Serikali yazindua kituo cha Tehama Chato

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,877
6,326
1575870025941.png

Serikali imesogeza huduma za mawasiliano kwa wananchi wa Chato kwa kuzindua kituo cha Tehama, Telesenta Chato mkoani Geita baada ya kukamilisha usimikaji miundombinu ya mawasiliano kituoni.

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Isack Kamwelwe jana alizindua kituo hicho cha Tehama ambacho kimejengwa na Halmashauri ya Wilaya ya Chato.

Aliipongeza Halmashauri ya Wilaya ya Chato kwa ubunifu wao kwa kujenga kituo cha Tehama kwa lengo la kuhakikisha kuwa wananchi wanapata huduma za mawasiliano katika maeneo wanayoishi

“Hongereni kwa ubunifu huu wa kujenga kituo hiki na kumvutia Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), James Kilaba kuja kusimika miundombinu ya mawasiliano na kuweka vifaa vya Tehama na huduma ya intaneti. Sasa wananchi wa eneo hili watanufaika,” alisema Kamwelwe.

“Kupitia kituo hiki, wafanyabiashara watapata bei za bidhaa mfano kukiwa na mnada wa ng’ombe, utapata bei za sehemu mbalimbali nchini na nchi nyingine na kuuza ng’ombe kwa bei ya soko,”alisema.

Alisema serikali kupitia kituo hicho itatoa huduma za mawasiliano vijijini kama ilivyo kituo cha Chato ili kuhakikisha huduma za mawasiliano zinapatikana na maeneo ya vijijini na sio maeneo ya mijini pekee.

Alitoa wito halmashauri nyingine kuiga mfano wa Chato kujenga vituo vya Tehama kuhakikisha ujenzi wa vituo hivi unaendelea maeneo mengine kuongeza upatikanaji huduma za mawasiliano kwa wananchi.

Akimkaribisha Waziri, Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Mawasiliano), Dk Maria Sasabo alisema serikali imejenga Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano unatoa huduma za mawasiliano nchi nzima na itawawezesha wananchi wa Chato kuwasiliana kupitia kituo hicho kwani dunia imekuwa kijiji kutokana na ukuaji wa Tehama na kuongezeka huduma za mawasiliano.

Mkurugenzi Mkuu wa TCRA, James Kilaba alisema wamegharamia ununuzi wa vifaa vya Tehama na kompyuta 20 na betri 20 za kutunzia umeme kwa muda, kichapishi moja, mashine za kivuli moja, skana moja, binding mashine moja, lamination machine moja, runinga moja na kisimbusi ambacho kimelipiwa mwaka.

Chanzo: Habari Leo
 
Kupitia kituo hiki, wafanyabiashara watapata bei za bidhaa mfano kukiwa na mnada wa ng’ombe, utapata bei za sehemu mbalimbali nchini na nchi nyingine na kuuza ng’ombe kwa bei ya soko,”alisema.

Hii si inaweza kupatikana hata kwenye simu ya kiganjani?
 
Hicho kituo kimejengwa kwa kutengewa hela na maelekezo toka juu..wanasema halmashauri nuingine nazo ziige wazo hilo kwa kujenga vituo vya Tehama !! Thubutuuu hela wapate wapi ?
 
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Isack Kamwelwe jana alizindua kituo hicho cha Tehama ambacho kimejengwa na Halmashauri ya Wilaya ya Chato.

Aliipongeza Halmashauri ya Wilaya ya Chato kwa ubunifu wao kwa kujenga kituo cha Tehama
kwa lengo la kuhakikisha kuwa wananchi wanapata huduma za mawasiliano katika maeneo wanayoishi

Wengi wa waliokwisha tangulia kuweka comments zao wanaruka kuzisoma kwa uzuri hizi paragrafu mbili...
 
Kuna wilaya imeshawahi kujengwa kituo cha namna hii?au ndio cha kwanza
 
beth,
Hv ule uwanja wa taifa wa mpira wa chato umefika wapi jmn? Africa Africa yaan next tym tutafute Rais Mzungu atutawale maana kuna shida sana
 
Back
Top Bottom