Bams
JF-Expert Member
- Oct 19, 2010
- 16,489
- 40,999
Kwa mafunzo niliyoyapata toka kwa wakufunzi wa NATO, kuna vitu vya kuzingatia mara kunapokuwa na Crisis.
1) Automatically the most Senior Officer becomes the Crisis Management Manager. Maana yake, yule mwenye cheo kikubwa kuliko wote, moja kwa moja anakuwa Meneja wa Menejimenti ya Janga
2) Formation of Crisis Management Teams. Huwezi kuwa na timu moja kwenye Menejimenti ya Janga. Timu zinaweza kutofautiana kufuatana na aina ya janga, lakini msingi wake huwa haubadiliki:
a) Kamati ya Upashaji habari. Kukiwa na janga ni lazima kuwe na constant communication, kati ya kamati, kamati na idara za uokozi, kati ya kamati na jamii. Inategemea aina ya janga. Lakini mara nyingi inashauriwa, utoaji wa taarifa uwe kila baada ya nusu saa mpaka masaa 2. Usipofanya hivyo, unajenga mazingira ya watu kuzigeuza hisia kuwa habari kamili. Unataka kuliziba hilo pengo kwa utoaji wa habari za mara kwa mara. Ndiyo maana wenzetu wanakuwa na live updates.
b) Kamati ya uokozi. Kamati hii, umahiri wake upo katika kuwaokoa watu wengi kadiri inavyowezekana. Ufanisi wa kamati hii hutegemea nyenzo walizo nazo, taarifa wanazozipata toka idara za uchunguzi na intelijensia, ushirikiano wa haraka wanaoupata toka mamlaka za uamuzi. Lakini kwa vile yule mkubwa kabisa ndiye Meneji wa Menejimenti Timu, maamuzi hufanyika mara moja na kwa haraka.
b) Kamati ya uchunguzi na intelijensia. Kamati hii ndiyo yenye jukumu muhimu sana la kuzifanya kamati zote zitende kwa ufanisi. Wao hutoa taarifa sahihi za ukubwa wa janga, mwelekeo wa janga, uwezo wa kulikabili janga, uwezo uliopo wa kulishinda janga, mapungufu ya uwezo na mapendekezo ya njia za haraka za kulishinda janga. Kwa janga lililopo, kamati hii ndiyo ingekuwa pia na uwezo wa kutafuta taarifa za uwezekano wa wagonjwa ambao ama kwa kutojua au kwa makusudi wanaamua kutokwenda kuzitafuta huduma za afya kwa hofu ya kwenda kufungiwa bila kupewa huduma za kuwasaidia.
c) Kamati ya Rasilimali. Kamati hii kazi yake kubwa ni kutafuta rasilimali zinazohitajika. Wanapokea zaidi taarifa toka kwenye kamati ya uokozi na ya intelijensia. Kamati hii moja kwa moha inasimamiwa na Meneja.
d) Kamati ya Elimu na Uinuaji wa Morali. Hii kamati kazi yake ni kuwaeleimisha watu, kuwahamasisha na kujenga morali ya mapambano.
Kwetu hapa, kuhusiana na tatizo hili la Corona, inaonekana kuna tatizo kubwa katika menejimenti. Yawezekana hatuna wataalam wanaofahamu mbinu za kukabiliana na majanga, au wamepuuzwa.
Ni jambo la ajabu mno, kuona inapita hata siku nzima au 2 au hata 3, Waziri wa afya, ambaye nadhani ndiye kiongozi wa kamati ya Upashaji habari, hajasema lolote.
Kwa mtu anayejua wajibu wake, hawezi kufanya kosa kama hilo ambalo ni la wazi mno. Hata kuwaambia wananchi kuwa, leo hatuna maambukizi wala kifo, ni habari. Unakuwa umezuia ombwe ambalo watu watajaza habari zao.
Kwa nini tunashindwa hata kwenye basics tu. Ukiangalia TBC ni upuuzi mtupu. Ukiangalia TV stations za nchi nyingine, vipindi vingine vinaendelea, lakini chini au pembeni, unaona updates. Na ni nadra sana ikapita hata saa moja bila ya kusikia ujumbe unaohusiana na tatizo la Corona. TBC wanaona kuonesha taarabu au miziki ni muhimu zaidi kuliko kutoa elimu kwa watu, elimu ambayo ingeweza kusikia watu kuchukua tahadhari zaidi.
Labda tuseme kuwa sisi Tanzania hatupo kwenye mapambano dhidi ya Coronavirus. Huwezi kusema upo kwenye mapambano, halafu habari za hayo mapambano unaziweka kwenye mafaili.
Serikali yetu inaonekana kushindwa kumeneji mapambano haya au kwa makusudi, au kwa kutokujua au kwa ukaidi. Vyovyote iwavyo, kuna nafasi ya kujirekebisha.
Kwenye mapambano kama haya, Rais ndiye Meneja wa Menejimenti ya Crisis. Meneja wa Crisis anakaa hata wiki bila ya kuzungumza na watu wake ambao wanahitaji kusikia mipango, mbinu, mwelekeo na mwanga uliopo kuelekea ushindi. Hii inafikirisha, inaleta wasiwasi na kukatisha tamaa.