Mtoto wa Shule
JF-Expert Member
- Nov 16, 2014
- 11,641
- 8,575
"From April 14 onward, New York City has provided - and will continue to provide - the updated number of probable deaths in its daily reports." Source: (Worldometer; Last updated 20/04/2020). Hapo ni New York wanatoa taarifa kila baada ya masaa 24. Unasemaje!Kwanza sidhani unachokisema ni sahihi. Ni lini mara ya mwisho kupata updates za ugonjwa huu? Masaa 48 (siku 2) hayajafika?
Updates utoe kila baada ya muda gani - hutegemea aina ya janga. Lakini muda unaoshauriwa, isiwe zaidi ya masaa 2 bila update. Hii inaweza kuwa screen update (kama zile number unazoziona kwenye TV stations za CNN au BBC), lakini detailed update, inatarajiwa angalao isipungue mara 1 katika masaa 24.
Kinacholengwa zaidi ni kutotengeneza ombwe la habari, na watu wakaliziba. Kiuhalisia huwezi kutunza ombwe. Kama huna cha kuweka ili kuziba ombwe, kuna watu watalijaza.
Wewe hujasikia watu wakisema kuwa serikali inaficha taarifa za maambukizi na vifo vinavyotokana na Coronavirus? Unadhani habari kama hizo, zaidi zinachangiwa na nini?
Haikustahili watu kushuhudia marehemu aliyefariki kwa maradhi ya Covid 19, kabla ya serikali kutangaza vifo vilivyotokea. Watu wakijua kuna mtu amefariki kwa Coronavirus wakati serikali haijatangaza, hata kama Serikali haikuwa na nia ya kuficha chochote, watu wanapata uthibitisho wa yale yanayosemwa kuwa Serikali inaficha taarifa, kwa sababu kwa muda ule, tayari wana uthibitisho. Lakini kiuhalisia, huenda Serikali imepanga kutangaza taarifa ya vifo siku 2 au 3 mbele.
Government must not create an environment for gossiping.