Serikali yetu, Mahakama na Bunge vipo mifukoni mwa wawekezaji | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Serikali yetu, Mahakama na Bunge vipo mifukoni mwa wawekezaji

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Isango, Aug 17, 2011.

 1. I

  Isango R I P

  #1
  Aug 17, 2011
  Joined: Jul 23, 2008
  Messages: 295
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Nimefanya uchunguzi kuhusu sekta ya uwekezaji nchini, nimegundua kuwa kwa kiwango kikubwa tunawalaumu wawekezaji lakini serikali yetu ndio inalea ubovu huu watu wanahamishwa ovyo katika maeneo kupisha wawekezaji, na wawekezaji wanawafanyia watanzania vitendo vya kikatili wakisaidiwa na serikali. Ifike mahali serikali iangalie matatizo haya na iijrekebishe.

  UKATILI WA SERIKALI YETU TUONE KWENYE STAR TV LEO SAA 4:30 USIKU DIRA YA MNYONGE. TUNAPELEKA CHAKULA SOMALIA LAKINI NDANI YA NCHI YETU WATU WANAKUFA NJAA. JE NI BUSARA? WANA JF ANGALIENI STAR TV LEO MUDA NILIOWATAJIA, TUPEANE MAONI.
   
 2. s

  smz JF-Expert Member

  #2
  Aug 17, 2011
  Joined: Dec 18, 2010
  Messages: 251
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Ndugu zangu,

  Chakula kilichoripotiwa kupelekwa Somalia kimeonekana kwenye maduka ya wajanja wachache Dar kinauzwa. Hii nchi ni sarakasi kwa kwenda mbele.
   
 3. M

  Mkurugenzi New Member

  #3
  Aug 17, 2011
  Joined: Oct 5, 2010
  Messages: 4
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hapo Bunge limeingiaje? ni Bora ukajua mipaka ya Utendaji wa Kila Mhimili! Wawekezaji wanawezaje kuliweka Bunge Mfukoni? ningependa nami nielewa wajameni!!!!

   
 4. I

  Isango R I P

  #4
  Aug 17, 2011
  Joined: Jul 23, 2008
  Messages: 295
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  MKURUGENZI, SOMA HII MAKALA UONE MIHIMILI HIYO INAVYOTEGEMEANA. KAMA SERIKALI IMEKOSEA, NA BUNGE NDIO MSIMAMIZI WA SERIKALI, KWANINI TUTETEE BUNGE. HEBU SOMA HAPA UNIPE MAONI YAKO!

  Serikali, Mahakama na Bunge ndani ya mfuko wa Mwekezaji, nini Hatima ya Tanzania?

  Nchi yetu imefikia pabaya. Hatuhitaji mwekezaji toka Ulaya kuelewa hili. Wenye pesa wameamua sasa kujichukulia madaraka kutesa wasio na pesa. Wenye pesa katika nchi yetu wanaabudiwa, serikali inaimba nyimbo za matajiri, Mahakama inaitikia kiitikio cha wimbo wa matajiri, wabunge ovyo wanapiga makofi na kushangilia wimbo huo ovyo usio na tija kwa watanzania. Serikali inaimba, Mahakama zinaitikia, bunge linapiga makofi na kushangilia Upuuzi huo, nini hatima ya Watanzania?

  Serikali yetu imewekwa katika mifuko ya wawekezaji. Serikali imekuwa tayari kufanya lolote hata kuua raia wake kusudi isigombane na wawekezaji. Ni vigumu sana kwa mwenye akili timamu kusadiki kuwa serikali yetu inawajali watanzania. Hatungetarajia serikali yetu iwe ya Malaika isiwe na kasoro, hata hivyo hatutarajii serikali ifanye ukatili huu wa kuua raia wake kwa kuendekeza uchimbaji wa dhahabu unaofanywa na makampuni ya kigeni nchini.

  Serikali yetu sasa haiwezi hata kukemea wawekezaji. Wanafanya kila wanachoona kinafaa. Tumelalamika sana kuhusu sumu za mto Tigite kule Nyamongo Mkoani Mara, lakini hakuna hatua zilizochukuliwa, wananchi wale wameendelea kuteseka, kuugua, kufa, wao pamoja na mifugo yao. Hii ni athari ya mgodi na faida pekee wanayopata watanzania kutokana na wawekezaji. Mpaka sasa serikali haijaweza kuwapa wananchi wale maji mbadala na mifugo yao, wanaendelea kutumia sumu.

  Serikali yetu inafanya ukatili kuungana na wawekezaji kuua raia wake, kuwanyang’anya ardhi bila kuwapa fidia stahiki. Wanakijiji waliohamishwa kutoka eneo linaloitwa Mine mpya katika kata ya Mtakuja na kuhamishiwa katika kata Kalangalala Wilaya ya Geita hawa walihamishwa usiku toka katika makazi yao na polisi, huku wakiwa hawajalipwa. Operesheni ya kikatili ilisimamiwa na Mkuu wa wilaya Geita, na vipigo vya polisi, wananchi walitolewa katika nyumba zao walipelekwa katika jengo la iliyokuwa Mahakama ya Mwanzo, halina madirisha, halina milango, ni sakafu tupu, wakarundikwa wote, Baba, Mama, Mtoto, Mke, Mume, hadi wakwe zao, bila kujali jinsia zao, serikali ikawarundika usiku. Asubuhi yake Makazi ya wananchi wale na Mashamba yao walisambazwa na Buldoza la Kampuni ya Geita Gold Mining, licha ya kuwepo Amri mbili za Mahakama zilizokuwa zimesema wananchi hao wasihamishwe kwani suala hilo lipo Mahakamani.

  Amri ya Mahakama ya Rufaa kuisimamisha kampuni ya Geita Gold Mining kutowahamisha wananchi hao ilitolewa katika Mahakama ya Rufaa, na Jaji E. N. Munuo, tarehe 9 Machi 2006

  Amri nyingine ni ile ya makama Kuu, kitengo cha ardhi ilitolewa Dar es Salaam na Jaji P. A. Rugazia, tarehe 3 Agosti 2007. amri zote mbili zilikiukwa, wananchi wakatimuliwa kama mbwa, mahali waliporundikwa hawana mashamba, hawana chakula, walikaa ndani ya jengo hilo mpaka pale Taasisi za dini zikiwemo Makanisa zilipoamua kupeleka Maturubai na Mahema kusaidia. Naomba madhebu ya dini fikeni Geita mjionee unyanyasaji huu na muwasaidie hawa watu. Sasa maturubai na mahema yamechanika, yamechakaa, msimu wa mvua unakaribia, wananchi hao hawajui mustakabali wa maisha yao. Serikali iliwatupa, haitaki kuwaona, na sasa waliofariki katika lile eneo ni watanzania tisa.

  Serikali ya Tanzania inayojidai kuwa ni serikali njema, inayowaweka wakimbizi wa nchi zingine, imewaacha watanzania wake hawana nyumba, hawana chakula, imevunja nyumba zao, imefukia mashamba yao,hawa wameachwa wafe taratibu ili hata kesi waliyofungua mahakamani iishe kistaarabu. Hii ndio faida pekee waliyopata wakaazi wa kijiji cha katoma, kijiji kilichobadilishwa jina na wawekezaji na kikaitwa ‘mine mpya’.

  Faida nyingine wanayopata watanzania kutokana na uwekezaji katika sekta ya madini ni kunywa maji yenye sumu. Ukiachilia mbali madhara ya sumu yaliyowapata wana tarime, Geita hawakukwepwa na hili. Barua ya mkurugenzi wa Wilaya ya Geita ya tarehe 18/6/2004, yenye kumbukumbu Namba GDC/W.10/1/7 inathibitisha kwa kauli moja ikisema kuwa “tulipeleka sampuli ya maji ya Bwawa la Nyamalembo kwenye maabara ya Uchunguzi wa Ubora wa Maji Ubungo Dar es slaam, majibu yaliyopatikana ni kuwa maji ya bwawa hilo hayafai kwa matumizi ya binadamu na wanyama pia. Utafiti umeonyesha kuwa Bwawa la Nyamalembo limechafuliwa na kiwango kikubwa cha Zebaki kutokana na shughuli za uchimbaji wa dhahabu na usafishaji zinazofanywa na vijito vinavyopeleka maji katika bwawa hilo. Barua hiyo ilifafanua kuwa madhara ya kutumia maji hayo ni kama kuharibu mfumo wa kujikinga na magonjwa, kubadilisha mfumo wa urithi wa kizazi (alter genetic and enzemes systemes), kuharibu mfumo wa fahamu, na kuharibu hisia za kugusa, kuonja, kuona na maadhara mengine. Hizi ndio faida za mgodi kwa wananchi hawa?. Rais Jakaya Kikwete amewazingua kila mara kuwapa maji safi lakini hakuna utekelezaji, wananchi hayo na mifugo yao wanaendelea kunywa Zebaki, hawana maji mbadala wao na mifugo yao hadi sasa.

  Wabunge wanapokuwa bungeni wanajadili mambo ya posho, wanajadili mishahara, wanajadili wawekezaji, je wananchi hawa wa Katoma walioachwa katika jengo la Mahakama, wakadanganywa kuwa kijiji chao kipya kitaitwa Sofia town, ambao hawana mavazi, hawana chakula, hawana makazi, hawana mashamba, majaliwa yao ni nini? Serikali ndio imewafukuza, amri za zuio zilizotolewa na Mahakama zimekiukwa bahati mbaya serikali ndio iliyosaidia kuvunja amri za Mahakama ili iwape eneo wawekezaji, Wabunge wao hawawakumbuki, rais, mawaziri, na wabunge hawawajui kama wapo katika nchi yao. Nini hatima ya watanzania hawa? Hivi wanaharakati jamani, harakati zenu ni Dar es salaam, Arusha na Mwanza tu?. Watanzania wameshauzwa Geita, wanaishi ugenini kwenye machozi.

  Wiki iliyopita tumeona serikali ikiamrishwa na wauzaji wa mafuta. Bado hali ni tete, na bado serikali inakanusha kwa nguvu kuwa serikali sio legelege au ya kishikaji. Hapa nimewaonyesha jinsi amri za zuio za mahakama mbili muhimu katika nchi yetu zilivyokiukwa, na wenye migodi hawajachukuliwa hatua, na wiki hii mmeshuhudia ninyi watanzania jinsi kampuni nyingine ya kuchimba madini yenye ‘madhambi meusina dhuluma nyingi kw watanzankia’ ilivyokodisha ndege kupandisha wabunge ili wakaikague. Wema gani wa kampuni hii ya kutoa ofa ya tiketi ya ndege? Na wabunge wetu wasiojiongeza waliohasiwa akili, wasiojali watanzania katika mateso tunayotendewa na wawekezaji hawa wa madini bila aibu waliamua kuhasi akili zao wakapamba ndege eti kufanya uchunguzi kwa siku moja. Migodi hiyo yote ya geita na Nyamongo nilivyoitembelea haiwezekani mtu kufanya ziara kwa siku moja ukaweza. Hawa walienda kupokea posho, na/au kutalii. Mateso tunayofanyiwa mpaka kuhurumiwa na watu wa nje ya nchi sisi tunajidai hatuyaoni. Serikali yetu inayaona kuwa ni propaganda za kijinga. Walipouawa wale vijana wa Tarime na wawekezaji wa Barrick, wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Toronto nchini Canada ilipotoka ile kampuni, waliandamana, wakagoma hata kulipiwa ada na kampuni hiyo wakisema ni pesa chafu, zinazotokana na unyanyasaji na mateso ya watanzani. Sisi ambao ndio tumetendewa hayo tunajiona tuna nafuu. Wanafunzi wa Chuo cha Toronto wanaona uchungu wa watanzania waliouwa kwa sababu ya madini yao, ila sisi ambao ndugu zetu wameuwa kwa sababu ya kutaka kuhoji wizi wa madini yao sis indo tunacheka, na tunatumia nguvu nyingi kuwakamata wanaharakati wanaotaka tuhoji juu ya yaliyotokea. Haitoshi kuwakamata tu na mashtaka tunawafungulia. Wenye Barrick wanaandama, Barrick ni ya Canada, wanaona madhambi ya kampuni yao, sisi tunaikumbatia, dhambi zao zinaonekana takatifu katika nchi yetu. Dhuluma zao zinaonekana ni zawadi kwetu, wanatuibia ng’ombe mzima kisha wanatununulia supu na sisi tunaanza kuhubiri kuwa jamaa hawa ni wema. Wawekezaji wana kiburi, wanaruhusu mbwa kuuma vijana wetu, wanalazimisha dada zetu kulala na mbwa wao, walinzi wao wanabaka dada zetu, wanadhalilisha kila aina ya udhalilishaji hawachukuliwi hatua zozote. Wana pesa. Lakini wao bado wanakula sahani moja na serikali, hata maamuzi ya mahakama hayawezi kufurukuta. Kampuni za kuchimba madini nchini kwetu zipo juu ya serikali, zipo juu ya mahakama, tena zipo juu ya Bunge. Wabunge wachache wanaoona huruma na unyama huu wanazidiwa nguvu na wale wengi kwa makofi kwa kuwa walio wengi wamefadhiliwa na makampuni hayo wao na chama chao kupata pesa za kampeni. Pesa za Mwekezaji sasa inanunua mpaka viwanja vya Mahakama au serikali inakubali kubomoa sehemu ya Mahakama eti kwa lengo la kupanua biashara za wawekezaji. Tunapoelekea siko. Ukombozi wa Tanzania utapatikana tu.
   
 5. mwaJ

  mwaJ Tanzanite Member

  #5
  Aug 17, 2011
  Joined: Sep 27, 2007
  Messages: 4,076
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Kwa kweli inatia hasira sana! Imekuwa wawekezaji wawekezaji! Huku wananchi wakiachwa wanateseka bila mtetezi!
   
 6. T

  Tikerra JF-Expert Member

  #6
  Aug 17, 2011
  Joined: Sep 3, 2008
  Messages: 1,704
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Wawekezaji ndio mabosi wa serikali, kama hujui hali ndivyo ilivyo.Kama mambo ndio hivyo ,unategemea nini.Wenyewe wanasema,give me the economy of a country,and I don't care who rules it.
   
 7. M

  Mapujds JF-Expert Member

  #7
  Aug 17, 2011
  Joined: May 12, 2011
  Messages: 1,291
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  <br />
  <br />
  nasikitika nitakuwa naangalia mpira wa barca na madrid,je kitarudiwa lini na sangapi?
   
Loading...