Serikali yaziunganisha Benki za TPB na TIB Corporate na kuwa Benki moja ya Biashara

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,806
11,968


SERIKALI imziunganisha benki za TPB Bank Plc pamoja na TIB Corporate ili kuimarisha utendajikazi wa benki hizo na kuhimiri ushindani wa kibiashara kwenye sekta ya fedha.

Kauli hiyo imetolewa leo Jijini Dodoma na Msajili wa Hazina, Athuman Mbutuka alipokuwa akizungumza na vyombo vya Habari.

Aidha Mbutuka amesema kuwa Kufuatia uamuzi huo leo Juni Mosi mwaka huu, benki ya TPB itachukua mali na madeni ya benki ya TIB huku serikali ikisisitiza kulinda maslahi ya wafanyakazi wote kwenye benki hizo.

Mbutuka amesisitiza kuwa maslahi ya wenye amana na wateja wote yatalindwa kwa mujibu wa sheria, kanuni na taratibu za usimamizi wa benki na taasisi za fedha.

“Serikali imeendelea kuchukua hatua mbalimbali ili kuboresha utendaji wa mashirika na taasisi za umma ikiwemo kuunganisha taasisi zinazotekeleza majukumu yanayofanana kwa lengo la kuongeza ufanisi na kupunguza gharama za uendeshaji,” ameeleza Mbutuka.

Mbutuka ameongeza kuwa serikali imechukua uamuzi huo kwa lengo la kuleta mageuzi makubwa ya kiutendaji, kimfumo, kimuundo na kitaswira ili benki iweze kuhimili ushindani kwenye sekta ya fedha nchini

Mbutuka amehitimisha kwa kuwatoa hofu wateja wa benki wa TPB na TIB wataendelea kuhudumiwa kwenye matawi yao ya sasa hadi hapo watakapotaarifiwa vinginevyo na huduma za kibenki hazitaathirika kwa vyovyote kutokana na mabadiliko hayo.
 
Tulikuwa tunajua toka zamani. Ni mpango w Magu kuiba pesa ndefu. Na tender nyingi zitakuwa zinapitia hapo.

Crooks are leading the country what do you expect?

Hata NMB hawatalipa salary tena. Hii bank ndio italipa . mtegemee vipigo kwa lend mbele. Doto ndio master mind akipoke maelekezo from Chato regime
 
... idea nzuri kivipi wakati benki ya biashara ya serikali (NBC) ilikuwepo ikauwawa na serikali? Ni nini kipya ambacho benki hii mpya itakuja nacho ambacho NBC ilishindwa?
Wait and see,au tupe idea yako kidogo,sio kupinga tu vitu bila hoja...
 
Back
Top Bottom