Serikali za Zanzibar na Oman kuchunguza sababu za kuporomoka kwa jengo la kitalii la Beit Al-Ajaib

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,877
6,326
Baada ya sehemu ya mbele ya jengo la kitalii la Beit Al-Ajaib kuporomoka jana, Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imesema itaunda Tume Maalum ya Uchunguzi kubaini kilichotokea, na kuishauri Serikali hatua stahiki za kuchukua

Aidha, Wizara ya Urithi na Utalii ya Oman ambayo inafadhili ukarabati wa jengo hilo nayo imesema itaunda Timu kujua sababu za sehemu ya kuporomoka kwake, na hatua zinazotakiwa kuchukuliwa haraka ili kulilinda

Wizara ya Utalii na Mambo ya Kale Zanzibar imesema itafanya jitihada zote kwa yenyewe binafsi au kwa msaada wa wahisani kuhakikisha jengo hilo linarudi lilivyokuwa awali

Kauli ya SMZ:

F9FD56C9-EBB7-4804-89F9-94F07657DE4C.jpeg
A585CF66-2DB7-4082-AB88-8A551B7A472B.jpeg


Kauli ya Serikali ya Oman:

The Ministry of Heritage and Tourism on Friday issued a statement following the partial collapse of Beit Al Ajaib building or popularly known as the House of Wonders in Zanzibar.

In a statement issued online by the Ministry said “The Ministry, with regret, followed up the partial collapse of the Beit Al-Ajaib in Zanzibar. As the Ministry, is the funding body for the comprehensive restoration, maintenance and rehabilitation project, it will form a team to find out the causes and determine the urgent and necessary measures to preserve and protect the building from any additional repercussions.”

Meanwhile, His Excellency Salim Al Mahrouqi, Minister of Heritage and Tourism has informed that the Royal holdings were transferred to a safer location.
 
Ama kweli serikali zetu zinapenda mno kuunda kamati za kuchunguza hiki na kile, yaani hadi watafika kuunda kamati ya uchunguzi kuchunguza kwa nini waliunda kamati ya kuchunguza kile na hiki.

Ni mwananchi gani wa zanzibar asiejuwa kuwa sababu kubwa ya kuporomoka sehemu ya jengo lile ni kutokufanyiwa ukarabati toka mwaka 1964 baada ya sultani kupinduliwa na jengo lile kufanywa mali ya serikali. Miaka yote hiyo jengo limesimama bila ya kufanyiwa ukarabati wowote zaidi ya kurushiwa chokaa kila baada ya miaka kadhaa.

Kusema kweli wananchi wa zanzibar pia wanangoja tu siku majumba ya michenzani, welezo na michenzani yatakapoanza kuporomoka, maana toka yalipojengwa na rais wa kwanza wa zanzibar mzee karume, hadi hii leo hayajafanyiwa ukarabati wowote ule, tunangoja tuone ni kamati ngapi zitaundwa.
 
Nyerere asingeiweka Zanzibar mfukoni hawa Waomani wangeendelea kutawala Zanzibar. Na inawezekana sasa Zanzibar ingekua kama Dubai.

Karume alishawaondosha waomani kabla ya zanzibar kuungana na tanganyika, usimpe nyerere credit za kiuongo. Baada ya karume kuuliwa na aboud jumbe kuwa rais wa zanzibar na nyerere kuwa rais wa muungano wa tanzania, ndio wakati zanzibar ulipoanzisha uhusiano tena wa zanzibar na nchi za kiarabu, huu ndio wakati ambapo aboud jumbe alifanya ziara chungu nzima nchi za kiarabu kuhakikisha uhusiano wa zanzibar na nchi za kiarabu unadumishwa. Nyerere hakuzuia au kupinga kuwepo kwa uhusiano huo hakuna nchi yeyote ya kiarabu ambayo ilijaribu kuitawala tena zanzibar.
 
Nyerere asingeiweka Zanzibar mfukoni hawa Waomani wangeendelea kutawala Zanzibar. Na inawezekana sasa Zanzibar ingekua kama Dubai.
Kiasili ama kijografia visiwa vya Zanzibar ni sehemu ya Tanzania bara

Visiwa vya Zanzibar vimetoka/vilimeguka kwenye bara Africa

Oman hana chake, hao warabu wakatafute maeneo mengine, mbona visiwa vipo vingi tu

Zanzibar ni ya Tanzania bara ova
 
Back
Top Bottom