Serikali zipo tatu kwenye katiba ya 1977

Crashwise

JF-Expert Member
Oct 23, 2007
22,227
8,735
Katibu mkuu wa chama cha demokrasia na maendeleo CHADEMA Dk. Willbroad Slaa ambae pia ni kiongozi wa msafa a UKAWA kanda ya kaskazini amesema licha ya kuwepo kwa mvutano wa muundo wa serikali kwenye katiba mpya,katiba ya mwaka 1977 inayotumika sasa ina mfumo wa serikali tatu.

Dk. Slaa amesema hayo wilayani Bunda mkoa wa Mara kwenye mkutano wa Umoja wa katiba ya wananchi UKAWA ambapo amesema katiba ya Tanzania ya mwaka 1977 inayotumika hivi sasa inabainisha wazi mambo ya muungano na yasiyokuwa ya muungano na kwamba katiba hiyo imeweka wazi mfumo wa serikali ya Zanzibar hivyo wajumbe wanapaswa kupitisha rasimu ya katiba mpya ili kuiweka Tanganyika hadharani kama ilivyo Zanzibar.
 
Kwa nini umetukana? Kama sio serikali tatu twambie tafsiri ya mikono miwili inayoonyeshwa na ccm kila mkono unaimanisha serikali zipi? Mikono yote miwili inalingana na kwa kila mkono wananyosha kidole kimoja. Ni serikali ya Zanzibar na serikali ya muungano? Mbona hazilingani? Kana serikali ambayo iko ila tunazuiwa kutaja jina lake. Kwa nini? Kuwa huru na ulazimike kuisema-Tanganyika. Ebu fikiri kwa bongo, Pinda ni waziri mkuu wa wapi? Zanzibar, of course no, kwa hiyo wapi? Mawaziri wasio wa shughuli za muungano wanaendesha serikali ipi? Toka kwenye box, fikiria tena. Serikali mbili ni usemaji bali ktk uhalisia ni tatu. Kuna sababu ccm wanaficha bila kutuambia na wanakuwa na kigugumizi kumwambia Warioba hivo kukosa sababu ya kukubali kuendeshwa kiunafiki unafiki. Tumeisha amua kurudi Tanganyika ni lazima.

Mimi nadhani CCM wanataka kuuvunja huu muungano. Katika serikali hizo mbili wanazozidai ni Tanzanyika na Zanzibar, sasa hiyo serikali ya Muungano hawaitaki kwasababu ya kukwepa gharama.
 
Kwa nini umetukana? Kama sio serikali tatu twambie tafsiri ya mikono miwili inayoonyeshwa na ccm kila mkono unaimanisha serikali zipi? Mikono yote miwili inalingana na kwa kila mkono wananyosha kidole kimoja. Ni serikali ya Zanzibar na serikali ya muungano? Mbona hazilingani? Kana serikali ambayo iko ila tunazuiwa kutaja jina lake. Kwa nini? Kuwa huru na ulazimike kuisema-Tanganyika. Ebu fikiri kwa bongo, Pinda ni waziri mkuu wa wapi? Zanzibar, of course no, kwa hiyo wapi? Mawaziri wasio wa shughuli za muungano wanaendesha serikali ipi? Toka kwenye box, fikiria tena. Serikali mbili ni usemaji bali ktk uhalisia ni tatu. Kuna sababu ccm wanaficha bila kutuambia na wanakuwa na kigugumizi kumwambia Warioba hivo kukosa sababu ya kukubali kuendeshwa kiunafiki unafiki. Tumeisha amua kurudi Tanganyika ni lazima.
Ndugu, Mmeamua lazima kurudi Tanganyika wewe na nani?.

Jenga hoja kwa nafsi yako na inafahamika kuwa ni kosa kimantiki kuwaweka wananchi wote kwenye box la fikra zako.
 
tusipo liweka hilo sawa leo kizazi kijacho kitatulaum na historia itatuhukumu,upo umuhimu wa kulijadili hilo kwa kina na kuliweka sawa katika misingi ya uhalisia wake,leo sisi tunamlaumu mwl Nyerere kwa kutoliweka hilo sawa mpaka ameingia kaburin,na sisi kizazi cha leo tumetembea katika historia tuliyoikuta aliyoiacha mwl kwamba muungano wetu ni matokeo ya kuungana kwa nchi mbili za tanganyika na zanzibar ,kizazi hiki cha leo kinapohoji hiyo tanganyika ipo wapi ,ipo haja waonyeshwe tanganyika yao,kwani hawawezi kuhoji zanzibar kwa sababu wanaiona,mwl alipaswa kulitabiri hilo kwamba kizazi kijacho kitakuja kudai hilo,leo sisi tungekuwa tunajadili mambo mengine ,lakini tukiliacha suala lipite hata ipite miaka ishirini,hamsin,mia na kuendelea kizazi kijacho nacho tunakiachia tatizo ambalo kimsingi kizazi cha leo ilibidi walitatue ,kwani na wao watasoma maandiko yanayoonyesha historia ya muungano wao.
 
Ndugu, Mmeamua lazima kurudi Tanganyika wewe na nani?.

Jenga hoja kwa nafsi yako na inafahamika kuwa ni kosa kimantiki kuwaweka wananchi wote kwenye box la fikra zako.

Sheria iliyotufikishia rasmu ya Warioba ndio ilikuwa elekezi kwa uharali wa mabilioni ya fedha zilizotumika. Wapinzani mapungufu waliyaona ccm wakapofuka ndiooo ikajaa wakatoka nje ya bunge. Matokeo yaja eti waliosema ni wachache! Ebo, CCM ni vi hiyo? Hiyo sheria iliagiza tume kuzingatia katiba zilizopo, zote 2 zina serikali 3 isipokuwa hazisemi Tanganyika, ni za wananchi. Kuzingatia tume za awali zilizochukua maoni ya wananchi nakupata serikali 3. Warioba, wananchi 61% walimwambia serikali 3. Sasa ni wanani ndani ya box? Ofisi ya rais, (rais alichaguliwa kwa 28% ya wtz) ilipitia rasmu mara 8 ikaona sawa. Wabunge wakaiona ya kwanza na kusahihisha. Hapo huoni suala la serikali mbili halikuwepo kwenye mchakato wa wengi bali limechomekwa na linatupeleka kubaya. Bado ninyi mnakaa kuimba wimbo msio ujua! Eh
 
Ndugu, Mmeamua lazima kurudi Tanganyika wewe na nani?.

Jenga hoja kwa nafsi yako na inafahamika kuwa ni kosa kimantiki kuwaweka wananchi wote kwenye box la fikra zako.

Halafu ndugu yangu wewe unajitiaga unajua kuchamba sana japo kuchamba kwingi hutoka na$&^/$@

Unamshauri mwenzako asiweke wananchi kwenye box la fikra zake while kiuhalisia wewe na wenzako mmetiwa kwenye box la zidumu fikra za mwenyekiti,mmefungwa minyororo ya akili hamfikirii nje ya box stil unakuja kunyoshea kidole wenzako wakati vidole 4 vyote vinakunyoshea wewe?

Jaji wariomba aliteuliwa na nani?

kwa nini rasimu ya kwanza mwenyekiti wa ccm taifa aliikubali wakati ilikuwa inaweka wazi uwepo wa serikali 3?

Rasimu ya pili ya katiba katiba kabla haijaenda bunge la katiba mwenyekiti alipewa kuisoma na yeye akabariki kuwa ikajadiliwe kama ilivyo bila marekebisho yoyote lkn ghafla akabadili mawazo,na je kama angeendelea kusupport serikali 3 wewe leo ungesupport pia?

Kuna mda humu ndani tunajaribu kukaa kimya na kusoma mawazo ya kila mchangiaji ila mawazo yako wewe yametekwa sana na fungu la kukosa mpaka hujitambui kuwa wewe ni Mtanga na nyika ama Mtanza na nia maana kila unaloletewa mezani na mwenyekiti wako wewe wabugia tu
 
Sheria iliyotufikishia rasmu ya Warioba ndio ilikuwa elekezi kwa uharali wa mabilioni ya fedha zilizotumika. Wapinzani mapungufu waliyaona ccm wakapofuka ndiooo ikajaa wakatoka nje ya bunge. Matokeo yaja eti waliosema ni wachache! Ebo, CCM ni vi hiyo? Hiyo sheria iliagiza tume kuzingatia katiba zilizopo, zote 2 zina serikali 3 isipokuwa hazisemi Tanganyika, ni za wananchi. Kuzingatia tume za awali zilizochukua maoni ya wananchi nakupata serikali 3. Warioba, wananchi 61% walimwambia serikali 3. Sasa ni wanani ndani ya box? Ofisi ya rais, (rais alichaguliwa kwa 28% ya wtz) ilipitia rasmu mara 8 ikaona sawa. Wabunge wakaiona ya kwanza na kusahihisha. Hapo huoni suala la serikali mbili halikuwepo kwenye mchakato wa wengi bali limechomekwa na linatupeleka kubaya. Bado ninyi mnakaa kuimba wimbo msio ujua! Eh

Mkuu unahangaika na watu wasiothamini mawazo ya wenzao,ccm inajua kila hatua inayotakiwa kufuatwa ili hii katiba ipatikane ila kwa makusudi kabisa kazi hyo wameamua kuipa kisogo na mwisho wa siku UKAWA wameliona hilo ndiyo maana wana support mawazo ya tume ya rais ya badaliko ya katiba iliyochini ya jaji warioba kada maarufu na mmoja wa waasisi wa chama tawala

Fikra ya Mtanzania wa leo haiwezi fanana na fikra ya Mtanzania wa jana,kwa sasa mtanzania wa kawaida kbs anaweza kuhoji na kupambanua mawazo yake bila kuelekezwa na mtu yoyote pamoja na kwamba sisiemu haitaki kbs jamii ijieleiwe,tuvishukuru vyama vya upinzani kwa kutoa elimu ya uraia bure kbs hususani chadema
 
Huu ndio ukweli ila kwa kuwa watu wa magamba wana akili za kushikiwa wanakubali kumezeshwa kila kitu na viongozi wao. akili zao hazitofautiani sana na akili za kuku wa kieneji!
 
Dkt Slaa naye anazeeka vibaya! Sasa kama Katiba ya JMT, 1977 inaeleza kuwa Tanzania ina Serikali 3, sasa Kikundi hiki haramu cha UKAWA wanazunguka nchi nzima kuwasumbua wananchi kwa nini?
Ni sawa na ule wimbo wa "Zanzibar ni Nchi kamili" na korasi yake inasema "tunataka nchi kamili ya Zanzibar!"
Haya Dr.W.Slaa, endeleeni kuchanganya makande, sukari, chumvi, nk kwa wakati mmoja!
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom