Seriously...Hivi MAFUTA ya TRANSFORMER Wanayaiba Kwa Ajili Ya Matumizi Gani?!!

Steve Dii

JF-Expert Member
Jun 25, 2007
6,402
1,254
Baada ya habari za uhalifu wa mara kwa mara uhusianawo na wizi wa mafuta ya transformer, tafadhali sana naomba mnisaidie kujua... ukiachia mbali matumizi yake yaliyokusudiwa ndani ya transformer za kupozea umeme kwenye gridi za Taifa, hivi hayo mafuta yanatumika kufanyia nini?!

Akhsante.

SteveD.
 
Steve, wewe unajua bwana sema unataka kujua wakinanani wanahusika humu JF.
 
Aisee, Kunta.... kweli kabisa napenda kujua tu matumizi yake. Kamwe huu si mtego..

Akhsante kwa wazo...

SteveD.
 
Steve, wewe unajua bwana sema unataka kujua wakinanani wanahusika humu JF.

ha ha ha haaa....!!!

duh... ha haaa... aisee, yaani kumbe kuna watu wana madili hayo humu? ha ha haa...

Anyway, naskia hayo mafuta wanayatumia wakaanga chipsi/samaki mitaani kwakuwa hayaungui haraka kama haya mafuta ya kupikia ya kawaida. Side effects zake nini, mie sijui ila kama yanafaa kwa transfoma, naamini kwa binadamu ni mtego!
 
Nimewahi kusikia kuwa mafuta hayo ni mojawapo ya malighafi ya kutengenezea Mkorogo, aidha malighafi zingine ni pamoja na maparachichi....
 
ukiangalia thamani ya vitu kama mkorogo au kukaanga chips, cost-benefit ya wizi wa mafuta hayo haiwezi kuwa justified.

Ukweli ni kuwa mafuta hayo yanatumiwa na watu wenye malori/mabasi yaendayo safari za masafa. Mafuta hayo yanadaiwa kudumu kwa muda mrefu na yanasaidia kupooza engine. They are too expensive to be bought in the open market.

Swali ni kuwa : TANESCO wako serious kuzuia wizi huo?
 
Mgirima, Swali lako zuri sana.... na kwa kweli kama wako serious ni lazima waje na mbinu kabambe ya kuzuia wizi wa mafuta....

Wazo langu hapa ni kuwa; kwanini wasiagize mafuta hayo wao wenyewe na kuwa uzia wenye malori/mabasi?! Nina imani kuwa kama Tanesco wanahitaji kupunguza wizi huu, na sababu ya wizi huu unasababishwa na mahitaji ya oil za magari makubwa, basi sioni haja ya transformers kuendelea kulipuka na kuleta hasara kubwa zaidi na kero juu yake..... hali Tanesco wanaweza kabisa kuyaagiza kihalali mafuta hayo na kuwauzia wenye mahitaji moja kwa moja, hivyo kuepusha transformer zao kunyonywa mafuta..... Unajua wenzetu wanaule msemo "extreme circumstances merit extreme measures"...... mimi nadhani ni huu ni wakati mwanana kwa Tanesco kuchukua extreme measures!!

SteveD.
 
Kukaangaa Samaki

Hii ni mojawapo, mi nimeambiwa pia hutumika sana na watu wapika chips mitaani. Tofauti yake na mengine ni kuwa, haya una-add kidogo na yale mengine na utayapikia Chips mwezi mzima hivi, hayaishi.

Best Believe that!
 
Uzembe juu ya uzembe!

2uj4k03.jpg

Picha kwa hisani ya: mjengwa.blogspot.com

Inasikitisha!! Ama kweli ndivyo tulivyo....

Hivi inagharimu kiasi gani kujengea uzio ulio imara kuikinga hiyo transformer ya mamimilioni? Matokeo yake tunaishia kuombea Mungu eti isitokee tu... kumbe ni uzembe wa kuzuilika. Hao hao Tanesco wanaweza kuanza kulalama transformer zao zinagongwa na magari... na hao madereva nao wanaweza kulalama transformer za Tanesco zinalipuka na kuwapatia madhara. One disgrace after another. Na mijitu mingine ndiyo kwa kujifanya mission town inadiliki hata kwenda kupandika matangazo kwenye transformer hizi. It is disheartening to say the least. :(

SteveD.

My God vua likidondoka jingi na maji kuifunika hii mashine nini hivi hutokea. Nafikiri Nabii Issa aje tu kutuchukua maana wanadamu wengine wan maana mbaya na sisi Watanzania, watuibie, watuuwe, watudharau, watumasikinishe, watubomolee nyumba, watunyime au kutuzuia au kutucheleweshea huduma za jamii, na sasa mambo namna hii.

Kwanza hapa ni wapi isijekuwa Zimbabwe hapa. Aisee! Na kama ni Tanzania je iliko hii mashine na BOT na Ikulu kuna umbali gani na je barabara hii wakuu hawakatizi kabisa? Hadi kamera ya Mzalendo Mjengwa imeona na haina damu wala haina uhai. Jamani jamani kweli hi kasi mpya ya kuelekea ujinga na umasikini zaidi 360mph na maradhi usiseme.
 
ukiangalia thamani ya vitu kama mkorogo au kukaanga chips, cost-benefit ya wizi wa mafuta hayo haiwezi kuwa justified.

Ukweli ni kuwa mafuta hayo yanatumiwa na watu wenye malori/mabasi yaendayo safari za masafa. Mafuta hayo yanadaiwa kudumu kwa muda mrefu na yanasaidia kupooza engine. They are too expensive to be bought in the open market.

Swali ni kuwa : TANESCO wako serious kuzuia wizi huo?

Haya nadhani yatakuwa yale malori makuukuu yenye miaka si chini ya 30 kama Bedford, Leyland, Scania, Fiat yaliyofanyiwa modification kiasi kwamba yanakwenda hata kwa mafuta ya alizeti.
 
Mafuta ya Transfoma yanatumika kukaangia chips sifa yake kubwa yanachukua muda mrefu kwisha yaani lita 4 unaweza kukaanga chips mwezi mzima ilhali katika hali ya kawaida ingekutuma debe 5 za Mohammed Enterprises
 
Baada ya habari za uhalifu wa mara kwa mara uhusianawo na wizi wa mafuta ya transformer, tafadhali sana naomba mnisaidie kujua... ukiachia mbali matumizi yake yaliyokusudiwa ndani ya transformer za kupozea umeme kwenye gridi za Taifa, hivi hayo mafuta yanatumika kufanyia nini?!

Akhsante.

SteveD.

Heshima jako Mkuu,

Mafuta ya Transfoma yana matumizi makuu mwawili na yo ni:-

1. Kukaangia Samaki/Maandazi/Chips na Vitu vyote vinavyo tumia mafuta kukaangia. Hapa ieleweke kuwa hajatumiki mafuta ya transfoma pekee ila yanawekwa kiasi kidogo tu kwenye karai na kuchanganywa na ya kawaida imethibitika kuwa haya mafuta yanasaidia mafuta ya kupikia/vegetable oil yanakuwa hayaishi hivyo kuweza kumudu ugumu wa maisha na kupata faida kwenye biashara tajwa. Hii ndio how to be creative! Wabongo wamefanya hiyo research jamani! Kwli ugumu wa maisha kipimo cha akili.

2.Mafuta haya yanatumiwa pia katika maswala ya urembo! Hapa inahusu mkorogo ule kuna wanaosema mafuta hayo huchanganywa na mavi ya kuku na vitu vinginevyo ili kuupata weupe hayo ndio mambo ya urembo wanasema waungwana ukitaka uzuri lazima udhurike maana kiwango kikikosewa si ajabu mtu kubabuka uso na kuwa na ngozi kama ya kenge.

Alamsiki
 
Wanajamvi nafahamu kuwa wengi wetu tumeshasikia juu ya matumizi ya mafuta hayo kukaangia viazi(chips).
Mara nyingi sipendi kuamini maneno ya vijiweni, hivyo nimekuja kwenu nikiamini kuwa naweza kupata taarifa makini toka kwenu. Je, hili swala lina ukweli?
 
Tena ilikuwa ni wakati muafaka Serikali kukemea na kuelezea ubaya wa mafuta ya Transformer kutumika kupikia chips kuliko kujikita katika mafuta ya ubuyu ambayo wananchi wameyatumia kwa muda mrefu tena hata huyo anaye kanusha akiwa mmoja wapo.

Inasemekana kwamba kuna vijana wanatumia mafuta ya transformer kupikia chips kwasababu mafuta hayo hayaishi haraka na hayachafuki kutokana na moshi mara zote ni mafuta yaliyo safi na yanadumu kwa takribani miezi sita hivi kwa lita moja. Najisikia nafsi inanisuta hata ninavyobdika duration yake ya miezi sita maana kama wahalifu wa chips wakiona hii watawalisha watu wengi mafuta ya transformer huko mitaani.
 
Ingekuwa vizuri kama tungepata eye witness person au mtaalamu aje kutueleza chemistry ya mafuta hayo na kama kweli yanaweza kutumika kwa matumizi yanayodaiwa na watu.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom