Serious Business: Nani ana hali nzuri leo; Mtanzania, Mtunisia au Misiri? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Serious Business: Nani ana hali nzuri leo; Mtanzania, Mtunisia au Misiri?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kichuguu, Feb 12, 2011.

 1. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #1
  Feb 12, 2011
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,202
  Likes Received: 863
  Trophy Points: 280
  Matukio yaliyotokea Afrika mwanzoni mwa mwaka huu ni fundisho kubwa sana kwa nchi ambamo raia wake wanaishi maisha ya ufukura sana huku wachache wao wakiwa wanaishi kama wako kwenye bustani ya Aden.

  Kitu cha kwanza kwa umuhimu katika uhai wa binadamu na viumbe vyote ulimwenguni ni maji; ndiyo maana NASA imekuwa inafanya utafaiti wa kujua ni sayari gani nyingine zaidi ya dunia ambayo ina maji. Kwa Afrika, Tanzania ni nchi pekee yenye akiba kubwa sana ya maji (yanayoimarisha uhai) kuliko nchi nyingine yoyote ya Arfika. Zaidi ya kuwa na akiba ya maji kwenye maziwa yetu, Tanzania pia ina madini mengi sana kuliko nchi yoyote Afrika; tuna dhahabu, almasi, Tourmaline, Ruby, chuma, makaa ya mawe, Cobalt, Chromium, Alexandrite, Tanzanite, na madini mengine mengi sana. Zaidi ya maji na mdaini, Tanzania ina ardhi kubwa sana yenye rutuba (hatuna jangwa), halafu watu wetu ni watulivu sana wenye kupenda kuheshimu sheria inayolinda amani. Pamoja na hayo yote, Tanzania bado ni nchi maskini sana duniani ikiwa ni kati ya nchi kumi maskini: yaani inachanganywa na kuzidiwa na visiwa vya Haiti visivyokuwa na raslimali yoyote, na inashindana Jamhuri ya Somalia ambayo imekuwa na vita ya wenyewe kwa wenyewe kwa zaidi ya miongo miwiili sasa.Kuna watanzania wachache sana ambao wana connection ndio wafaidi kwa gharama ya watanzania wengine wote kwa kupitia kamisheni za 10%, 20% na viu kama hivo.

  Tatizo letu ni nini?

  Leo hii tunazidiwa kwa mbali sana na Rwanda, nchi ambyo watu wake tumewafadhili kwa zaidi ya miaka arobaini wakiwa wanauana wenyewe kwa wenyewe. Kuna watu wengi sana wengine wakiwa ni wabaya wetu ambao wameshagundua udhaifu wetu kama watanzania. Sasa hivi wamekuwa wanatumia udhaifu wetu huo kutuangamiza zaidi. Je tutendelea kuangamia namna hiyo hadi lini? kama wenzetu huko kaskazini wamefanikwa kuwandoa viongozi wanaowapotosha kwa kuwapinga hadharani, je sisi tunashindwa nini

  Kwenye uchaguzi uliopita, wote Mubaraka na Bin Ali walikuwa wamepata zaidi ya asilimia 99, lakini leo wameng'olewa madarakani kutokana na ugumu wa maisha ya watu wao; je Tanzania tunangoja nini? Maisha yuetu ni mazuri kuliko ya Tunisia na Misri? Nadhani wakati huu ndio mzuri sana kwetu kuanza mara moja kujiweka katika njia ya jinsi tunavotaka kuishi maisha yetu ya baadaye kabla dunia haijanyamza.

  It is tricky, lakini kweli mnasemaje wenzangu? Haiwezekani Tanzania tuwe na raslimali zote hizo kwa ajioli ya watu wengie tu; lazima tujitazame tena, na kusema sasa basi.

  Tanzania na sisi tuamke!!!!!!!!!!!!

  (------nitaedit baadaye typos kwenye post hii-----------)
   
 2. BONGOLALA

  BONGOLALA JF-Expert Member

  #2
  Feb 12, 2011
  Joined: Sep 14, 2009
  Messages: 13,782
  Likes Received: 2,392
  Trophy Points: 280
  slogan NCHI YETU YA AMANI!m....****!
   
 3. Speaker

  Speaker JF-Expert Member

  #3
  Feb 12, 2011
  Joined: Aug 12, 2010
  Messages: 6,357
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Watanzania wana raha sana narudia kusema,...
  polisi wanakula na kulala vyema,.....watoto wao wanasoma elimu bora......
  walimu mishahara ni mizuri sana na kwao hakuna mifumuko ya bei........
  wanajeshi ndo usiseme,wanakula kuku kwa mrija................
  Mtaani watu wana "party" kila siku,yaaani sherehe kama wakati wa mavuno vile.......

  Waandamane watanzania kwa lipi?
  Au,waache wa furahie maisha yao
   
 4. Mallaba

  Mallaba JF-Expert Member

  #4
  Feb 12, 2011
  Joined: Jan 30, 2008
  Messages: 2,560
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 133
  we are even worsier than those from Egyypt and Tunisia.
   
 5. Mallaba

  Mallaba JF-Expert Member

  #5
  Feb 12, 2011
  Joined: Jan 30, 2008
  Messages: 2,560
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 133
  wananchi wanaodanganywa kwa kutishiwa Amani siku zote huwa ni masikini na hiyo ndiyo hali hakisi ya Tanzania.
  Nchi zote zilizoendelea kwa njia moja ama nyingine zilipitia au zinapitia social/political/economical conflicts like civil war in USA during MLK ndio hayo matunda ya USA kwa sasa.
  Ukiangalia China pia utaona yale maandamano yaliyofanyika TianAnmen Square ingawa watu wengi waliuliwa hiyo ndiyo iliyokuwa turn up point kwa China , na mifano mingine mingi tu.
  Ttaizo kubwa wa watz ni kuwa ni waoga na wanafiki sana katika mambo ya msingi.Mtu anaumwa amelazwa hospitalini unamwuliza anakujibu SALAMA, je hiyo salama iko wapi? tumezoelea?
  hiyo ndio hali kadhalika yetu tumezoelea kila kitu, tumezoelea kutoa Rushwa na tunaona ni sehemu ya maisha yetu eti nisipotoa sitahudumiwa, wakati mwingine hata mhusika hajakuomba ila ni ujinga na uwoga wetu wenyewe mtu unaanza kutoa pesa mwenyewe?
  Una nunua haki yako? je hao waliopewa kulinda haki hizo wanapoona hayo sio kwamba ndio wanaanza kupigilia kabisa.
  Matatizo yetu mengi yamesababishwa na sisi wenyewe.
   
 6. Mallaba

  Mallaba JF-Expert Member

  #6
  Feb 12, 2011
  Joined: Jan 30, 2008
  Messages: 2,560
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 133
  kweli watz wanaraha sana tena ya kupindukia.
  Ni wazembe sana wakufikiria kwani hapa ni wachache mno kwenye majukwaa ,jaribu kuwauliza wengine watakueleza walivyochoka na kuridhika.
  Watz wameridhika sana hata kwa kula mlo 1 kwa siku.
  Hata kwa kudanganyw kila siku na ahadi za uongo bado wameridhika
  sasa utamsaidiaje mtu aliye ridhika?
  Ni sawasawa na Mwanamke aliyeolewa na huwa anapata kipigo kila siku kutoka kwa mme wake ,pamoja na ushauri wote bado alishangangania , kisa nini? anampenda mme wake.
  Hivyo sioni ajabu kuona kuwa hata watz wengi bado wanampnda sana NDULI CCM
   
 7. M

  Mapinduzi JF-Expert Member

  #7
  Feb 12, 2011
  Joined: Aug 23, 2008
  Messages: 2,427
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  haya matukio mwalimu kichuguu hayatokei Afrika bali mashariki ya kati, au tuseme in the Arab world.

  Tunisia, Egypt, Algeria ni Afrika?
   
 8. n

  ngoko JF-Expert Member

  #8
  Feb 12, 2011
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 574
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  tuko gizani akili zetu zimefugwa na ufito wa green na njano, Hatujui kama jamaa tunaowachagua wanamchango mkubwa kwenye ugumu wa maisha yetu badala yake wakifika kwenye majukwaa wanamsingizia Mwenyezi Mungu hajaleta mvua ya kutosha , akileta mvua ya kutosha wanasema kaleta mafuriko etc.
   
 9. Speaker

  Speaker JF-Expert Member

  #9
  Feb 12, 2011
  Joined: Aug 12, 2010
  Messages: 6,357
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135

  Hayo tunayo yaona kwa wenzetu tuendelee kuyaona tu,ila kwamba watapatikana watanzania wenye uchungu na nchi yao au watanzania watakoa onewa walie au waseme tumeonewa!!!!!!

  Kizazi kijacho,100 years from now
   
 10. Speaker

  Speaker JF-Expert Member

  #10
  Feb 12, 2011
  Joined: Aug 12, 2010
  Messages: 6,357
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135

  Black people are black even in their minds,...hebu angalia waarabu wanavo ondoa madikteta kwao,zimbabwe vipi?
  Wanaotea moto,tanzania ndo usiseme kabisaaaaa
   
 11. M

  Mapinduzi JF-Expert Member

  #11
  Feb 12, 2011
  Joined: Aug 23, 2008
  Messages: 2,427
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Miaka 50 ya uhuru bado hatuna umeme reliable, na asilimia zaidi ya Watz hawana access na umeme. Kwa nini?

  Hilo la kuanza nalo, watanzania na wanaharakati tulishikie bango tudemand right ya kupata umeme reliable kwa watanzania wote. Tumechoka kukaa gizani, si enzi za ujima hizi.

  Hili litazaa mengine yote. Hatua moja huzaa nyingine.
   
 12. Mallaba

  Mallaba JF-Expert Member

  #12
  Feb 12, 2011
  Joined: Jan 30, 2008
  Messages: 2,560
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 133
  hivi wewe unaishi afrika ya wapi? hujui kuwa Egypt,Tunisia na Algeria ni North Africa? au kwa kuwa wao ni waarabu? mbona wako AU ?:clap2::clap2:
   
 13. Mallaba

  Mallaba JF-Expert Member

  #13
  Feb 12, 2011
  Joined: Jan 30, 2008
  Messages: 2,560
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 133
  There are currently 8 users browsing this thread. (5 members and 3 guests)
  Hapa inaonyesha kuwa kazi bado sana kwa watz:coffee::laugh:
   
 14. Semilong

  Semilong JF-Expert Member

  #14
  Feb 12, 2011
  Joined: Mar 5, 2009
  Messages: 1,711
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  nina rafiki yangu mmoja mganda nilimwambia kuwa museveni ni next kutolewa akaniambia we east africans are cowards. lakini ukiangalia ata egyptians walikuwa waoga ndio maana jamaa aliwatawala for 30yrs, lakini vagi lilivyoanza hawakusimama mpaka jamaa ameng'okatofauti iliyokuwepo kwa sub sahara africa ni kuwa elimu ndogo kwa hiyo divide and rule ni kitu kirahisi na hichi ndio kinachotokea zimbabwe leo hii na hata TZ na ccm
   
Loading...