Serikali yazitaka mamlaka za maji kuwarejeshea huduma waliokatiwa ili waweze kukabiliana na Corona

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
31,246
2,000
Naibu waziri wa maji Mh. Awesu amezitaka mamlaka za maji kuwarejeshea Huduma wale waliokatiwa na kisha kuwawekea utaratibu wa kulipa polepole.

Mh Awesu amesema wakati huu wa janga hili la Corona kila mtu anapaswa kuwa na maji ya uhakika ili kuweza kukabiliana nalo.

Source: Clouds tv!

=====

Wizara ya Maji imeiagiza Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (Ewura), kuwarejeshea huduma za maji wateja wote nchini waliokatiwa huduma hiyo kwa makubaliano

Lengo ni kuwawezesha kupata huduma hiyo katika kipindi hiki cha mapambano dhidi ya maambukizo ya ugonjwa wa COVID 19), ambao unasababishwa na virusi vya corona.

Aidha, Ewura kuhakikisha inadhibiti bei za ankara ya maji nchini zinazopandishwa kiholela na kubambikiwa wateja zinazofanywa mamlaka za maji nchini bila kupata kibali kutoka Mamlaka hiyo sambamba na kutoa elimu kwa wananchi.

Agizo hilo lilitolewa jijini hapa jana na Naibu Waziri wa Maji, Juma Aweso, wakati akizungumzia masuala mbalimbali na menejimenti ya Ewura, yakiwamo malalamiko ya ankara kubwa za maji zinazotolewa kwa wateja.

Alisema taifa liko katika mapambano na vita dhidi ya corona, hivyo jambo muhimu ni kuchukua tahadhari na kuzingatia maelekezo yanayotolewa na wataalamu.

Aweso alisema silaha pekee ya kukabiliana na maambukizo ya virusi hivyo ni maji tiririka na kunawa kwa sabuni.

Alisema kutokana na umuhimu wa maji, anaagiza wateja wote waliokatiwa maji warejeshewe kisha Uwura iweke utaratibu mzuri wa kulipa madeni yao.

Alisema licha ya mambo mazuri na kazi kubwa inayofanywa na Mamlaka hiyo, bado kuna matatizo na changamoto ambazo zinahitaji kupatiwa ufumbuzi ili kutoa huduma bora kwa wananchi na hasa masikini.

Alieleza kuwa, zipo mamlaka za maji ambazo ni vinara kwa kuwabambikia na kuwapandishia wananchi bei za maji kiholela, hivyo aliiagiza Ewura kuhakikisha inafikisha ripoti ya mamlaka za aina hiyo wizarani ili kuzichukulia hatua stahiki, kwa kuwa wizara ndiyo yenye mamlaka ya mwisho.

Kadhalika, aliwataka watumishi wa Ewura kutoa elimu kwa watumiaji wa maji, juu ya wajibu na haki yao, hatua aliyosema itasaidia kuondoa malalamiko tofauti na sasa ambapo wateja wanapata haki ya kutumiwa ankara kwa njia ya simu bila ushirikishwaji.

Alifafanua zaidi ya kuwa kazi ya Ewura si kusimamia ankara pekee, bali ina wajibu wa kusimamia ubora wa maji ambayo lazima yawe safi na yenye ubora.

Kaimu Mkurugenzi wa Maji na Usafi wa Mazingira, Titus Safari, alisema Ewura, imetoa jumla ya leseni 119 katika kipindi cha Juni 2019.

Alisema, imekuwa ikifanya ukaguzi kwa mamalaka za maji nchini zisizopungua 50, na kutoa maelekezo ya kuboresha na kuongeza ufanisi katika kutoa huduma Bora kwa watumiaji wa maji.

Naye Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Ewura, Godfrey Chibulunje, alisema maagizo yote yanayotolewa na wizara, likiwamo kurejesha huduma ya maji kwa waliokatiwa huduma watayafanyia kazi haraka iwezekanavyo.

IPP Media
 

Zero Hours

JF-Expert Member
Apr 1, 2011
11,980
2,000
Mwezi uliopita bili ilikuja tarehe 2. Maji wakaja kufunga tarehe 8. Kufatilia Mwawasa wakasema tumechelewa tulitakiwa kulipa ndani ya wiki ya kwanza. Tukapigwa fine ya 15000. Na bili ilikuwa ni 8000 tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom