Bill
JF-Expert Member
- Oct 5, 2007
- 8,414
- 8,686
Ni habari mbaya na kusikitisha kusikitisha kusiskia na kuona Ma albino wanaenedelea kuuawa ndani ya nchi yao wakati serikali inayopaswa kuwahakikishia ulinziikiwa haichukua hatua za ziada na makusudi kuwalinda.
Vitendo vya kikatili dhidi ya Ma albino vimekuwa vikiongezeka kila kukicha. Hapo tarehe 03/05/08 Mwananchi liliripoti kisa cha Vumilia Makoye mkazi wa kijiji cha Ilunga wilayani Magu kukatwa panga kisogoni na kisha kukatwa Mguu sehemu ya paja na wauaji hao kutokomea na mguu kusikojulikana.
Sidhani kama ikiwa wana jamii hawawatambua watu wanaotekeleza unyama huu, siamini kabisa ikiwa nguvu iliyotumia kumng'oa kanali Bacar visiwa vya Commoro inashindwa kutumika kuwang'oa makafiri hawa, haingii akilini kuona mfano wa mauji ya kimbali kama ya Rwanda yanatokea kwa kundi fulani la watu katika nchi ya Tanzania huku serikali ikishindwa kuchukua hatua kali na madhubuti ili kudhibiti.
Nashawishika kuamini kuwa, kuendelea kwa mauaji ya kundi hili la Ma albino serikali imeshindwa!!!!!!!! Kwani haitoshi tu kusema IMANI ZA KISHIRIKINA. Hawa wanaotekeleza mauaji haya tunawafahamu.
Hebu jaribu kusimama katika nafasi ya Vumilia Makoye ghafla watu wanakupiga Panga na kuondoka na Mguu wako. Hakika inauma sana. Hebu fikiria Ma alibino wengine wanaishi maisha gani kutokana na wimbi hili la kuwasaka na kuwa geuza deal.
Ikiwa serikali imeweza kukomesha ujambazi, kwa hili inatania.
Kutokana na hali hii nawaomba wana JF tujitokeze kuweza kuwasaidia ndugu zetu hawa Ma albino. Tuwataje kwa majina wapangaji, watekelezaji, mawakala, na wanunuaji wa viungo vya Ma albino. Naamini hapa JF hakuna linaloshindikana.
Kwa pamoja tutashinda.