Serikali yenye akili lazima iache kabisa kuingilia kusambaza bidhaa hasa kwenye miradi hii ya COVID-19. Inaweka mzigo na mwanya wa rushwa

William Mshumbusi

JF-Expert Member
Mar 27, 2012
1,657
2,252
Kuna baadhi ya halmashauri zilijaribu kununua na kusambaza cement kwenye hii miradi kilichotokea NI kuwa bidhaa hizo waliwauzia taasisi kwa Bei kubwa kuliko Bei ya soko.

Sioni mantiki ya Serikali kuingilia biashara hizo kwa visingizio vyovyote vile huko ni kuturudisha kwenye ujima na ujamaa wa kishamba wa Sukita na Rtc. Hiyo NI kwasababu.

1. Kunaua na kudunisha Sekta binafsi ambazo NI mdau mkubwa wa kulipa Kodi na faida wanazopata hujenga nchi.

2. Uweka urasimu na kutoa mwanya wa watendaji kukwepa ulipaji Kodi hivyo kupunguza kipato tra.

3. Hakuna mtendaji wa Serikali atakayekuwa na msukumo wa ndani na uzoefu wa biashara husika hivyo itapelekea Kazi kujivuta.

3. Wafanya biashara wataongeza Bei za usafiri ili kufidia dili la biashara walionyanganywa na Serikali.

4. Serikali inatakiwa ihakikishe bidhaa husika haziishi sokoni ata wa watu wa kawaida isiangalie miradi yake tu na wao kwenda viwandani sio suluhisho. Hali hiyo itasababisha ukosefu na ongezeko la Bei mtaani. Kwani Serikali itatumia mabavu kuchukua Hoda zake mwanzo na kuwavuka watu walioweka Oda mwanzo.

Mimi nadhani Sekta binafsi zinatakiwa kuimarishiwa mitaji na kupewa masoko ili maendeleo ya miundo mbinu iguse Sekta binafsi ili kuuchochea biashara mtaani.
 
Back
Top Bottom