Serikali zingine nazo!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Serikali zingine nazo!!

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Pdidy, Dec 17, 2009.

 1. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #1
  Dec 17, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,585
  Likes Received: 5,771
  Trophy Points: 280
  Serikali Nayo!

  Serikali zingine hazina dini! SERIKALI NA TALAKA
  Mtazamo wa serikali kuhusiana na talaka umewekwa kutokana na kile raia wake wanataka (desires).
  Kama raia wake watataka kuwa na sheria zinawapa au kuruhusu talaka kirahisi, serikali huwapa.
  Tatizo kubwa ni kwamba binadamu mahali popote walipo kawaida huwa wanapenda uhuru wa kufanya wanavyotaka na hawataki kuishi katika standards za kibiblia au katika uadilifu ambao Mungu ameuweka.

  Mungu ameweka institution mbili duniani ambazo ni serikali na ndoa na hizi zinawafunga wanaoamini (waliokoka) na wasioamini).
  Wote wanahitaji kutii serikali kama vile kulipa kodi haijalishi umeokoka au la kwani bila kulipa kodi kuna adhabu yake tena ya uhakika.
  Hata kwenye ndoa uwe umeokoka au hujaokoka lazima utii standards za ndoa na kinyume chake ni penalty.

  Serikali nyingi (English speaking) zinaweza kutoa talaka hata kwa kuwepo kwa tofauti katika ya mke na mume (differences and disagreements) .
  Hata kama serikali inatoa talaka hii haina maana kwamba talaka zinaruhusiwa. Serikali haina common sense linapokuja suala la uadilifu (God’s morality standards). Hata kama serikali inauza pombe (liquor) hii haina maana pombe ni kitu sahihi.

  Serikali haiwezi kutatua tatizo lolote la uadilifu wa binadamu kufuata standards ambazo Mungu ameweka.
  Suala la talaka haliwezi kutatuliwa na binadamu yeyote aliye na hekima wala mahakama.

  Mke na mume wanapoenda mahakamani ili kupeana mahakama jaji huwaeleza ukweli kwamba wao kama mahakama hawahusiki na suala la kiroho, sheria za Mungu, au sakramenti au kiapo chochote cha dini kuhusiana na kuachana kwani hilo ninyi wahusika mtatatua wenyewe na kwamba sheria za serikali au mahakama hazina uwezo wa kuamua kile mliahidiana mbele za Mungu.

  Hii ina maana ninyi mnaopeana talaka mtahusika na Kipengele cha “Hadi kifo kitakapo tutenganisha” na kwamba mahakama haiwezi kutengenisha kile kilichounganishwa na Mungu.

  Jaji William J. Gainer wa New York Marekani ameeleza wazi kwamba pamoja na kwamba mahakama ina uwezo wa kutoa talaka bado suala la kiroho linabaki mikono mwa wahusika (Plaintiff na Defendant) kwani mahakama haiingilii sheria za Mungu.
  Maana yake unaenda mahakamani na kupeana talaka hata hivyo conditions zote za kuwa mke na mume bado zinabaki palepale untouched.
  Bado ninyi ni mke na mume na kila anayeoa au kuolewa anazini
   
 2. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #2
  Dec 17, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,585
  Likes Received: 5,771
  Trophy Points: 280
  Ndoa ni ......

  Hawa nao ni Adamu na Eva! NDOA, TALAKA NA KUOLEWA TENA
  UTANGULIZI
  Ndoa ilianzishwa (instituted) na Mungu. Mungu aliumba mke kwa ajili ya Adamu kwa kuwa Mungu aliona "Haikuwa vema" kwa Adamu kuwa peke yake.
  Mungu alimuumba mke (Eva) kuwa msaidizi (suitable helper) wa Adamu kutawala dunia, kulea familia na kumuabudu Mungu.
  (Mwanzo 2:18, 42)

  Ndoa ni mke mmoja na mume mmoja (monogamous).
  Mungu alimuumba Eva peke yake kwa ajili ya Adamu na si Eva na Jane, Ingawa Mungu alikuwa na uwezo wa kuumba wanawake wengi kadri anavyoweza ila alimuumba Eva peke yake kwa ajili ya Adamu.
  Agano la kale kulikuwa na polygamist na matokeo yake hakukuwa na amani.
  (Mwanzo 2:22)

  Ndoa ni mke na mume. Biblia haizungumzii kuumbwa kwa Adamu na James au Eva na Linda na kufanya ndoa bali Adamu na Eva.
  (Mwanzo 2:22, 1:28)

  ndoa inahusisha Mume kuondoka kwa wazazi ili kuanza familia yake kama mke na mume na pia kuna kuwa na taarifa kwa jamii (public recognition) kwamba fulani na fulani ni mke na mume hata kama formalities au tamaduni hutofautiana.

  Ndoa inawafunga mke na mume hadi kifo.
  Marko 10:9
  1Wakorintho 7:39
  Warumi 7:2-3

  Ndoa inahusisha wajibu wa kila mmoja katika mahusiano kwa mke kutii (submissive) na Mume kumpenda mke wa kujitoa sadaka (sacrificial love)
  Efeso 5:22-24, 25-28)


  Ndoa huhusisha mume kuwa kichwa cha nyumba au mke kama Kristo alivyo kichwa cha kanisa
  Efeso 5:23
  1Wakorintho 11:3

  Ndoa ni suala zito ni uamuzi wa pili kwa uzito duniani (kwanza ni wokovu na pili ni ndoa) hivyo si kuingia tu kwa kadri unavyijisikia kwani barabara unayoingia ni dead end hakuna kutoka hadi kifo.

  Dunia imejaa udanganyifu wa kila aina kuhusiana na suala la ndoa jambo la msingi ni kujua kweli na kweli itakuweka huru.

  Unapoingia kwenye ndoa unahitaji kuwa makini, mbele ya safari kujitetea eti nilikuwa bado nina akili ya kitoto, au nilidhani atabadilika au sikuwa na akili timamu au sikujua kama itakuwa hivi haitakusaidia kwani ukiingia ni hadi kifo kitakapowatenganisha hivyo kama hujaoa au kuolewa please be extra carefull siyo unabeba bora liende then kesho unasema "I made a terrible mistake" naweza kuachana naye! hakuna kitu kama hicho.

  Ubarikiwe!
   
Loading...