Several Kenyan Women from PCEA church THIKA killed in Tanga,Tanzania Accident

habari, mwenye taarifa za kina juu ya kusafirishwa kwa marehemu wa ajali ya Makole.

je wamesafirishwa?

Rafiki, kabla au baada ya kupost jitahidi kusoma thread nyingine zilizoko janvini. JF huwa na majibu mengi......... Na ya kutosha, acha uvivu wa kuperuzi.
 
Serikali ya watu wa Kenya imetoa ndege mbili kwa ajili ya kusafirisha marehemu na wahanga wa ajali hiyo, nadhani hili lingetokea kwa waTanzania (Mungu epushia mbali) serikali yetu ingetoa sijui maguta maana ndege zenyewe za ATCL zote zipo gereji tena gereji bubu
 
NEWS

map.jpg

A google map showing the accident scene at Tanga, Tanzania where at least eight Kenyan church faithful were feared dead after an accident involving two buses in Tanzania August 10, 2012. GOOGLE MAPS

By NATION Reporter

Posted Friday, August 10 2012 at 09:28

Eleven Kenyan church faithful died Friday after an accident involving two buses in Tanzania.

Many others from the Presbyterian Church of East Africa (PCEA) Thika Women's Guild are believed injured.

A church official confirmed the number of those dead and but could not immediately put a figure on the injured.



He said 81 people were on board the buses.

The women's group was headed to the Tanzanian capital, Dar es Salaam for a retreat when the accident occurred at Chalinge, 20 kilometres from Tanga at around 5.30am Friday.

According to eyewitnesses, one of the buses apparently stalled and its occupants called for help from colleagues on the other vehicle.

Reports indicate that the bus turned back in response to the distress calls.

At the scene, a truck rammed both buses from behind.

Rescue efforts are underway

 
Julieth Ngarabali, Pwani na Hamida Shariff, Morogoro

WATU 11 wanaoaminika kuwa raia wa Kenya wamefariki dunia papo hapo, huku wengine saba wakiwa mahututi baada ya mabasi waliyokuwa wakisafiria kutoka Nairobi kwenda Dar es Salaam kupata ajali katika Mto Wami mkoani Pwani.Mbali na vifo hivyo, ajali hiyo pia ilisababisha majeruhi 25 na saba kati yao waliripotiwa kuwa mahututi na walipelekwa katika Hospitali ya Tumbi, Kibaha kwa matibabu.


Ajali hiyo ilitokea katika Kijiji cha Makole, wilayani Bagamoyo wakati abiria hao ambao ni wanakwaya walipokuwa wakisafiri kutoka Kenya kwenda Dar es Salaam kushiriki katika tamasha la uimbaji.

Ajali hiyo ilitokea jana saa 11 alfajiri ikihusisha magari manne, mawili kati yake yakiwa ni mabasi hayo yakitokea Kenya na malori mawili ya hapa nchini.Tukio hilo pia lilifunga Barabara Kuu ya Chalinze - Segera kwa zaidi ya saa nane hivyo abiria waliokuwa wakisafiri kuelekea na kutoka mikoa ya Kaskazini ikiwamo nchi ya Kenya kwenda na kutoka Dar es Salaam kukwama.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Ernest Mangu alisema raia hao wa Kenya ni waumini wa Kikristo na walikuwa wakielekea Dar es Salaam kwenye tamasha la kwaya.

Ajali ilivyotokea
Mangu alisema awali, mabasi hayo yalikuwa yametokea Segera, huku yakiwa yameongozana na moja ilipofika eneo la Makole ghafla liliyumba na kupinduka kisha kutumbukia kwenye korongo.Alisema basi la pili lililokuwa likifuatia nyuma lilipita eneo hilo, lakini baada ya mita 500, dereva alipigiwa simu na mwenzake kuwa amepata ajali na wametumbukia korongoni hivyo ikawalazimu kugeuza kurudi nyuma ili wakawasaidie wenzao.

“Haikuwa rahisi kwa mtu ama gari kuliona haraka hivyo wenzao walipofika hapo nao walipita bila kujua kama kuna gari limeanguka, lakini muda mfupi tu dereva alipigiwa simu na mwenzake akimjulisha kuwa amepata ajali na wametumbukia mtaroni,” alisema Kamanda Mangu.
Alisema baada ya kugeuza na kurudi eneo la ajali, baadhi ya abiria walishuka ili kuwasaidia wenzao na wakati wakiwa kwenye harakati hizo, ghafla lilitokea lori ambalo lililiparamia basi la pili ambalo pia lilitumbukia kwenye korongo.

Kamanda huyo aliongeza kuwa, wakati basi hilo likigongwa, tayari lilikuwa limegeuzwa kuangalia uelekeo wa Chalinze na kwamba baadhi ya abiria walikuwamo ndani.
Alisema baada ya lori hilo kuligonga basi hilo, liliendelea mbele kwa kasi na kugongana uso kwa uso na lori jingine lililokuwa likitokea uelekeo wa Segera, hivyo kufunga barabara hiyo kwa zaidi ya nane.
“Kwa hiyo njia ilikuwa imefungwa kuanzia saa 11:00 alfajiri hadi saa 6:30 mchana baada ya askari wetu kufanikiwa kuyaondoa malori hayo kwenye barabara kuu na sasa (jana) safari zinaendelea kama kawaida,” alisema Mangu.

Majeruhi
Baadhi ya majeruhi walitibiwa katika Zahanati ya Chalinze na baadaye kuhamishiwa katika Hospitali ya Tumbi.
Hata hivyo, RPC Mangu alisema baadaye majeruhi na miili ya marehemu wote walihamishwa na kupelekwa Hospitali ya Taifa Muhimbili kutokana na maombi ya Ubalozi wa Kenya nchini.
Habari zilizopatikana jana jioni zinasema kuwa Serikali ya Kenya kupitia ubalozi wake hapa nchini ilikuwa ikifanya mipango ya kuwarejesha nyumbani majeruhi na baadaye maiti kwa ajili ya mazishi.
Ajali hiyo ni kati ya saba ambazo kwa mujibu wa Mangu zilizotokea usiku wa kuamkia jana na baadhi yake zilisababisha majeruhi zaidi ya 20 katika maeneo ya Msata, Chalinze na Mbala, wilayani Bagamoyo.

Ajali za Sumry, Allys na
Shabiby ndani ya dk 10

Kutoka Morogoro; watu 45 wamenusurika kufa kwa ajali baada ya mabasi matatu waliyokuwa wakisafiria kuacha njia na kupinduka eneo la Mkundi kwa Makunganya nje kidogo ya Manispaa ya Morogoro, katika Barabara ya Morogoro - Dodoma.
Ajali hiyo ilitokea saa 2:30 asubuhi kwa kuhusisha mabasi matatu, Kampuni ya Shabiby lililokuwa likitokea Dodoma kwenda Dar es Salaam, Allys Sport na Sumry yaliyokuwa yakitokea Morogoro kwenda Mwanza.

Baadhi ya majeruhi waliokuwa wakisafiri na basi la Shabiby walisema basi hilo lilianza kuyumba na baadaye kuacha njia kisha kupinduka.Mmoja wa abiria hao, Rashid Shaaban alisema baada ya basi hilo kupinduka, ghafla waliona basi jingine la Sumry likiacha njia na kupinduka wakati lilipojaribu kulipita gari jingine jirani na eneo hilo.Alisema kuwa wakati kukiwa na msongamano wa magari katika eneo hilo la ajali, basi jingine la Allys Sport liliacha njia na kupinduka na hivyo kutokea ajali tatu katika muda usiozidi dakika 10.

Shaaban alisema baada ya ajali hizo walitokea watu waliokuwa wakijifanya kutaka kutoa msaada, lakini lengo lao lilikuwa ni kuiba mali za majeruhi. Hata hivyo, alisema lengo lao hilo halikufanikiwa kwani muda mfupi baada ya kutokea, askari walifika na kuimarisha ulinzi.
Katika Hospitali ya Mkoa wa Morogoro, madaktari na wauguzi walionekana kuzidiwa na wagonjwa kutokana na idadi kubwa ya majeruhi waliokuwa wakihitaji huduma.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Faustine Shilogile alithibitisha kutokea kwa ajali hizo na kusema kuwa uchunguzi wa awali umebaini kuwa zimetokana na utelezi na mwendo kasi.
Hata hivyo, alisema kuwa uchunguzi unaendelea ikiwa ni pamoja na kuwahoji madereva wa mabasi hayo.

Maafa
 
Mkuu ajali hii imenisikitisha SANA, nawapa pole Serikali ya Kenya na ndugu za walio tangulia mbele ya haki; wengi wa wahanga hao walikuwa ni wanawake-very sad indeed. Hivi hiyo saa kumi na moja asubuhi bado kuna giza sana au nini, ilikuwaje basi la wenzao kupita katika eneo la ajali bila ya kujuwa kilicho tokea mpaka walipo pigiwa simu.

Kusema kweli barabara hii ya Morogoro ni kama "HELL RUN"! Barabara yenyewe ni nyembamba alafu madereva wa mabasi na heavy duty vehicles zinakwenda at a cut throat speed bila ya kujali sheria za barabarani!
 
Poleni wahusika

Hivi hii nayo ni laana??

Nakumbuka ajali ya meli zanzibar kuna wachungaji walidai hii ajali ni laana baada ya wamsho kuchoma makanisa zanzibari. sasa tusubiri watasemaje kuhusu wana kwaya wa kanisaaa ..
 
Poleni sana ndungu zetu wa Kenya kwa kuwapoteza dada zetu,kaka zetu,mama zetu na baba zetu, mungu aziweke roho za marehemu mahali pema peponi amen
 
11 Kenyans dead in Tanzania road crash

map.jpg


By NATION Reporter
Posted Friday, August 10 2012 at 09:28

The women's group was headed to the Tanzanian capital, Dar es Salaam for a retreat when the accident occurred at Chalinge, 20 kilometres from Tanga at around 5.30am Friday.

At the scene, a truck rammed both buses from behind.

Rescue efforts are underway.

11 Kenyans dead in Tanzania road crash- News|nation.co.ke

Poor journalism,

RIP wafiwa.
 
Glad the survivors are all back in Kenya for treatment and the governments supports for the deceased and their families.
 
Back
Top Bottom