Serikali yazitaka shule binafsi kutoongeza ada na vilevile watoto warudi shule Juni 29 kama ilivyopangwa

Influenza

JF-Expert Member
Jul 1, 2018
1,445
3,402
EbbMxjjWkAYoJEx.jpg

EbbG7I5XsAA6i9D.jpg
 
Hapo kwenye kusema hela ya mishahara kwa walimu hata kipindi cha kufunga shule ndo wazazi walipe bado nahoji.
Shule nyingi ziliwasimamisha(likizo ya bila malipo) walimu wake kabisa.Maana kwamba ndo imetoka hivyo.
Kama wazazi watalazimiwa kulipa hiyo hela basi haki itendeke kwa hao walimu mana wengine walifukuzwa kabisa baada ya kudai haki zao na wengine watarudi ila mishahara ya mwezi wa 4,5 na 6 hawajalipwa.
 
Ndio wameeeleza nini hapa sasa? Mbona hawataki kuwa wazi? Wanaandika Kwa kujificha ficha hata huelewi uamzi wao ni upi
 
Mara wapokelewe pasipo vikwazo Wakati wanajua kuwa vikwazo ni Ada, huku wanasema wazazi walipe Ada sasa huuyu kaandika nini? Katatua nini? Si ameongeza utata? Anazungumzia nyongeza, hiyo nyongeza ni ipi? Kwa nini huyu alieandika hii barua asijiuzuru? Maaana barua haieleweki imetatua nini
 
Mara wapokelewe pasipo vikwazo Wakati wanajua kuwa vikwazo ni Ada, huku wanasema wazazi walipe Ada sasa huuyu kaandika nini? Katatua nini? Si ameongeza utata? Anazungumzia nyongeza, hiyo nyongeza ni ipi? Kwa nini huyu alieandika hii barua asijiuzuru? Maaana barua haieleweki imetatua nini
Pole mkuu naiona jazba yako dhidi ya wamiliki wa mashule hasa ukirejea na uzi wako, kimsingi wameelekeza ada ilipwe kulingana na makubaliano yaliyokuwepo mwanzo wa mwaka. Pasiwepo na nyongeza ya aina yoyote ile. Na kwa upande wa wazazi wameaswa kulipa bila kulalamikia siku ambazo watoto hawajaenda shule. Ila kwa michango ya chakula na nauli imeachwa kuwa busara ya body za shule husika zijadili.
 
Nadhani hii barua imejificha. Yaan iko katikati ya barabara.

Inajaribu kuwaambia wamiliki wa shule kua wasije kugoma kuwapokea watoto ambao hawajalipa ada ili wahudhurie masomo ya muhula huu na ujao.


Kingine anawaasa wazazi kulipa. Kibongo bongo ni kwamba wazazi hawatolipa wakijua watoto wao watapokelewa tu. Ndo maana wameandika kwa herufi kubwa "WAPOKELEWE"
 
  • Kicheko
Reactions: rr3
Mmh shule nyingine zimeamuru ada zote zilipwe za kuanzia mwezi April hadi sasa.
 
Back
Top Bottom