Serikali yetu inatakiwa kupambana na wimbi la vijana wengi kukosa ajira

Elisha Emma

New Member
Jul 27, 2021
3
3
Kwa sasa Dunia nzima inahangaika juu ya vijana wengi kukosa ajira. Juzi nchi jirani iliamua kuwagawia vijana wasiokuwa na ajira chakula, lakini walisahau kuwa shida yao si chakula bali, ni nini kitawapatia chakula endelevu? Na vijana wale walikataa kile chakula na huku wakiendelea kuhitaji ajira. Mimi kama mtanzania nimefikiria kwa mapana sana kuhusu hili swala la ajira na nimeona vitu vinavyotakiwa vifanywe na serikali yetu.

Kubadilisha mfumo kutoka kuhesabu miaka ya watu hadi kuhesabu miaka ya kazi. Kanuni na sheria zetu zinahitaji mtu afanye kazi hadi atakapofika muda wa kustaafu ambao ni miaka 60 kama hana shida yeyote. Mimi ningependa serikali isihesabu miaka ya kustaafu kwa wafanyakazi, bali iangalie miaka ya mtu alivyofanya kazi.

Mfano mtu mmoja akiajiriwa na miaka 25 anatakiwa afanyekazi miaka 35 ndo astaafu, wakati hapo kwa miaka 35 kuna watu wanatengenezwa kufanya kazi hiyohiyo. Hivyo serikali inatakiwa iweke mfumo wa kufanya mzunguko katika kuajiriwa, mfano serikali iangalie kila mtu atafanya kazi miaka 20 tu alafu astaafu aje mwingine, hiyo itasaidia kwa kila mwaka kutakuwa na watu zaidi ya 500 watakaokuwa wanastaafu katika sekta zote.

Na mfumo huu utawafanya watu wengi wapate ajira kila mwaka kwa sababu watu wanastaafu na pia zinatokea kazi nyingine mpya. Mimi ni mwanafunzi wa chuo, kuna madaktari wapo tangia 1995 wanafundisha, huyu daktari ametoa watu waliosomea kitu chake hicho kwa miaka 26 mpaka sasa, je hao watu wote wapo wapi? Ukiwa ni huu mfumo unaruhusu yeye kustaafu, na meingine anaingia hapo.

Ajira isiwe ni mategemeo ya watu bali iwe ni sehemu ya kuitumikia nchi yetu tu.

Asante kwa kusoma, Mungu akubariki.
 
Nani akupambaniae Wewe kijana.

Amka dunia haina huruma, pambana na hali yako, ukipata mtu kuonea onea, ukipata mwanya pita hapo hapo.
 
Serikali imesema mkajiajiri! Wapi? Mtajua wenyewe!! Yenyewe imetingwa kuanzisha kamati za kujadili suala la tozo, ila siyo hilo tatizo la ajira kwa nyinyi vijana.
 
Back
Top Bottom