Serikari yabaini mtandao wa watu wanaowaleta walemavu na kuja kuwatumikisha hapa Dar es salaam

BVR 2015

JF-Expert Member
Jul 29, 2015
227
410
Serikali imegundua mtandao wa watu ambao uwakusanya walemavu nchini na kuja kuwatumikisha mjini Dar es salaam kwa ajili ya kujipatia kipato.

Walemavu hao wapatao 25, wamegundulika wakiwa wamehifadhiwa katika gesti moja hapa Dar es salaam maeneo ya Tandare karibu na Manzese.

Timu ya viongozi ikiwa na naibu waziri wa afya na mkuu wa wilaya ya Kinondoni walifanya uvamizi katika hiyo gesti na kuwakuta hao walemavu wakiwa wamehifadhiwa ndani.

Katika ilo tukio naibu waziri aliwaadhibu fimbo 5 kwa kila anaewasaidia hao walemavu kusukuma hizo baiskeli.
 
Attachments

  • VID-20210103-WA0009.mp4
    21.5 MB
Hiyo habari nimeiona jana, nikajiapiza sitakuja kumpa tena mlemavu sumuni yangu unless nimejihakikishia kwamba hayuko kwenye mitandao ya namna hii.
Unforgetable
 
Kigoma wapo vizuri
 
Ndo Mana naona Dar omba omba walemavu wekuwa wengi sana, hadi kwenye madaraja ya kuvukia wamejaa
 
Hii inatakiwa imaanishe means za kujikwamua kiuchumi ni tatizo. Zikirekebishwa hizo cartel kama hii hautaweza iona, pia inamaanisha walemavu hawapati misaada na uwezeshwaji stahiki.

Ingekua wana pato la kila mwezi kutoka serikalini na gharama asilimia 0 kujiunga VETA na msaada wa asilimia 60 mtaji ni mlemavu yupi angeridhia kuzururishwa?
 
Hiyo habari nimeiona jana, nikajiapiza sitakuja kumpa tena mlemavu sumuni yangu unless nimejihakikishia kwamba hayuko kwenye mitandao ya namna hii.
Unforgetable
Yaani wewe umejua jana! Huu ni mradi upo kitambo sana Dar na kuna chimbo nyingi sana za wanatunzwa walemavu. Anayesukuma kitoroli anaula 10,000 kwa siku.
 
Afadhari ya hawa kuliko wale maacm waliokuwa wanawakata maalbino mikono ili washinde kura za maoni
 
Daaaa....nimesikia jamaaa akisema kuna mwana katafuta wheel chairs kama ishirini zen anakusanya 3,000/=kwa kila wheel chair moja kwa siku.
 
Hii biashara kwa hapa Dar imeshamiri sanaa. Watu wanashindana kwa kumiliki idadi kubwa ya walemavu.

Miaka km 4 iliyopita Kuna mwandishi aliandika makala gazeti la mwananchi aliichambua vizuri Sana hii biashara. Alienda deep akafika hadi guest moja inaitwa mauwa manzese huko. hapo ndio kwenye chimbo lao kwa pande hizo.
Akafanya mahojiano na walemavu pia namajirani wapande hizo. Ni ukatili na aibu tupu!
Ukweli ni kuwa walemavu hapa Dar wamefanywa kuwa km bodaboda au bajaji.
Watu wanashindana kwenda vijijini kuwakusanya walemavu kwa ahadi yakuja kuwasaidia mjini. Mwisho wasiku wanapangiwa hesabu na kuingizwa mitaani.
 
Back
Top Bottom