Seriously...Hivi MAFUTA ya TRANSFORMER Wanayaiba Kwa Ajili Ya Matumizi Gani?!!

Hata mimi pia natokea huko huko vijiweni, ila maarifa ya matumizi ya mafuta ya transfoma ninayo!
 
Mafuta ya transformer yapo kundi gani katika extraction ya crude oil? Tuanzie hapo
 
kweli kabisaaa...kama huamini nenda mitaa ya mama john pale mbeya utapata walau ka uzoefu juu ya hii kitu na ufanisi wake jinsi ulivyo malidhawa katika kazi ya kukaanga chipsi.
 
Mafuta ya transformer yapo kundi gani katika extraction ya crude oil? Tuanzie hapo

Nadhani kwenye transformer yanatumika kama coolant hivyo yatakuwa kwenye kundi la oil i.e baada ya diesel na kabla ya grease.
 
Ngoja waje wataalamu wa mafuta ya vilainishi watujuze kuhusu hili jambo.
 
Yanatunika kwenye viwanda vya chuma... na hata kwenye magari wanachanganya na diesel... kuipata gari nguvu zaidi, ila baada ya muda pump ya gari inakufa kwa sababu ni mepesi sana...
 
Kuna watu wanaagiza matransfoma wanakosa pa-kuyauza, sasa mimi nahisi ili wauze inabidi hizi zilizopo ziharibike kwanza, si ndio?
 
Kwa skendo za huku uswazi ni kwamba futa la trans ukichanganya na la kupigia unaweza ukakaanga gunia zima kwa lita tano tu....
Ina maana futa la trans linazuia chips kunyonya mafuta mengi unapozikanga? Hii inataka tafiti zaidi pamoja na madhara ya mafuta ya trans kwa mlaji.
 
Kazi nyingine ya mafuta ya transfoma ni kuendeshea mitambo viwandani sambamba na kuchanganywa kwenye vipodozi mbalimbali.
 
Back
Top Bottom