Serikali za Majimbo-The way Forward!

mmakonde

JF-Expert Member
Dec 26, 2009
965
66
Baada ya kuona wateuzi wa mikoa ,hasa wanajeshi (anayekwenda Kagera) ,nimejiluliza hii status quo itakwisha lini?Huyu Kanali anasifa gani za kuongoza mkoa huo?Nikakumbuka haya mambo yalianza tangu enzi za Nyerere,kuteua mabalozi,DC,RC wanajeshi wastaafu .Hii ilikuwa wakati wa ukoministi,dunia ya sasa imesonga mbele.

Really hatuhitaji DC,RC,DAO,DED etc etc ,bali strong serikali za mitaa.hii itarahisisha maendeleo ya wananchi.
Katiba inayokuja lazima iangalie hiii issue maana ni wastage wa resources.

Mfano wangu say suppose tutaita jimbo la MWASHITA(Mwanza ,Shinyanga,Tabora).
Hili litakuwa na bunge lake,say kila wilaya itatoa mmoja.
Bunge hili litakuwa na makao makuu either katika mikoa hiyo.
Kila mkoa na wilaya utakuwa na Meya ambaye atachaguliwa na wananchi .Meya ndio atashikilia bajeti ya mkoa au wilaya.

Wabunge hawa wa kutoka mikoa hii watachagua nani kati yao kuunda serikali ya MWASHITA,na Wizara gani.Kumbuka hii nonsense ya
Wabunge wa kuteuliwa ndio itaishia hapa
JImbo la Mwashita litakusanya na wizara say ya Fedha,Madini,Kilimo ,Usafirishaji elimu ,afya ,sheria etc.Kutakuwa na formula
fulani ya kucontribute kwenye serikali kuu

Mfano huo utaona hakuna kilaza yoyote atakayekuwa parachuted toka DSM ,eti Kanali mstaafu kuja kongoza mkoa fulani.

Serikali kuu
Serikali kuu itakuwepo ,maana kila mkoa uteua mbunge mmoja au wawili kutokana na ukubwa mkoa na population kwenda kwenye bunge la Muungano au Tanganyika .Hawa wachache ndio wataunda serikali kuu.
Serikali kuu bado itakuwa na majukumu ya ulinzi ,polisi,magereza etc.

Can you imagine tungekuwa na jimbo say la Nyanda za Juu(Iringa,Mbeya,Rukwa etc) ,kama Rais Mkapa angethubutu eti kuinunua Kiwira kinyemela?
Au mikataba ya madini iliyosainiwa na mafisadi bila la bunge la mikoa hii kuruhusu?
 
Kwakweli watu kama nyinyi nddio mnatakiwa kuwa washauri wa baba Ridhi hii nchi ingekuwa mbali sana hata mafisadi wangepungua
 
Mfumo huu wa utawala niliwah kuutafakari kwa kina. Nilifurahishwa zaidi na namna CDM walivyouelezea kwenye ilani yao mwaka 2005-2010.

Mfumo huu unashabihiana na ule wa USA, isipokuwa hilo suala la kuwa na mawaziri kila jimbo ndio lina walakini.

Kama Taifa tukiridhia mfumo huu, tutafika mbali
 
Hakuna kitu kinachonikera kama kuletewa mkuu wa mkoa ambaye hajui A wala C ya mkoa wetu! Yeye ndiye anakuwa top wa watu wote mkoa wote' eti hata wabunge waliochaguliwa na wananchi! Mbaya zaidi wanateuliwa bila kuwa na vigezo maalumu! SERIKALI YA MAJIMBO NDIYO ILIYONIFANYA NIJIUNGE NA CHADEMA MWAKA 2005,KWA KUONA KUWA NI CHAMA KINACHOONA MBALI
 
Back
Top Bottom