Changanyikeni), ambacho kwa sasa kimeshakuwa parokia tangu kuanzia mwaka 2017. Kuna Kanda 4 za Wanafunzi, na Kanda 6 za wasio wanafunzi. Kuna jumla ya Jumuiya Ndogondogo (JNNK) 56 za wanafunzi, na JNNK 37 za wasio wanafunzi. Kwa mujibu wa sensa ya 2010/2011, kuna jumla ya Wakristu 3,830 katika Parokia hii, idadi hii ikijumuisha watoto 880 na Watu wazima 2,950.

Kanisa la Parokia ni la mseto, lililojengwa kwa ushirikiano wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC) na Baraza la Kikristu Tanzania (CCT). Huduma za kiroho hutolewa katika Kanisa hili kwa kupeana zamu.

Mwanzoni mwa miaka ya 60, Ibada za Misa Takatifu ziliendeshwa nyumbani kwa Mlezi, wakati ule akiwa Padre Moore. Baadaye mwaka 1967, Ibada ya Misa Takatifu iliendeshwa katika Mhadhara wa Sayansi, SB (Science Theatre B). Katika kipindi hiki, Sakramenti za Ubatizo, Komunio ya Kwanza, Kipaimara na Ndoa zilitolewa katika Parokia ya St. Peter’s Parish, Oysterbay.

Huduma hizi zilianza kutolewa rasmi katika Kanisa la Chuo Kikuu mwaka 1974 kwa upande wa Ubatizo, na mwaka 1980 kwa upande wa Komunio ya Kwanza na Kipaimara. Lugha iliyotumika kuendesha ibada ya Misa Takatifu ilikuwa Kiingereza, mpaka miaka ya 80 ilipobadilishwa kuwa Kiswahili.
 
Pongezi na wema apewe Mungu kwani huyu alikuwa msimamiaji tu na ndiyo kazi aliyotumwa na Mungu kuifanya so ni jukumu lake.

Kingine....tunashukuru kumfahamu!
 
Chuo Kikuu (UDSM), Padri alitununulia pete, ilikuwa ya shaba, kisha akatununulia soda, nikanywa pepsi, mke wangu akanywa mirinda, mambo yakaishia hapo" Rais Dkt John Magufuli


"...nasikia yupo Tanga siku hizi"
 
Kwa Mujibu wa mh anasema alienda na mkewe vipi hiyo ndoa ilifungwa bila wasimamizi?

Mkuu wala hajasema uongo huwa hii inatokea sana, issue huwa hivi kunaweza kukawa na sakramenti ya ndoa kwenye ibada fulani. Baada ya padre kufungisha ile ndoa iliyokuwa kwenye ratiba anaweza kutoa offer kwa waamini ambao wanaishi uchumba sugu (wanaishi bila ndoa ) kwamba ambao wako pale na wako tayari kufunga ndoa watoke mbele wafungishwe, hapa hao wawili wakikubali basi wanafungishwa ndoa, nadhani hiki ndicho kiliwatokea na katika mazingira hayo wasimamizi wanapatikana pale pale kanisani.
 
Ni faraja kuona ulioashiriki kuwaunganisha wanadumu pamoja na changamoto zilizopo,hata uzee wako na wao.
 
Sheria ya ndoa inaseme hivi mkuu
Napa kidogo umeghafilika
Mkuu wala hajasema uongo huwa hii inatokea sana, issue huwa hivi kunaweza kukawa na sakramenti ya ndoa kwenye ibada fulani. Baada ya padre kufungisha ile ndoa iliyokuwa kwenye ratiba anaweza kutoa offer kwa waamini ambao wanaishi uchumba sugu (wanaishi bila ndoa ) kwamba ambao wako pale na wako tayari kufunga ndoa watoke mbele wafungishwe, hapa hao wawili wakikubali basi wanafungishwa ndoa, nadhani hiki ndicho kiliwatokea na katika mazingira hayo wasimamizi wanapatikana pale pale kanisani.
 
Hahahahahaah

Rais kajikuta katangaza bidhaa Za Pepsi bila ya kujua
Angesema nilikunywa soda lakin kutangaza Pepsi Na Mirinda ni Makosa kwenye Anga la Biashara ya 'fair competition'

Rais Jakaya aliwahi kukataa kuvaa tshert ya Kampuni Fulani ya Simu kwenye maonesho Fulani Kwa kuhofia kuingilia Biashara Za watu
 
Back
Top Bottom