tutafikatu
JF-Expert Member
- Dec 17, 2011
- 3,232
- 4,448
Kuna waraka umetolewa na Wizara ya Afya, ukitoa taarifa kwamba kuanzia tarehe 01 Juni 2022 hatua kwa hatua kutasitishwa matumizi ya form 2c. Form 2c ni fomu inayotumika na hospitali zinazohudumia wagonjwa wa NHIF kujaza dawa zisizokuwepo hospitali, ili mgonjwa au ndugu wa mgonjwa akachukue dawa husika kwenye maduka binafsi (mengine yako nje ya hospitali ila yanamilikiwa na hospitali husika au serikali) nje ya hospitali.
Maduka haya ya dawa, huingia mikataba ya kisheria na NHIF ya kutoa huduma kwa wateja wao. Ingawa waraka huu unasitisha utoaji wa form 2c kwa vituo vyote vya afya hata binafsi, ukweli malengo makuu ni hospitali za Serikali, lakini kwa sababu form 2c zinatumika na hospitali zote zilizoingia makubaliano na NHIF kutoa huduma kwa wanachama wake, hivyo imebidi tu nazo wazihusishe.
Huu ni uamuzi wenye faida na hasara. Binafsi kama mfamasia naamini kuna hasara zaidi. Ukisoma waraka huu unaweza gundua mambo kadhaa hasi toka Serikali kwa watumishi wake wa afya na maduka ya dawa.
Mtazamo wa Serikali
Nini kitatokea
Maoni
Pia soma > Serikali yasitisha matumizi ya Fomu ya 2C inayotumika kuchukua dawa maduka ya nje
Maduka haya ya dawa, huingia mikataba ya kisheria na NHIF ya kutoa huduma kwa wateja wao. Ingawa waraka huu unasitisha utoaji wa form 2c kwa vituo vyote vya afya hata binafsi, ukweli malengo makuu ni hospitali za Serikali, lakini kwa sababu form 2c zinatumika na hospitali zote zilizoingia makubaliano na NHIF kutoa huduma kwa wanachama wake, hivyo imebidi tu nazo wazihusishe.
Huu ni uamuzi wenye faida na hasara. Binafsi kama mfamasia naamini kuna hasara zaidi. Ukisoma waraka huu unaweza gundua mambo kadhaa hasi toka Serikali kwa watumishi wake wa afya na maduka ya dawa.
Mtazamo wa Serikali
- Kwamba watumishi wa hospitali wanafanya makusudi kuhakikisha hospitali zao zinakosa dawa zote ili kutoa mwanya kwa maduka ya dawa yaliyopo nje ya hospitali kufanya biashara
- Kwamba maduka ya dawa binafsi ni chanzo cha dawa kukosekana ndani ya hospitali.
- Kwamba maduka ya dawa yanapata faida kubwa ambayo ilipaswa iingie ndani ya mifuko ya hospitali na kuzisaidia hospitali kujiendesha.
- Kwamba kukosekana kwa dawa kunasababisha usumbufu mkubwa kwa wagonjwa
- Kwamba tatizo la kukosekana kwa dawa linaweza tatuliwa mara moja kwa kutoa mikopo kwa vituo hivi vya afya ili viweze nunua dawa za kutosha kuwafanya wateja wao wasiende kuchukua dawa nje ya hospitali.
- Kwamba hospitali inaweza kuwa na dawa zote zilizopo kwenye soko, bila kujali sababu zinazochangia manunuzi kama uhitaji wa mara kwa mara n.k.
- Kwamba ubora wa dawa unafanana, hakuna nia ya kuwa na alternative brand
- Kwamba serikali yenyewe ipo juu ya mikono ya sheria na inaweza vunja mikataba waliyoingia NHIF na maduka ya madawa bila kuwa na madhara yoyote.
- Kuwa imekuwa ikitoa bajeti hewa za dawa.
- Kwamba asilimia 99 ya matatizo ya ukosefu wa dawa inayasabisha yenyewe na sheria zake za manunuzi
- Kwamba serikali huwa haikiri mapungufu yake katika kuchangia upatikanaji wa dawa endelevu ndani ya vituo
- Imewaambia MSD kama hospitali zake zimeenda kununua dawa na dawa huziko hazipo, basi itabidi wajieleze kwa nini dawa husika hazipo, na hii kuifanya MSD kutotoa vibali vya out of stock ili kuruhusu hizi hospitali za Serikali kwenda kununua dawa kwa washitiri na kuendelea kutoa huduma.
- Inasingizia sana upotevu wa dawa kama ni chanzo kikubwa cha dawa kutokuwapo hospitalini.
- Kwamba Serikali malengo yake makuu ni kusimamia utoaji huduma bora za afya na si kutengeneza ushindani na maduka ya dawa.
- Kwamba Serikali yenyewe haifanyi biashara kwenye afya, ndio maana, mishahara ya watumishi wa afya inatoka kwenye kapu kuu, ila hawa wenye maduka mishahara yao inatoka kwenye mauzo hayo hayo yatokayo kwenye maduka
- Haya maduka ya dawa yaliingia mikataba ya kisheria na NHIF kutoa dawa
- Kwamba watapoteza ajira katika sekta binafsi.
Nini kitatokea
- Hakuna hospitali itaweza kuwa na dawa zote, hakuna. Kama itaweza basi kuna dawa nyingi zita expire, kwa sababu ama zina shelf life fupi au zina matumizi madogo.
- Wagonjwa wengi wataanza malalamiko pale watakapokuwa wanasubirishwa kupata dawa wanayotaka wao ambayo haipo hospitali (maana hospitali itabidi ikanunue dawa haraka ili kumpa mgonjwa husika.
- Wizara itashindwa vibaya na kurejesha utaratibu wa nyuma
Maoni
- Serikali isiwaonee donge wenye maduka ya dawa, kama inaona wanapata faida kubwa isimamie na kurekebisha sheria zake za manunuzi, na kuondoa vyanzo vya ukosefu wa dawa katika vituo vyake. Hii tu itaondoa maduka ya dawa.
- Serikali iondoe imani ya kuwa sekta binafsi ni mshindani, wakati huohuo inataka mamilioni ya Watanzania wajiajiri wenyewe.
- Watumishi waliopo wizarani wawe na historia ya kufanya kazi vituo vya afya, kuna watu toka waanze kazi wapo kwenye uongozi, hawajui jinsi vitu viendeshwavyo mahospitalini na bado wanapewa nafasi za kufanya maamuzi magumu kuhusu hospitali.
- Serikali ifanye maamuzi kwa kuonesha inaheshimu sheria kwa kupitia mikataba iliyopo kabla ya kufanya maamuzi makubwa. Kutojali huku kumefanya tuwe wahanga hasa kwenye mikataba ya kimataifa