Crashwise
JF-Expert Member
- Oct 23, 2007
- 22,227
- 8,735
Katibu mkuu wa chama cha demokrasia na maendeleo CHADEMA Dk. Willbroad Slaa ambae pia ni kiongozi wa msafa a UKAWA kanda ya kaskazini amesema licha ya kuwepo kwa mvutano wa muundo wa serikali kwenye katiba mpya,katiba ya mwaka 1977 inayotumika sasa ina mfumo wa serikali tatu.
Dk. Slaa amesema hayo wilayani Bunda mkoa wa Mara kwenye mkutano wa Umoja wa katiba ya wananchi UKAWA ambapo amesema katiba ya Tanzania ya mwaka 1977 inayotumika hivi sasa inabainisha wazi mambo ya muungano na yasiyokuwa ya muungano na kwamba katiba hiyo imeweka wazi mfumo wa serikali ya Zanzibar hivyo wajumbe wanapaswa kupitisha rasimu ya katiba mpya ili kuiweka Tanganyika hadharani kama ilivyo Zanzibar.