serikali

jiga2009

Member
Jul 3, 2008
8
0
kwa nini serikali yetu ya tz sio efficient na effective katika shughuli zake.Tatizo ni nini,mfano mipango mingi ya mendeleo huchelewa kutimizwa.
 
kwa nini serikali yetu ya tz sio efficient na effective katika shughuli zake.Tatizo ni nini,mfano mipango mingi ya mendeleo huchelewa kutimizwa.

Ndugu yangu Jiga, tatizo ni 'u ze comedy' wa serikali yetu!

-Siku hizi serikali yetu haina mawasiliano wala mshikamano kila mtu anatwanga lwake, leo huyu akisema hili kesho huyu anasema vile, hakiwezi eleweka kitu hapa! (No co-ordination at all!)

- tatizo lingine linalo ikabili serikali yetu ni dhambi zilizo tendeka kuhakikisha inaingia madarakani, tukianzia na kundi la mtandao, kukwapua pesa zetu BOT nk. --Serikali yetu inalazimika kuundwa kwa shinikizo la kishikaji na kulipa fadhila, haiangalii uwezo wa mtu!

----Pia serikali inalazimika kutumia muda na nguvu nyingi kuzima/kunyamazisha ama kupoteza kabisa ushahidi kwa kuunda tume juu ya tume, ili mafisadi wasiguswe kwa kile wanacho dai wameshikilia usalama wa nchi kumbe ni kujua asilimia mia moja kwamba serikali yenyewe ni sehemu ya mafisadi, kwahiyo wanabaki kuangaliana nani amfunge paka kengele, kupakana mafuta kwa mgogongo wa chupa, na mazingaombwe kila kukicha!

Kwa mtaji huu ndugu yangu usitegemee lolote!
 
Serikali ya kisanii na kiwizi tu hii. Ebu niambie mpango gani wa maendeleo umekuwapo tangu ichukue madaraka mbali na mpira?
 
na jamaa yuko ziarani tanga na atakaa huko kwa muda wa siku 9, nahuko nako ataahidi ya kuahidi halafu utekelezaji sifuri...lakini yote hayo ndo matokeo ya kuchagua sura badala ya wachapa kazi
 
na jamaa yuko ziarani tanga na atakaa huko kwa muda wa siku 9, nahuko nako ataahidi ya kuahidi halafu utekelezaji sifuri...lakini yote hayo ndo matokeo ya kuchagua sura badala ya wachapa kazi

Sioni shida kwa yeye kwenda Tanga maana wananchi wenzetu Tanga nao wana haki na raisi wao...asipotutembelea pia tutalalamika. Tumpeni nafasi afanye kazi badala ya kumlaumu kwa kila jambo
 
Sioni shida kwa yeye kwenda Tanga maana wananchi wenzetu Tanga nao wana haki na raisi wao...asipotutembelea pia tutalalamika. Tumpeni nafasi afanye kazi badala ya kumlaumu kwa kila jambo

Sawa kuwatembelea ni sawa lakini hakuna jipya la kufanya huko wewe mama!
Atawaacha na hali zile zile tu! Kwani muhimu ni rais kufika au rais kuhakikisha mambo yanakwenda? Kote alikokwisha tembelea na kutoa ahadi kibao tumesikia wabunge wa sisi emu wakilalama bungeni hakuna lolote limefanyika. Na huko Tanga wanaenda kuvuna hayo hayo?
 
Kwani akikaa Dar nako atafanya nini cha tofauti kama tayari inaonekana hafanyi kitu?
 
Kura yangu japo isilete mabadiliko makubwa lakini this time haiwezi kwenda kwa mtu asiye na mipango an ambaye atashindwa kuelezea kinaga ubaga na kuni-convince kuwa yeye sio mwenzao.
 
there is no enouhgt asprin in the world for a hedache like him...kwa hiyo hayo ndo matokeo ya kumchagua JK
 
Unapokuwa na kikundi cha watu wachache wameshikiria serikali unategemea nini? hakuna kitu cha msingi kitakachofanyika zaidi ya kuigiza na kila member wa serikali anasema kivyake kwenye issue ambazo ni sensitive kwa jamii, matokeo yake gharama za maisha zinazidi kuescarate kila siku huku wao wakitanua kwa gharama za wananchi masikini.
 
Kura yangu japo isilete mabadiliko makubwa lakini this time haiwezi kwenda kwa mtu asiye na mipango an ambaye atashindwa kuelezea kinaga ubaga na kuni-convince kuwa yeye sio mwenzao.

Gm, safi sana, hilo ndo swala la msingi, hata mie this time kura yangu haipati ngo' na hakika inabidi hata mke/mme mtoto, mjakazi na hata mgeni aliyeko malangoni mwangu/mwako hakikisha siku hiyo kura yake haipotezi kwa msanii huyu, na chama kinacho kumbatia mafisadi! kidogo kidogo tutashinda!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom