Serikali yetu na ikulu wanaabudu ushirikina na uchawi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Serikali yetu na ikulu wanaabudu ushirikina na uchawi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by PhD, Sep 13, 2010.

 1. PhD

  PhD JF-Expert Member

  #1
  Sep 13, 2010
  Joined: Jul 15, 2009
  Messages: 3,819
  Likes Received: 818
  Trophy Points: 280
  nimekuwa nikifuatilia mara kwa mara kauli zinazotolewa na mnajimu Sheikh yahaya kuhusu Rais wetu na kudhihirisha wazi kuwa JK ni mshrikina wa kutupwa na hata siku moja serikali wala ikulu haijawahi kukanusha madai haya hivyo nalazimika kuhitimisha kwa kusema Taifa hili limepotea kimaadili kwa kuruhusu ushirikina kushika hatamu za utawal, watanzania wenye maadili na dini zao fanyeni mabadliko ya uongozi kwa kumchagua mtu anayemuogopa mungu.
   
 2. Mfamaji

  Mfamaji JF-Expert Member

  #2
  Sep 13, 2010
  Joined: Nov 6, 2007
  Messages: 6,526
  Likes Received: 556
  Trophy Points: 280
  Rais mshirikina, mgonjwa , mwongo, anayedanganywa hovyo , asiye na vision, msafiri,( Vasco Dagama wa TZ) mtembeza bakuli (omba omba) , asiyepima kauli zake kabla ya kuongea na Wazee wa Darisalaam etc etc

  ETI Bado anaomba kura! Nasema na aondokeeeeeeeeeeeeeeeee ...................
   
 3. Tuko

  Tuko JF Bronze Member

  #3
  Sep 13, 2010
  Joined: Jul 29, 2010
  Messages: 11,186
  Likes Received: 397
  Trophy Points: 180
  Lakini usisahu ushirikina tulikuwa nao tokea jadi. Kwa hiyo hatujapotea bali tunatakiwa tutoke huku hasa katika zama hizi za sayansi...
   
 4. A

  Andulile Member

  #4
  Sep 13, 2010
  Joined: Sep 9, 2010
  Messages: 23
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 5
  Hakika,nchi inahitaji mabadiliko ya haraka na Mungu atusaidie Watanzania wote kuelewa hilo. Nchi haiwezi kuendelea katika mfumo huu wa kishirikiana. Serikali haiamini uchawi na ushirikina lakini leo Mnajimu anajinafasi kwa umma kwamba anamlinda Jk kwa ulinzi usionekana. Hii hatari sana. Tunahitaji mabadiliko ili nchi hii ikabidhiwe kwa MUNGU na sio majini ya mnajimu. Uchumi wetu hauhitaji unajimu ili kufanikiwa unahitaji umakini na maono ya wapi Taifa linahitaji kwenda.
   
 5. Kachanchabuseta

  Kachanchabuseta JF-Expert Member

  #5
  Sep 13, 2010
  Joined: Mar 8, 2010
  Messages: 7,290
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  [​IMG]

  Ukijua maana ya hiyo pete ndo utajua
   
 6. Askofu

  Askofu JF-Expert Member

  #6
  Sep 13, 2010
  Joined: Feb 14, 2009
  Messages: 1,668
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 133
  :confused2:
   
 7. S

  Safre JF-Expert Member

  #7
  Sep 13, 2010
  Joined: Sep 2, 2010
  Messages: 240
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Hata kama uchawi ulikuwepo lakin si karne hii si wa kuuendekeza kaka upo
   
 8. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #8
  Sep 13, 2010
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  pleeeease
  naomba kujua maana pls
   
 9. E

  Endaku's JF-Expert Member

  #9
  Sep 13, 2010
  Joined: May 25, 2007
  Messages: 322
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  kaka tufunue macho maana pete hizo !
   
 10. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #10
  Sep 13, 2010
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,475
  Likes Received: 4,134
  Trophy Points: 280
  Huyo shehe Yahya naona anatumika sana na serikali maana mpaka sasa ikulu haijatoa msimamo wake kuhusiana na kauli zake ambazo zinatuchanganya hasa wale wasioamini mambo ya ushirikina.
   
 11. makoye2009

  makoye2009 JF-Expert Member

  #11
  Sep 13, 2010
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 2,646
  Likes Received: 500
  Trophy Points: 280
  PhD,

  Aksante kwa kuanzisha topic hii.

  • Kama kuna jambo linalo nikera kwa sasa hivi ni hii habari ya SHEIKH YAYHYA kujihusisha na Kampeni za Kikwete kwa kuwatishia watu na UCHAWI.
  • Haingii akilini hata kidogo Serikali ya CCM iendeshwe na Kigagula Sheikh Yahya kwa Remote Control.
  • Alianza kuwatisha watu kabla hata ya Mchakato wa kuwapata wagombea wa Urais na Ubunge kwa kusema atakayempinga Kikwete atakufa kifo cha ghafla.
  • Baadaye akaja na nyingine kuwa Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2010 hautafanyika badala yake utaahirishwa kutokana na mmoja wa Wagombea nafasi ya Urais kufa.
  • Pale Jangwani baada ya Kikwete kuanguka ghafla alipoulizwa sababu za Kikwete kuanguka Sheikh Yahya akasema kuwa ni DALILI ZA USHINDI wa kishindo!!!!Hapa ameshasahau kuwa alisema kuwa Uchaguzi hautakuwepo.
  • Juzi akaja na mpya tena kuwa KUANGUKA KWA KIKWETE ILIKUWA NI MAMBO YA KISHIRIKINA kwa hiyo yeye ameamua KUMLINDA KIKWETE KWA NGUVU NYINGINE ISIYOONEKANA!!!!!UCHAWI(KAMA NI HIRIZI,KAMA NI MIFUPA YA ALBINO) wanajua Sheikh na Kikwete
  Ukiangalia bulltes zote hapo juu utagundua kuwa Sheikh Yahya anatumiwa na IKULU au KIKWETE mwenyewe ili aingie madarakani kwa kutumia NGUVU ZA GIZA.

  Hapa ndipo penye matatizo makubwa! Kama KIKWETE anajua kuwa anaitawala nchi hii kwa nguvu za giza kuna haja gani ya kufanya uchaguzi????

  Hivi vitisho vinavyotolewa na Sheikh Yahya na wao CCM na Serikali yao wanataka kutuambia nini Watanzania????Kweli kwamba sasa tumefikia mahali Tanzania inaongonzwa na mpiga ramli anayesoma Nyota na kututabiria nani agombee au asigombee?Nani awe Rais na nani asiwe Rais.

  Kwa hili mimi nasema NO kwa herufi kubwa kabisa. Nataka CCM wanisikie na wanisome huko waliko. Nataka Kikwete kama M/Kiti wa CCM,Mshambaa Makamba kama Katibu Mkuu wa CCM na Kinana kama Meneja wa Kampeni za Kikwete wajitokeze na wautangazie umma wa Wadanaganyika kuwa KWA SASA TANZANIA INAONGOZWA NA NGUVU ZA GIZA KUPITIA REMOTE CONTROL NA KIGAGULA SHEIKH YAYHA
  Nahitimisha kwa kusema kwamba kwa SERIKALI YA CCM KUANZA KUTUINGIZA KWENYE MAMBO YA USHIRIKINA ADHABU YAO NI KUWANYIMA KURA NA KUWAPA vyama vingine vya SIASA ikiwemo CHADEMA,CUF,UDP,TLP,NCCR-Mageuzi n.k

  Dk.Slaa nilimsikia juzi akisema kuwa Mungu aepushe mbali na mambo ya USHIRIKINA katika nchi hii.
   
 12. D

  Dick JF-Expert Member

  #12
  Sep 13, 2010
  Joined: Feb 10, 2010
  Messages: 477
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mh! mi chichemi!
   
 13. p

  pierre JF-Expert Member

  #13
  Sep 13, 2010
  Joined: Sep 3, 2010
  Messages: 211
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Nakubaliana na mtoa hoja kuwa huyu kigagula ana ushirika na ikulu,Mheshimiwa atakuwa mteja wake na ndio maana hajakanusha yote ayasemayo sheikh yahya.Akikanusha tu itakula kwake,majini ya sheikh yahya yatakula naye sahani moja,hivyo hawezi kanusha
   
 14. payuka

  payuka JF-Expert Member

  #14
  Sep 13, 2010
  Joined: Jun 17, 2010
  Messages: 832
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  jamani hizi ni propaganda za serikali ili kuweza kuwapunguza nguvu waleta mabadiliko......huyu mchawi mzee hana lolote zaidi ya kuwapagawisha watu!!!!! kwanza naye afya yake imezorota sana siku za hivi karibuni!!!! Ni sawa na wakati wa vita mataifa yanapopigana utasikia redio mbao mara ooh vikosi vimeuteka mji fulani na wameua watu kadhaa......lakini ukifika sehemu hiyo si ajabu kukuta wao ndio wameelemewa ile mbaya ...
   
 15. Ndibalema

  Ndibalema JF-Expert Member

  #15
  Sep 13, 2010
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 10,916
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  hiyo aliyovaa kidole cha mkono wa kushoto ni ya ndoa.
  hiyo ya mkono mwin gine sijui ni ya nini!
  Na kwa mujibu wa dini ya kiislamu mwanaume huwa havai gold, sasa sijui itakuwa ni pete ya nini!!
   
 16. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #16
  Sep 13, 2010
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 145
  Hata wachungaji wanatumia kuponya watu ngoja Rev. Masa aje atuthibitishie.
   
 17. N

  Nyumbu- JF-Expert Member

  #17
  Sep 13, 2010
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 969
  Likes Received: 121
  Trophy Points: 60
  Hapo kwenye paji la uso naona kuna uvimbe....au ni brain tumor?
   
 18. n

  ngwendu JF-Expert Member

  #18
  Sep 13, 2010
  Joined: Jun 7, 2010
  Messages: 1,967
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Nashangaa bado watu wanaendelea kuleta hii thread ya kipuuzi humu. Nilisema tangia jana kuwa mzee yahya hajaanza kipindi cha kikwete. hivi mmesahau kipindi cha mkapa alisema kuwa mtu mwenye upara ndo atakaeshinda? Mbona watu hawakumwambia mkapa ajitokeza uau mang'ula au m/kiti wa kampeni wake? Au kwa sababu huyu si mwenzetu? Tuache unafiki.
   
Loading...