Seriously, natafuta mwekezaji anunue ikulu

mpayukaji

JF-Expert Member
Oct 31, 2010
940
349
ikulu.jpg

Kama mtanzania ninayeambiwa nina haki juu ya nchi yangu, nimeona heri nibinafsishe ikulu yetu kwa vile imegeuka yao na haiingizi faida. Nafanya hivyo baada ya kusikia maoni ya gwiji la uwekezaji Benjamin Mkapa aliyesema kuwa waliamua kubinafsisha mali za umma kwa vile zilikuwa haziingizi faida zaidi ya hasara. Hivyo nami naona tuanze na ikulu kwa vile, licha ya kuwa chaka la mafisadi, imekuwa ikiliingizia taifa hasara hasa kutokana na wakazi wa mle kufanya watakavyo bila kuguswa. Wanapenda sana matumizi makubwa na kuzurura hata bila kujipa nafasi ya kufikiri na kufanya kazi yoyote zaidi ya uharibifu. Hivyo natangaza rasmi kuwa kama mtanzania nataka nipewe haki yangu ambayo ni kubinafsisha ikulu ilil angalau tupate watu wenye akili ili tutie akili.
 
Mpayukaji!
Hold on this could amount into treason watch your identity. You have gone overboard. If you are serious Ikulu is a sacred place you won't get buyers just think twice. Create a more functional thread.
 
Ooh...oooh!!
...mara ngapi?, mbona kama inamilikiwa na chama flani vilee!
Au kwa vile hawajabadili rangi!
 
At least ungeipeleka kwenye jukwaa la jokes, ila kuileta hapa kama serious post u r very wrong!
Naamini unaelewa unyeti wa ikulu sema tu umeamua kuandika huu mzaha.
Waliomo mule ndani hubadilika ila ikulu hubaki palepale.
 
Toa upuuzi wako huu. Kwanza aliyekuruhusu kupiga picha Ikulu ni nani?. Ikulu sio mahali pa kuchezewa hivi Mpayukaji ww. Hii nchi kuna uhuru wa kupayuka na sio kuchea ikulu. Mimi siipendi CCM kutokana na uozo wanaoutenda, Lakini siwezi chezea ikulu.
 
Mokerema try to live in terms of today not a thousand years ago. Your 'sacred' ikulu ceased to be the day Nyerere vacated it. Currently it is just like any shop where justice is sold
 
Mi nilishainunua tangu mwaka juzi, nalipa kwa installment na mwakani namalizia final installment.
 
Gembeson bado unaishi kwenye mwaka arobaina na saba siyo? Hivi kosa ni kupayuka au kuchafua ikulu? Kosa langu nini iwapo huoni kosa la wale walionilazimisha kupayuka? Anyway, ukielimika utajilaumu na kuniomba radhi. Otherwise acha ushama bro au sissy.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom