Serikali yetu imekosa mifumo Bora na thabiti, katika utekelezaji wa majukumu yake

Dec 26, 2021
33
23
Habari zenu.

Serikali ya Tanzania, ikitengeneza mfumo Bora wa utekelezaji wa shughuli, uwajibikaji na majukumu yake ya kiserikali basi Tanzania itaendelea.

Nje ya Katiba mpya, watanzania wanahitaji huduma za kijamii ziwafuate na sio kama ilivyo Sasa, watanzania wanazifuata na kukimbilia huduma za kijamii.

Leo ukitaka kufuatilia cheti chako cha kuzaliwa inabidi uende halmashauri, Wakati hili lingekuwa linaweza kutatulika ngazi ya kata.

Ngazi ya kata kwa sasa haiwezi kutekeleza, maana Haina watumishi au huenda Sheria hairusuhu.

Ndio maana ya kusema, serikali yetu Haina mifumo Bora wa kutekeleza majukumu yake.

Serikali imejikita sana ngazi ya Wilaya na Halmashauri, hivyo basi watanzania kulazimika kufuzifuata huduma hizi ngazi ya juu katika uongozi.

Tanzania usishangae kesi imefikia ngazi ya halmashauri, mtendaji wa kata hajui. Ni kwa sababu ofisi ngazi ya kata haina watumishi, hivyo mtanzania hulazimika kukimbilia huduma ngazi ya juu.

Kwa wataalamu wa Sheria za katiba ya Tanzania, huenda wanaweza kutuambia labda kama Kuna sheria inazuia ofisi za kata kukosa watumishi, Tena ambao wangeweza kuwafikia watanzania Kwa urahisi kabisa.

Tunapoteza muda mwingi sana, kwa taratibu mbovu na duni. Kufuatilia swala ambalo lipo kwenye mfumo wa kiserikali, inahitaji utenge muda na fedha nyingi. Nje ya hapo uwe na MTU WA kukushika mkono.

Unahitaji muda na fedha Gani kufuatilia hati yako ya kiwanja chako?

Huo muda unaopotezwa kwenye hati, ni dhahiri kuwa serikali yetu imekosa utekelezaji duni wa majukumu yake na huenda Sheria zake duni.

Dunia ya Sasa ukikosa Sheria Bora za kuokoa muda, Sheria Bora za haki na usalama wa Mali, umekosa wawekezaji.

Serikali zetu za kiafrika hazijatengeneza mifumo Bora wa kuwaokolea wananchi wake muda na gharama.

Kwenye ukusanyaji Kodi,
Leo afisa wa TRA, yupo ngazi ya wilaya na halmashauri, vipi wangekuwepo Hadi ngazi ya kata?

Kungekuwa na wimbi kubwa la wakwepa Kodi au wasiolipa Kodi?

Watanzania wengi wanamiliki ardhi, wanaolipa Kodi wamefikia robo tatu yake?

Mfumo uliopo ni kwamba Mimi mlipa Kodi nimfuate TRA nikalipe Kodi, Na nisipoenda TRA Hana mfumo Bora wa ukusanyaji Kodi. Kunifuatilia ni ngumu.

Kodi ya Ardhi, wangapi hawalipi? Ni kwa sababu tu serikali ngazi ya kata Haina watumishi was kutosha.

Taasisi za kutoa Huduma za kijamii.
RITA,NIDA, TRA, TANESCO, n.k hizi zimekomea ngazi ya wilaya na mkoa, huku ngazi ya kata hamna hivyo basi inakubidi utenge muda na fedha uzifuate zilipo.

Kwa uchumi wa mtanzania, ni watanzania wangapi wenye iwezo huu?

Tumekuwa taifa la kuikumbusha serikali yeti majukumu yake, ni kheri msimamizi akiwa imara maaana ataweza wakumbusha na kuwajibisha anao wasimamia.

Huduma kama hizi au utekelezaji wa majukimu kama haya, ungefikia mpaka ngazi ya kata ya nchi hi, tungefikia wapi?

Na ni suala ambalo linawezekana kutekelezwa.

Kuna mambo ambayo si kipaumbele, serikali ilibidi iachane nayo ili ipate kupunguza bajeti ya matumizi yake ya fedha. Na badala yake fedha hizo zingetumika kuwekeza kwenye namna ya kuokoa muda na gharama anazo- kumbana nazo mtanzania kwenye maisha yake ya Kila siku.

Mfano. Serikali yetu imekimbilia ufahari wakati bado ni maskini licha ya utajiri wetu wa asilia yeti.

Hatuna sababu ya kuruhusu kutumia magari ya millioni mia au mia mbili na zaidi.
Na magari haya yapo mengi nchini, kisingizio barabara mbovu. Suluhisho hapo ni kutengeneza Barabara au kununua gari?

Tumeshindwa kutatua mizizi ya matatizo yetu mara zote, serikali imejikuta ikiangukia kwenye matumizi mabovu ya pesa.

Serikali yetu ikitaka taifa letu liendelee inabidi ikubali kubadilika haswa kuanzia sheria za nchi na uundaji wa mifumo Bora kusimamia na utekelezaji wa majukumu yake.

Kuvutia uwekezaji wa ndani na nje, inabidi serikali ihakikishe Ina mifumo thabiti na Bora, ya kumuokolea muda na gharama.

Mwekezaji, akitaka kuwekeza aweze kufuatilia taratibu za kuweza kuwekeza kwa muda mfupi na gharama nafuu.

Labda anakuja mwekezaji anaetaka kuwekeza kwenye sekta ya madini, mpaka anakuja kukamilisha taratibu zake anakuwa ametumia gharama kubwa mno na amepoteza muda mwingi.
Lakini serikali ikihakikisha imetengeneza mfumo ambao itamuokokelea muda mwekezaji huyu na kuhakikisha gharama zinakuwa nafuu, taifa litapokea wawekezaji wengi.

Ubovu wa mifumo yetu serikalini ndio mbolea la wimbi kubwa la rushwa nchini.

Wilson M. M,
T. Civil Engineer,
Smart Ujenzi
Tuna-Husika,
1. Ramani za Nyumba na Majengo mbali mbali.
2. Ujenzi na Kuandaa tathmini za ujenzi.
Mawasiliano:
Simu na Whatsapp.
0762-704-031/0654-704-031.
 
Back
Top Bottom