#COVID19 Serikali yazindua mpango wa Chanjo tembezi kwa Wananchi wanaohitaji

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,500
9,279
SERIKALI imezindua mpango wa jamii shirikishi na harakishi wa chanjo dhidi ya UVIKO-19 wenye mambo 10 ikiwamo kuwapo kwa chanjo tembezi (mobile vaccination site) na kuwafuata wananchi walio tayari kuchanjwa kwa hiari.

Mpango huo ulizinduliwa jana na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee, Dk. Dorothy Gwajima, kwenye mkutano mkuu wa mwaka wa waganga wakuu wa mikoa na halmashauri uliofanyika jijini hapa.

Akitoa maelezo ya mpango huo, Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Prof. Abel Makubi, alisema mpango huo unalenga kuongeza vituo vya kuchanja kutoka 550 hadi 6,784, kuharakisha wananchi kuchanjwa mapema.

“Kwenye chanjo tembezi magari tumeshaagiza na nimeagiza tangu juzi, taasisi zetu na halmashauri zitoe magari kwa ajili ya kutekeleza huu mpango, nimesikia baadhi ya wakurugenzi wanasuasua kutoa magari, MSD na Mpango wa chanjo wametoa, TB bado hawajatoa, huu ni mpango wa kitaifa, nataka yatoke ndani ya saa 24 zijazo kwa taasisi zote ambazo bado,” alisema.

Alisema utasimamiwa na wakuu wa mikoa, Makatibu Tawala wa Mikoa na Waganga Wakuu wa Mikoa.

“Ni mwezi sasa tangu Rais Samia Suluhu Hassan azindue utoaji chanjo ambapo watu zaidi ya 350,000 hadi sasa wamechanja, bado tunahitaji wananchi wachanje mapema iwezekanavyo kutokana na asili ya ugonjwa wenyewe,” alisema.

Alisema ugonjwa huo ni wa mlipuko na unasambaa haraka na uchanjaji ni njia pekee ya kupunguza maambukizi ya ugonjwa huo.

Alibainisha kuwa vikundi, viongozi wa kijamii na serikali za mitaa ndiyo muhimili wa kuhamasisha chanjo mijini na vijijini.

“Mpango huo pia unalenga elimu itatolewa kupitia njia za asili za ngoma, kwaya, muziki, maigizo, semina, mikutano na pia TV na redio jamii, kutumia pia viongozo wa serikali, kijamii, kidini, wabunge, wasanii, watu maarufu, wataalamu, wawakilishi wa vikundi vya kijamii kama vile Vicoba,” alisema.

Alisema kila halmashauri itakuwa na lengo la kufikia kwa muda maalum utakaopangwa na kuwafuata wananchi walio tayari kuchanjwa bila wao kulazimika kwenda vituoni.

Kwa upande wake, Katibu Mkuu TAMISEMI, Prof. Riziki Shemdoe, alisema lengo la mpango huo ni kuharakisha utoaji chanjo kwa kuwa hadi sasa haujafikia nusu ya chanjo zilizoletwa zaidi ya milioni moja.

“Tutakutana na wakuu wa mikoa na timu mbalimbali kama sehemu ya uraghabishi na kupata nafasi ya kutoa ufafanuzi wa hoja mbalimbali, RMO utahitajika kufanya hili, tutatumia redio za kijamii,” alisema.

Aliwataka waganga hao kufuatilia matumizi ya fedha za mpango huo na kutoa taarifa ya matumizi yake kwake na fedha zitapelekwa wiki ijayo kwa Wakurugenzi wa Halmashauri kwa ajili ya kazi hiyo.


Ippmedia
 
Iinaenda kua kama ishu ya nyonya damu
Wakifika mtaan watu wanatoka nduki

Mashuleni ndo usiseme saaa
 
Mikopo imeanza kufanya kazi ya kupambana na Corona
Matajaza mafuta kwenye gari za Halmashauri bila kupata matokeo Chanya.
Kampeni mmezindua wenyewe Jana
 
Hii itakua kama ishu ya nyonya damu watu wakiona magari wanatoka nduki.

Shuleni ndo kabisaaa wasifike
 
Isijekuwa kama dawa ya kuua mbu majumbani watu wakaanza kukamatwa kwa lazima na kuchanjwa kama wanyama.
 
Naomba ratiba kamili ya vituo vya kuchanja chanjo ya Corona ili nisaidie kuhamasisha jamii ijitokeze kuchanja na kujilinda ili kutokomeza ugonjwa hatari wa Corona 19
 
Siamini kama shelf life ya hii jonson and jonson haijaisha hasa ukichukulia mazingira ya uhifadhi hapa bongolala......haishangazi watu kuanza kufuatwa hadi uvunguni.
 
Ina maana wafuasi wa chadema hawafiki milioni moja aiseeee

Mijamaa ilikua na mapovu ile kisa hakuna chanjo
 
Siamini kama shelf life ya hii jonson and jonson haijaisha hasa ukichukulia mazingira ya uhifadhi hapa bongolala......haishangazi watu kuanza kufuatwa hadi uvunguni.
Ni miezi mitano tangu zilipopokelewa nimesikia zitakua tayari
But soo far bado
 
ATUCHANJI ATUCHANJI ATUCHANJI ATUCHANJI ATUCHANJI ATUCHANJI KM NI MUHIMU TUNGELIPIA SIO KUPEWA BURE MBONA MATIBABU MENGINE TUNALIPA HUO UPENDO UPO KWENYE CORONA TU.
 
Back
Top Bottom