SERIKALI YETU SIKIVU; Mbona Vijana wa Nchi hii wanahangaika sana?

Mandla Jr.

JF-Expert Member
Dec 15, 2013
3,100
1,195
Vijana ni Taifa la leo na la Kesho.
Hivi nani asiyelitambua hilo, vijana katika kila sekta wamekosa dira mpaka hata wanaomaliza Vyuo Vikuu hakuna Dira.

Wanasiasa wote huwa wanawatumia Vijana katika kufanikisha shughuli zao za kisiasa, mbona huwa hamgeuki nyuma kuwatazama hawa vijana??

Vijana hivi kuna FURSA gani za kukamata ili maisha yaendelee mbele? Kuna yale MABILIONI ya Kikwete hivi sijui walipewa akina nani na kwa vigezo gani??

Vijana ni nguzo ya Taifa, msijali hayo ni maneno ya kuwafariji chini kwa chini. "Mwaka 2015 unakuja kwa kasi Vijana tunawategemea sana msituangushe" hayo ni maneno ndani ya viongozi wenu wa vyama vyemu.

Siku hizi kuna vijana wa "RED BRIGADE" na "GREEN GUARD" hivi huwa mnafaidika na nini kwenye hivyo vikundi?? Alafu vijana wanaandama sana ndani ya vyama vyao, hivi nani anaewajali baada ya hapo?

Tanzania yenye neema tele na Vijana tele tele...
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom