Serikali yazuia mjadala wa Richmond | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Serikali yazuia mjadala wa Richmond

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by BAK, Feb 13, 2009.

 1. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #1
  Feb 13, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,804
  Likes Received: 83,182
  Trophy Points: 280
  ‘Janja’ ya serikali yazuia mjadala wa Richmond

  • Sheria yawakuta wabunge wakiwa hawajajiandaa

  na Charles Mullinda, Dodoma
  Tanzania Daima~Sauti ya Watu​

  MKUTANO wa 14 wa Bunge, ulimalizika jana huku serikali ikifanikiwa kuzima mjadala wa maazimio 23 ya Bunge yanayohusu hatua ilizochukua baada ya kubainika kwa matatizo makubwa katika mkataba ulioipa ushindi wa zabuni ya kuzalisha umeme wa dharura Kampuni ya Richmond Development LLC.

  Kuzimwa kwa mjadala huko kumewezeshwa na hatua ya serikali kuamua kumfungulia mashitaka, mkurugenzi wa kampuni hiyo akituhumiwa kuisababishia serikali hasara.

  Akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa maazimio hayo bungeni jana, Waziri Mkuu Mizengo Pinda, alisema anafanya hivyo akitambua kwamba, Kanuni ya Bunge namba 64 (1) (C) toleo la mwaka 2007, inalizuia Bunge kujadili au kuzungumzia jambo linalosubiri uamuzi wa mahakama.

  Akinukuu kanuni hiyo, Pinda alisema: ‘‘Bila ya kuathiri masharti ya Ibara ya 100 ya Katiba yanayolinda na kuhifadhi uhuru wa mawazo na majadiliano katika Bunge, mbunge hatazungumzia jambo lolote linalosubiri uamuzi wa mahakama.”

  Alisema kwa msingi huo na kwa uelewa wake, ameona ni vema kutoa maelezo ya jumla kuhusu mchakato wa mashauri yaliyopo katika mahakama yanayohusisna na mikataba baina ya TANESCO na Richmond.

  Akizungumza kuhusu maazimio yaliyokwisha kutekelezwa na serikali alisema, Septemba 2008 alilifahamisha Bunge kuwa, mchakato wa utekelezaji wa maazimio 10 kati ya 23 ulikuwa umekamilika.

  Alisema tangu wakati huo mpaka sasa, maazimio mengine mawili, namba 17 na 18, yamekamilika ambayo ni kufutwa kwa Kampuni ya Richmond Development kutoka kwenye orodha ya makampuni halali nchini na wamiliki wa kampuni ya Richmond kufikishwa mahakamani ili wafunguliwe kesi ya jinai kwa udanganyifu na ujanja wa kuiibia serikali.

  Akizungumzia hatima za waliokuwa mawaziri wa Nishati na Madini kwa nyakati tofauti, Nazir Karamagi na wa kabla yake, Dk. Ibrahim Msabaha, ambao walitajwa katika maazimio hayo, Pinda alisema tayari taasisi za dola ziko katika hatua ya mwisho kukamilisha uchunguzi wa tuhuma zao kabla ya kufikishwa mbele ya vyombo vya sheria au la.

  Hata hivyo alisema katika azimio namba 14 lililotaka wanasiasa hao wawajibike, alisema tayari walikuwa wameshajiuzulu nyadhifa zao za uwaziri tangu Februari mwaka jana.

  Alisema pamoja na hatua hizo, serikali iliona ni busara vyombo vya dola vifanye uchunguzi zaidi kwa lengo la kujiridhisha kama kulikuwa na utovu wa maadili katika kushughulikia mchakato wa zabuni hiyo au la.

  Kuhusu azimio namba tano, saba, tisa na 14 pia alisema maudhui yake yanafanana kwa sababu yanaitaka serikali kuwawajibisha watumishi wote wa umma waliohusika katika mchakato wa mkataba huo wakiwemo wale wa TAKUKURU ambao walifanya uchunguzi kuhusu suala hilo.

  Alisema mamlaka za nidhamu zinazohusika na watumishi hao wa umma, zimekamilisha uchambuzi wa maelezo ya utetezi yaliyotolewa na kila mtumishi aliyeshiriki kwenye mchakato wa zabuni hiyo.

  Alisema uchunguzi kuhusu watumishi hao unaendelea na ushauri wa vyombo vya dola vya uchunguzi ndio utakaowezesha serikali kuona ni watumishi gani wanaostahili kuingia kwenye mchakato wa kuchukuliwa hatua za kinidhamu na wale watakaoonekana kutenda makosa ya jinai kuchukuliwa hatua zinazostahili.

  Tanzania Daima ambayo tangu mwanzoni mwa wiki hii iliuona mwelekeo wa jambo hilo kutojadiliwa bungeni kutokana na uamuzi wa serikali kulipeleka mahakamani ilipowasiliana na wabunge kadhaa, wote walionyesha kuwapo kwa fursa ya kuendelea nalo.

  Mbunge wa Kyela, Harrison Mwakyembe (CCM), aliyekuwa Mwenyekiti wa Kamati Teule ya Bunge iliyochunguza sakata la Richmond na kuwasilisha taarifa iliyosababisha kujiuzulu kwa aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Lowassa, Karamagi na Msabaha, alipoelezwa na mwandishi wetu Jumatatu wiki hii kuhusu utata wa kujadiliwa kwa suala hilo, alisema tayari serikali ilikuwa imeshawasilisha kwa kamati ya Bunge hoja zake kuhusu ilivyotekeleza maazimio ya Bunge.

  Mwelekeo huo huo wa kuwapo kwa matumaini ya kuwapo kwa mjadala huo, ulionyeshwa pia na Mbunge wa Karatu, Dk. Wilbrod Slaa (CHADEMA), ambaye naye aliieleza Tanzania Daima kwamba hoja hiyo ya Richmond ilikuwa ni lazima ijadiliwe.
   
 2. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #2
  Feb 13, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,804
  Likes Received: 83,182
  Trophy Points: 280
  Bunge limekuwa likiingilia mahakama kwenye mambo mbali mbali kama inavyooshesha katika hii article hapa chini na kauli ya Sitta kwamba, "Kama naingialia mahakama potelea mbali."

  Lakini inapokuja kwenye kujadili maamuzi mbali mbali yenye ufisadi na yanayohatarisha maslahi ya nchi yetu kama Masha kuingilia mchakato kuhusiana na vitambulisho vya urai na hatua zilizochukuliwa na serikali ili kutimiza mapendekezo ya kamati ya Mwakyembe basi Bunge ndiyo bunge linakuwa halioni umuhimu wa kuingilia mahakama!!!!!

  Waungwana mimi sina imani tena na Bunge letu maana limeweka mbele maslahi ya CCM badala ya yale ya Taifa. Mkiangalia maswala yote mawili haya yana maslahi kubwa kwa nchi yetu lakini Pinda na Sitta kwa kujua athari kubwa za majadiliano hayo kwa uongozi wote wa CCM uliokuwa madarakani umeamua kuwanyima Wabunge uhuru wa kujadili maswala haya mawili yenye uzito mkubwa. Shame to both you Pinda and Sitta.  Sitta amcharukia Jaji Mkuu

  Stella Nyemenohi, Dodoma
  Daily News; Monday,February 09, 2009 @20:04

  Wakati Bunge likitarajiwa leo kujibu kauli ya Jaji Mkuu Augustino Ramadhan aliyoitoa wiki iliyopita kuwa chombo hicho kimekuwa kikiingilia mahakama, Spika Samuel Sitta amesema malalamiko yaliyotolewa na jaji hayawezi kunyamaziwa. Amesema Bunge kama taasisi, haliwezi kukaa kimya kwa kuwa suala hilo ni la kikatiba.
  Akitoa taarifa hiyo bungeni leo mjini hapa, Sitta alionyesha kulaumu baadhi ya uamuzi ambao umekuwa ukitolewa na mahakama na kusema kwamba unatoa fursa kwa mtu mmoja kuliko jamii nzima, jambo linaloumiza. Alisema wao kama wabunge hawana nia mbaya na mahakama, lakini akatahadharisha kwamba chombo hicho cha sheria, hakina budi kuzingatia kwamba jamii inakiangalia.

  "Hapa watasema pia naingilia mahakama…potelea mbali," alisema Sitta bungeni hapo. Kwa mujibu wa kiongozi huyo wa Bunge, tamko la Bunge litatolewa kesho baada ya kipindi cha maswali na majibu. Akifafanua juu ya kile alichosema baadhi ya uamuzi kuegemea kwa mtu mmoja badala ya jamii, Sitta alitoa mfano kuwa Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Maji (EWURA) iliwahi kukifungia kituo kimoja cha mafuta kwa kuzingatia kanuni zake.

  Kwa mujibu wake, matajiri walikwenda mahakamani kupinga uamuzi huo ambao ulikubalika mahakamani na ikaamriwa kifunguliwe. Wiki iliyopita, katika maadhimisho ya Siku ya Sheria, Dar es Salaam, Jaji Mkuu licha ya kutaja Bunge kuingilia mahakama, vile vile alivionya vyombo vya habari kwa kile alichosema kwamba vimeshindwa kutofautisha kati ya maoni na ukweli.

  Katika hatua nyingine, Bunge leo jioni liliahirisha kikao chake baada ya Naibu Spika Anne Makinda kugundua kuwa hakuna mtu hata mmoja wa serikali.
   
 3. J

  Jujuman JF-Expert Member

  #3
  Feb 13, 2009
  Joined: Dec 7, 2008
  Messages: 248
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mkuu BUBU mimi naona hali hapa ilipo si mbaya kwani MAHAKAMA ndio mahali sahihi panapotatua matatizo na kutoa ADHABU kwa anaestahili nasote tunatuhumu kuwa kuna MAKOSA YA JINAI dhidi ya RICHMOND hivyo si swala la BUNGE bali la MAHAKAMA. tuamini kuwa sheria itatekeleza WAJIBU WAKE>
   
Loading...