Opportunity Cost
JF-Expert Member
- Dec 10, 2020
- 9,035
- 6,907
Habari zenu wanajamvi.
Serikali ya awamu ya Tano ilileta na Kuanzisha utaratibu wa ujenzi wa miradi mbalimbali kwa kutumia Force Account badala ya Wakandarasi kwa madai kwamba Force Account inapunguza gharama za ujenzi.
Lakini kwa hali ya kawaida wanaofanya makisio ya gharama za ujenzi yaani maximum ceiling price za miradi ni staff wa serikali sasa hiyo gharama kubwa ambayo inasemekana kuletwa na wakandarasi ni ipi?
Force Account ina hasara nyingi kuliko faida ambayo ni ya kusadikika,
1.Miradi kujengwa Chini ya kiwango.
Miradi mingi ya Force Account kama majengo,miradi ya maji nk imejengwa chini ya Kiwango bila kufuata viwango vya kihandisi.
Hapo awali miradi ya ujenzi ya serikali ilikuwa inajengwa kwa kufuata kanuni za kihandisi hivyo kuwa na ubora unostahili kiasi kwamba hata majanga yakitokea kama upepo,mafuriko na matetemeko inaweza kuhimili na kuwa kimbilio kwa wananchi.Lakini kwa sasa miradi mingi iko chini ya Kiwango na ujenzi wake umefanywa kienyeji kwa vile wanatumia local fundi na mtu yeyote ambae,yaani kila layman ni mtaalamu kwa sasa.
Kwa kutumia Force Account huwezi kuta quality control inafanyika kwa kutumia tests mbalimbali za kudhibiti ubora,wakati ukitumia wakandarasi udhibiti wa ubora unafanyika.
Yaani unavyojenga jengo lako huko mtaani ndivyo inafanyika.eg Hostel za Magufuli na expansion joint na Uhuru Hospital na ishu ya Lift.
2.Kukosesha serikali kodi na mapato.
Miradi karibu yote ya Force Account hailipiwi VAT na tozo nyingine kama tozo za Madini Ujenzi kwa sababu inafanywa na Serikali.
Kama miradi hii ingefanywa na wakandarasi, serikali ingepata VAT na kukusanya kodi mbalimbali na regulation na udhibiti mwingine ungefanyika vizuri.
3.Kupungua kwa ajira hasa za Wataalamu.
Ujenzi wa force Account umepunguza na kupoteza fursa za ajira hasa za Wataalamu kama wahandisi,technicians nk.Kwa sasa wanatumia wahandisi au layman wa taasisi husika kwa kushirikiana na mafundi mchungo.Kama Wakandarasi wangetymika inamaana ni takwa la kimkataba kutumia wataalamu wa fani husika kwenye ujenzi na hivyo ingepanua wigo kwa wasio na ajira mtaani kupata fursa.
4.Kuongezeka kwa wizi wa fedha za umma na urasimu wa kufanya maamuzi.
Kwa sasa watu wanaoitwa local fundi hawezi pata Kazi hadi awe amewekwa na wenye mradi,matokeo yake Ili fundi upate Kazi lazima uhonge au ukubali kutumika kama kipitisha fedha za wenye mradi.
Wanaojiita wahandisi huwa wanasubiri fundi akosee afu wamwambie afumue nae anajiongeza kwa kumpa mgao ilimradi kila mtu anakula kwa nafasi yake.
Yote haya yanawezekana kwa sababu kuna lundo la wasimamizi mara kamati,DED,DC,Afisa ugavi,Injinia,Wakuu wa Idara,Watendaji wa Kata na Vijiji na swkretariat hapo bado Diwani na watu wa Chama sasa matokeo yake miradi mingi iko chini ya Kiwango na kinachofanyika ni kufunika kombe mwanaharamu apite.
Afadhari kutumia Wakandarasi maana kama ni rushwa ni wakati wa kutafuta Kazi baada ya hapo kila mtu afe na mzigo wake kwa hiyo liability inabebwa na contractor ni rahisi kumbana but huko kwenye Force Account pesa ikitumika vibaya na ujenzi chini ya Kiwango inakuwa imetoka hiyo kinachobaki ni danadana.
5.Ujenzi kutokamilika kwa wakati.
Force Account inategemea uwepo wa pesa bila pesa kila kitu kinasimama na hivyo ujenzi huwa haukamiliki kwa wakati matokeo yake kuchelewa kwa huduma.
Ukitumia wakandarasi mara nyingi kama wamechaguliwa vizuri wanaweza kutumia mtaji wao wakabaki wanaidai serikali hivyo kuwahi kukamilika kwa miradi na huduma.Miradi inayochelewa ni ile mikubwa ya mabilioni ambayo mkandarasi anaanza kwa mtaji wake afu ndio serikali inatakiwa kitimiza wajibu wake.
Lakini vimiradi vya chini ya milioni 500 wakandarasi wanafanya vizuri kabisa na wanakuwa wameikopesha serikali.Walio vizuri zaidi wanaweza hata kukamilisha miradi ya mabilioni pia.
6.Risks na Liabilities kubebwa na Umma.
Ukitumia Force Account ni kwamba miradi ikiwa mibovu au kutokamilika kwa wakati mzigo wote unaangalia kwa umma,hakuna wa kumuwajibisha na ku claim.
Ukitumia mkandarasi mradi ukiwa chini ya Kiwango anarudia kwa gharama zake na pia uangalizi kwa mda fulani unakuwa juu yake.Akichelewesha mradi anakatwa pesa na kupokwa mradi kwa hiyo hasara kwa serikali inapungua kuliko kutumia Force Account.
Juu ya hilo usimamizi ni juu ya mkandarasi wataalamu wa serikali ni kuhakikisha quality control ambayo haifanywi ukitumia Force Account
WITO NA USHAURI.
Serikali irudishe utaratibu wa kutumia Wakandarasi ila tuu iimarishe sheria za manunuzi Ili mkandarasi mwenye uwezo na mtaji ndio afanye Kazi na wale wengine wanaweza kuungana .
Ishu ya gharama kubwa ni propaganda za wapigaji kwa mfano kwa sasa kujenga chumba 1 cha darasa kilichokamilika kwa force Account ni Tsh.25 m,,sasa ukiwa na package ya vyumba 4 ni mil.100,sasa mkandarasi gani atashindwa kuchukua tender hii?
Kama kuna ulazima wa kutumia Force Account basi watumie kwenye miradi ya ujenzi ambayo haizidi 50 mil.maana faida za kutumia mkandarasi ni kubwa kuliko Force Account.
Mwisho Ingefaa serikali ipeleke Tarura wizara ya ujenzi kama ilivyo Tanesco na REA.Juu ya hilo TBA wawepo kwenye kila Halmashauri badala ya ile idara ya Ujenzi Ili wasimamie ujenzi wote unaofanyika kwa ngazi hiyo.